Graduate wa UDSM huwa anajiamini popote pale

Levels baby

JF-Expert Member
Sep 26, 2019
831
768
Naandika kwa ufupi.

Nimefanya kazi katika kampuni mbalimbali kabla ya kuingia serikalini na kuwa mtumishi wa Umma ambaye mwakani naachana na kazi hii niifanyayo na kuwa mjasiriamali huko Tukuyu Mbeya mana baada ya research ya kutosha nataka nikapande zao la maparachichi.

Pia hali ya hewa ya kule imenivutia (kama upo Japan) kuwekeza tofauti na kwetu Dodoma.

Turudi kwenye mada. Jana nikiwa kwenye shughuli za kikazi nimekutana na vijana wanne ambao ni wageni kidogo ofisini kwetu.

Sasa katika kuwahoji na kuongea nao kwa urefu nikagundua mmoja anajiamini sana na ana uwezo wa kuongea nami kwa u-serious sana ingawa ni boss wake. Nilipomuuliza historia yake akanijibu kuwa chuo kasoma UDSM, palepale nika-note kutokana na;

1. Mimi ilikuwa nikienda kwenye interview nilikuwa najaribu kuongea sana na wenzangu kujua background zao pale nikijua wametoka vyuo vingine huko sijui IFM sijui UDOM basi najua tu hii kazi yangu mana nakuwa na confidence ambayo hawana.

2. Pia mwanafunzi yeyote wa UDSM lazima awaone wenzie viazi mahali popote anapokutana nao na lazima awaoneshe kuwa ametoka chuo kikubwa katika nchi hii.

NB: Mwanafunzi uliesoma UDSM yeyote na popote ulipo usikubali kupitwa na wengine waliosoma vyuo sijui gani gani huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom