Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,176
Ninawasikitikia sana vijana wa Tanzania. Vijana wanaotokea familia masikini, mafukara ambao wazazi wao wanaishi kwenye nyumba za tembe na kulala kwenye vitanda vya ngozi za ng'ombe.
Vijana wamejaaliwa vipaji vya elimu. Wazazi wao (wanaoshabikia CCM kwa sababu wanafikiri Nyerere bado yupo hai) wamejikamua kuuza mifugo na mazao wapate elimu. Baadhi ya vijana hawa wamepata bahati ya kufika vyuo vikuu na kupata shahada na stashahada. Wapo mijini. Hawataki kurudi vijijini kwa sababu vijijini hakuna umeme. Vijijini hakuna zahanati na hospitali. Vijijini hakuna lami. Vijijini hakuna daladala wala taxi. Wala vijijini hakuna warembo kama huku mjini. Vijini kupata netweki ya simu ni ishu. Vijijini kuchaji simu mpaka ulipie sh. 500 kwa mtu mwenye jenereta.
Mmmh! Vijana. Wasomi. Wanafanya mambo ya aibu. Wanakula takrima za CCM na kufanywa makamanda wa Green Guard. Wanafanya kazi ya kuratibu ugawaji wa fulana na kofia za CCM. Wanasafirishwa kwa malori na wengine kupoteza maisha kwenye ajali kwa ajili ya kuwatumikia mafisadi, wakati watoto wa mafisadi wako Upanga wanagombania rimoti za TV na kupunguza/kuongeza ubaridi wa viyoyozi.
Vijana masikini wa Tanzania wamesahau shida walizonazo wazazi wao. Wamesahau kuwa CCM na watawala wake wanaokula rushwa ndiyo chanzo cha matatizo yote ya nchi hii.
Tanzania inawalilia enyi vijana kutoka familia masikini za Tanzania. Jitengeni na CCM. Waacheni watoto na ndugu zao ndiyo wawe wapambe wao kwenye mikutano yao. Jiungeni na kundi la ukombozi.
Wakati ni huu. 2015 ni kesho tu.