Graduate, mshahara chini ya milioni moja usifanye kazi

Kua Uyaone Nilidhani ni Maghorofa.
Hata mimi nilikua kama wao, sasa hivi hata nikipata kazi ya elfu 60 kwa mwezi napiga.

Nisaideni.
 
Nilikuwa na ndoto za aina nyingine kabisa, mtu asiingie akilini kwangu manake atakimbia
 
Ni haki yao jamani...acheni wajipe moyo sababu kiuweli wakiujua uhalisia wa huku mtaani tutawakatisha tamaa na wataona shule haina faida kama ilivyofkikirika kipindi cha nyuma,naamini wengi tulishawaza hivyo na ilikuwa inatupa morale ya kusoma kwa bidii,ukiona harbody njiani unasema mi nkipata kazi ntachkua Volkswagen double cabin kali kuliko hardbody!..ndo hivyo,mambo hayako ivyo...laki tano, sita...budget yako ya mwezi laki tano una save laki kwa mbinde na lawama kibao toka kwa wadau wa karibu na ndugu...shit aint as t seems to be!
 
Shida vijana wengi wakituona tuko makazini tunasema maisha magumu wanatuchukulia kuwa sisi ni form 4 leavers wakati watu tuko na hizohizo degree zao na vyuo vya maana ila system ndo inabana, kila la kheri na ndoto zao labda watafanikiwa
 
Baada ya shule kuajiriwa......! Not true
Baada ya shule ni kazi nasi ya kuajiriwa kw 1m huku assignment, test na ue nikutafuta pesa karibuni mtaan ndo wajue sometime hata hiyo buku unaisotea
 
Mi nakumbuka jaman nilikaa hom 2 years jobless baada ya kumaliza chuo hadi nikafukuzwa nyumbani nikionekana km mtu nisiye na faida kabisa yaani ilibaki kidogo tu niwe mwendawazim kwa stress!! lol dat moment is unforgetable maana cku nilipopata kazi ya kulipwa laki tatu tu mi niliona km utajiri ndo inaninyemelea vile niliionaje kubwaaa
 
Tusiwahukumu tu jamani, hatujui wamesomea nini na ngazi gani. Mleta mada amehisi tu, labda wamesomea kitu tofauti pia
 
Leo nilikua nimeongozana na vijana flani kutokea wizara ya elimu kama unaenda chuo cha usimamizi wa fedha/makumbusho ya taifa.

Walikua mbele yangu kidogo ila nilikua nasikia mazungumzo yao(inaonyesha ni wanafunzi wa ifm). Mwenzao ukawa anawambia wenzake kua yeye kama akigraduate mshahara anaotaka ni kuanzia milioni moja chini ya hapo hafanyi kazi. Tena akawa anashangaa kusikia eti graduate analipwa laki 6.

Akasema vinginevyo ataenda jeshini maana huko graduate analipwa milioni 1.5. Wenzake pia wakawa wanamuunga mkono bila hiyo hela bora waache kazi.

Inaonekana vijana wakiwa mashuleni wanadanganyana sana,wanapeana matumaini makubwa ambapo wakija mtaani wakakuta hali ni tofauti wanaishia kua wezi na uuzaji wa dawa za kulevya. Malizeni shule muje mkutane na mshahara wa laki 2 na digrii zenu ndio mtakoma. Acheni kudanganyana,mtaani hakuko hivyo.

chuo kinawadanganya. Wengine wapo mitaani hata hiyo laki mbili wanaisikia kwenye bomba na digree zao.
 
Mi nakumbuka jaman nilikaa hom 2 years jobless baada ya kumaliza chuo hadi nikafukuzwa nyumbani nikionekana km mtu nisiye na faida kabisa yaani ilibaki kidogo tu niwe mwendawazim kwa stress!! lol dat moment is unforgetable maana cku nilipopata kazi ya kulipwa laki tatu tu mi niliona km utajiri ndo inaninyemelea vile niliionaje kubwaaa

Usiseme best. Mimi miaka nane napiga vibarua vya hadi sh elfu tano
 
Back
Top Bottom