Graduate, mshahara chini ya milioni moja usifanye kazi

Mfukua Makaburi

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,334
2,000
Leo nilikuwa nimeongozana na vijana flani kutokea wizara ya elimu kama unaenda chuo cha usimamizi wa fedha/makumbusho ya taifa.

Walikua mbele yangu kidogo ila nilikuwa nasikia mazungumzo yao (inaonyesha ni wanafunzi wa IFM). Mwenzao ukawa anawambia wenzake kua yeye kama akigraduate mshahara anaotaka ni kuanzia milioni moja chini ya hapo hafanyi kazi. Tena akawa anashangaa kusikia eti graduate analipwa laki 6.

Akasema vinginevyo ataenda jeshini maana huko graduate analipwa milioni 1.5. Wenzake pia wakawa wanamuunga mkono bila hiyo hela bora waache kazi.

Inaonekana vijana wakiwa mashuleni wanadanganyana sana, wanapeana matumaini makubwa ambapo wakija mtaani wakakuta hali ni tofauti wanaishia kuwa wezi na uuzaji wa dawa za kulevya. Malizeni shule muje mkutane na mshahara wa laki 2 na digrii zenu ndio mtakoma.

Acheni kudanganyana, mtaani hakuko hivyo.
 
Ynaa

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
243
250
Maisha ya chuo mara nyingi hua ni fake life tena yenye expectation kubwa mnoo kushinda uhalisia!Ila akimaliza chuo na kurudi katika dunia halisi atajua maana ya mshahara wa laki!! Yani ukimaliza chuo na mzazi nae anaona ametua mzigo wa ada,sasa kazi ni kwako tu kusugua kiatu na vibahasha!! Wapiii upate kazi ya milioni tena fresh graduate!!
 
jubilant

JF-Expert Member
Feb 16, 2009
308
500
Leo nilikua nimeongozana na vijana flani kutokea wizara ya elimu kama unaenda chuo cha usimamizi wa fedha/makumbusho ya taifa.

Walikua mbele yangu kidogo ila nilikua nasikia mazungumzo yao(inaonyesha ni wanafunzi wa ifm). Mwenzao ukawa anawambia wenzake kua yeye kama akigraduate mshahara anaotaka ni kuanzia milioni moja chini ya hapo hafanyi kazi. Tena akawa anashangaa kusikia eti graduate analipwa laki 6.

Akasema vinginevyo ataenda jeshini maana huko graduate analipwa milioni 1.5. Wenzake pia wakawa wanamuunga mkono bila hiyo hela bora waache kazi.

Inaonekana vijana wakiwa mashuleni wanadanganyana sana,wanapeana matumaini makubwa ambapo wakija mtaani wakakuta hali ni tofauti wanaishia kua wezi na uuzaji wa dawa za kulevya. Malizeni shule muje mkutane na mshahara wa laki 2 na digrii zenu ndio mtakoma. Acheni kudanganyana,mtaani hakuko hivyo.

Nimecheka sana!!
Waache tu wanapata jeuri kwa sababu ya hivyo viboom vyao, wakimaliza shule watakutana na kanjbai, veve mimi iko kupa laki bili, ona said fanya kaji juri sana nampa laki nusu..
Wakikaa mtaani mwaka mzima unafikiri hayo mawazo ya 1.5m watakuwa nayo tena??
 
dizzle kiraka

JF-Expert Member
Aug 12, 2012
416
250
"Nkimaliza zangu Chuo ntaaplai zangu kazi Voda, ntalipwa milioni 3.5/mwezi, ntajibana zangu kila mwezi natumia laki5 tu, izo 3m naifaZi benki, baada ya miezi mi3 nanunua gari la 9m/=, nkishakua na gari basi 3m ya mwezi unaofatia napanga nyumba ya laki mbili na amsini kwa mwezi, 3m inayofatia nanunua fenicha, kwanza adi apo ntakuwa nshatimiza miezi 6 kazini, adi apo naruhusiwa kukopa, nakopa zangu 10m/= afu natafuta kiwanja cha 6m tu, si ntakuwa nakatwa 1m/= za mkopo kila mwezi, izo 4m nafungua kabishara, bado ntakuwa nabakia na 2m/= /mwezi baada ya makato ya mkopo, izo 2m zinatosha kila mwezi kupandisha tofali, Mungu jaalia kabla Jakaya ajatoka madaLakani, nna mjengo, gari na kijibiashara changu pale Mwenge.
.
Mliosoma vyuo naamini mmewahi kuwa na muono huo mkiwa chuoni, huu muono unapangika fresh sana, huitaji hata Kalkyuleta, hii kwa kizungu inaitwa "Theory", wahisani wetu Watu wa Marekani wanaitaga "PLAN A". Maliza chuo sasa uje mtaani, utakutana na kitu kwa kizungu inaitwa "Implimentesheni", ndo neno "PLAN B" linapokujaga, plan B kuielezea ni ngumu labda nitunge sentensi fupi huyo kijana apo juu atayoituma akitoka zake Job, of kozi mwezi wake wa 10 job: "Mwana shwari, leo nmetoka mapema mwana ila sina hata ela ya Bajaj, mwana unawezakuwa na efamsini ya karibu Mkuu nmalizie ngwe, ntakurudishia mwisho wa mwezi mshahara ukitoka, sijasteblaizi bado mwana!"
 
maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
8,922
2,000
mi nilisota nikawa natafuta hata chekea nifundishe nikakosa... ila kila mtu na bahati yake
 
Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
53,516
2,000
"Nkimaliza zangu Chuo ntaaplai zangu kazi Voda, ntalipwa milioni 3.5/mwezi, ntajibana zangu kila mwezi natumia laki5 tu, izo 3m naifaZi benki, baada ya miezi mi3 nanunua gari la 9m/=, nkishakua na gari basi 3m ya mwezi unaofatia napanga nyumba ya laki mbili na amsini kwa mwezi, 3m inayofatia nanunua fenicha, kwanza adi apo ntakuwa nshatimiza miezi 6 kazini, adi apo naruhusiwa kukopa, nakopa zangu 10m/= afu natafuta kiwanja cha 6m tu, si ntakuwa nakatwa 1m/= za mkopo kila mwezi, izo 4m nafungua kabishara, bado ntakuwa nabakia na 2m/= /mwezi baada ya makato ya mkopo, izo 2m zinatosha kila mwezi kupandisha tofali, Mungu jaalia kabla Jakaya ajatoka madaLakani, nna mjengo, gari na kijibiashara changu pale Mwenge.
.
Mliosoma vyuo naamini mmewahi kuwa na muono huo mkiwa chuoni, huu muono unapangika fresh sana, huitaji hata Kalkyuleta, hii kwa kizungu inaitwa "Theory", wahisani wetu Watu wa Marekani wanaitaga "PLAN A". Maliza chuo sasa uje mtaani, utakutana na kitu kwa kizungu inaitwa "Implimentesheni", ndo neno "PLAN B" linapokujaga, plan B kuielezea ni ngumu labda nitunge sentensi fupi huyo kijana apo juu atayoituma akitoka zake Job, of kozi mwezi wake wa 10 job: "Mwana shwari, leo nmetoka mapema mwana ila sina hata ela ya Bajaj, mwana unawezakuwa na efamsini ya karibu Mkuu nmalizie ngwe, ntakurudishia mwisho wa mwezi mshahara ukitoka, sijasteblaizi bado mwana!"

Hahahaaaa....mkuu umenichekesha sana aisee...mi mwenyewe nlikuwaga na ndoto japo hazikufika huko.....sijui hata zimepotelea wapi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom