Grace Kiwelu asema -Walio husika na Richomd waweke Pasi zao rehani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Grace Kiwelu asema -Walio husika na Richomd waweke Pasi zao rehani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Feb 14, 2008.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mjadala wa Richmond unashika kasi sasa .Grace Kiwelu akitoa hoja bungeni amesema anaomba wote walio tajwa na kujiuzuru ili kuepusha wao kukimbia Nchi na wapelekwe Mahakamani na pia amemshauri Lowasa kama ameona hajatendewa haki aende Makahamani ndiko haki na kila kitu kitasikika .

  Kazi kubwa Keenja kasimama anatetea hoja ni ya CCM na wapinzani waachane nayo .Keenja anaongea sasa .
   
 2. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu Lunyungu,

  ebu tufafanulie alikuwa anamaanisha nini, maana hayo maneno yanakatisha tamaa kweli kweli.

  Inaonekana anakerwa sana na upinzani.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Keenja ni kama kawaida yake na CCM leo wanataka kuonekana heroes baada ya Richmond kuwaondoa watu .Ndiyo maana yake na anasema hoja hiyo ni ya CCM na Rais wao wa CCM kaitikia kilio chao.

  Sasa anaongea Mbunge wa CCM na amehoji msemo wa Kasungura kadogo kumbe Lowasa alikuwa anakula sehemu kubwa .
   
 4. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mbunge gani kauzliz aSuala la Kasungura,atakuwa Mjomba wake na Mwanakijiji..Sasa hivi tunapewa Pimbi..Je watakuwala peke yao au tutagawana wote?
   
 5. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Lunyungu

  wana mpango gani na RA na Yona maana waliidharau kamati kwa kukataa kuhojiwa na mwanahalisi wamesema kamati ilidokezwa na Salva kuwa richmond ni ya RA.

  Hakuna aliyeanza kuwashika bango?
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Wabunge wengi wa CCM sasa wanadai kwamba Rostam na Yona wa face justice na hawakubali kwa wao kudharau kamati ya Bunge .Wabunge wa CCM sasa wanadai kuanzia Lowasa na wote walio husika waweke PP zao Uhamiaji wasije kimbia ili hatua zichukuliwe kwa uhakika.Hawa ni Wabunge wa CCM. Kuna mchangia mmoja tu kwa asubuhi anakuja . Wameomba mikataba ya BoT
  wameomba Ofisi ya mwanasheria ipanguliwe na Takukuru iwe chini ya Bunge .Hoja ni nzuri na wote wanaunga mkono hoja za Kamati ya Mwakyembe .
   
 7. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Grace Kiwelu?
   
 8. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Shukrani Lunyungu

  endelea kutuhabarisha yanayojiri hapo Dom
   
 9. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Huyo babu sasa naona akili zake zimechakaa vibaya! Anamaanisha CCM wakitoa hoja wapinzani hawaruhusiwi kuchangia? Kama hivyo basi wangeitoa katika kikao ambacho wapinzani huwa hawahudhurii, huko kwenye mikutano ya CCM huko! Si adabu kutamka maneno yasiyofaa kwa mzee, lakini kwa uzee wa aina ya Keenja ni sahihi kabisa kumwita mpumbavu! Anasahau kuwa hiyo hoja ni ya Kamati Teule ya Bunge ambayo Mwenyekiti wake Mwakyembe aliisoma siku kadhaa nyuma? Au anataka kutudanganya kuwa ile Kamati teule ya Bunge ni ya CCM. Narudia, ni mpumbavu na anapaswa kupuuzwa! Kaniudhi sana. (Mtoto wake Elia alikuwa mwanafunzi wangu, akiisoma post hii aniwie radhi tu, nimeshindwa kuvumilia!)
   
 10. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  naam mkuu lunyungu lete habari za huko, wapinzani hawajaomba kuchangia?
   
 11. green29

  green29 JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 35
  Haina shida mwalimu, inafikia mahali hata familia za mafisadi inabidi zipingane na ndugu zao walio mafisadi. Usishangae kukuta huyo dogo Keenja nae anapigana vita dhidi ya mifisadi humu JF. LIkely akakupa 5 mkuu.
   
 12. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2008
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Hata mimi kaniudhi. HIli suala la Richmond, CCM wamelidandia, lakini liliibuliwa na upinzani! EPA vivyohivyo, sasa wanaleta longolongo eti oh alisimama fulani mwaka juzi... lakini hawakulisimamia bango, walisema tu, wakanyamazishwa na 'bosi' wao Lowassa, sasa wanaleta longolongo. If they lacked courage then, they lack courage now na wanajifanya wakali !
   
Loading...