Govt: We goofed on 1.85bn/- deal

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Govt: We goofed on 1.85bn/- deal

Lowassa---Knew about the deal

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE government admitted for the first time yesterday that it erred in selling a prime piece of land in Dar es Salaam earlier this year for a ridiculously cheap price.

''It is true that the 440m/- price tag was quite low compared to the actual value of the plot,'' the Minister for Planning, Economy and Empowerment, Dr Juma Ngasongwa, told THISDAY.

He made the remarks in an interview with THISDAY in Dar es Salaam after being asked to explain circumstances behind the government's bizarre decision of selling a prime property valued at 1.85bn/- for just 440m/-.

The plot, number 162/38 at the junction of Mirambo Street and Samora Avenue in the city's central business district, was sold by the Parastatal Sector Reform Commission (PSRC) to El-Hillal Minerals (Tanzania) Limited in May this year.

Following an outrage over the questionable deal, the PSRC was forced to revise the price tag upwards and demand an extra payment of 1.41bn/- from the buyer to match the final purchase price with the property's stated market value of 1.85bn/-.

However, apart from admitting that the initial 440m/- price tag was flawed, Ngasongwa defended the government's decision to sell the property at the new price of 1.85bn/- despite criticism that proper procedure and due process were not followed in the transaction.

''I am happy that the PSRC has corrected the unfortunate mistake over the price of the plot and is now demanding payment of an amount equal to the market value of the property,'' he said.

Ngasongwa noted that despite the initial error of selling the property cheaply, the government still made the right decision in selling the plot to El-Hillal Minerals for the development of a proposed international diamond auction market in Dar es Salaam.

Once fully operational, the proposed global diamond auction to be based in the city would give small-scale diamond miners in Tanzania better prices for their gemstones and significantly boost government revenue, he said.

''The world trade diamond centre that the investor, El-Hillal Minerals, plans to develop will be of great benefit to the nation not only as a source of revenue, but also as a vital tool for job creation,'' he explained.

Asked why there was no public tender for the sale of the plot, he dismissed suggestions that the government could have earned even more than the 1.85bn/- if a competitive bidding process was followed.

The PSRC recently came out of its shell and sought to explain its earlier decision of selling the property to the private developer at a throw-away price.

As already reported by THISDAY in a series of investigative reports, Prime Minister Edward Lowassa met with the owner of El-Hillal Minerals, Hillal Hamad Hillal, sometime last year where the businessman is understood to have informed the PM about his intention to buy the expensive government property for just 440m/-.

After the meeting, Premier Lowassa officially directed the PSRC to ''assist'' Hillal as per existing laws and regulations after his previous attempts to buy the plot had come to nought.

In a public statement issued by his spokesman, the PSRC executive chairman, Ali Karavina, announced that El-Hillal Minerals had been given until the end of this month to pay the additional 1.41bn/- for the plot, short of which the government would repossess the property.

The sale of the property ruffled some angry feathers in government with many officials arguing that the plot should have been used to construct a multi-storeyed office accommodation building to house government ministries and agencies.

The Treasury currently pays billions of shillings to private landlords each month from taxpayers' money for the accommodation of government offices.
 
Global diamond auction centre? Yale yale!Naona tunaliwa tena. Kwani Botswana na South Africa wanazo centre kama hizo? Mimi ninavyojua ( and I stand to be corrected) kuwa centre za biashara ya almasi ni Antwerp, Amsterdam na Mumbai. Tunaubavu wa kushindana nazo maana sidhani production yetu ya almasi inaweza kusustain centre hii!Naona tena tunadanganywa na mjanja anayepata hapo mahali kwa sababu zake.
Pili,jee hao wakuu wameishajiuliza athari za kujenga jengo kama hili katikati ya jiji wakati hatujaweza kutatua tatizo la infrastucture? Jengo hili litaongeza traffic loads, mahitaji ya sewerage, maji safi, kinga za moto n.k. Kwa nini tusifungue centre nyingine ili tupunguze mzigo katika historical centre? Huko tutaweza kutengeza infrastructure itakayoendana na mahitaji ya majengo kama haya. Au ndiyo uvivu wetu, kukazania kile tulichoachiwa bila kutaka kukiendeleza?
 
Haya,

I did said before, improvement in communication sector in terms of infrastructure and easier dissiminating of news/information will help Tanzanian a lot?

No doubt this issue was among the order of the day issues in those days;;; but for now now, it is just a history, those who believe they can still continue doing these mauza uza, they are lieing to themselves.
 
FM, asante kwa kushinikiza hilo.... Manake unajua sisi sijui lini tutaacha kukubali kuwa kichwa cha mwendawazimu jamani?? Manake tunajua kujenga kwelikweli, lakini vyoote katikati ya jiji (CBD)... Maji, hakuna, sewerage (usiseme mvua zikinyesha ni maji ya mvua na nanihii.... vyote pamoja nje nje - kipindupindua ndio maana hakiishi etii), parking (duh siku hizi hata kama unayo ile 300 unaweza kosa hata pa kuitumia - house full), foleni (mh, haya hapo sisemi tushazoea hilo- teh teh teh kwani ni wingi wa magari "CRAP"), and the list keep going on and on and on.... Mipango miji wamelala, by the way tunao hawa watu kweli pala nchini manake kama wapo watakuwa wanakula kulala tu hatuoni mafanikio, au wanangoja JK and EL watekeleze???
Lakini walisema kwenye kutakiwa lazima tuseme ukweli na kutoa "Compliments" zangu za mwezi huu zinaenda kwa Muhimbili Medical Centre na Chuo, MHSS) hawa jamaa wafanya kitu ambacho idara nyingi za serikali zimeshindwa - kujenga chuo nje ya Dar, wajemeni karibuni Kisarawe kwetu na sisi tuwe karibu na huduma za afya na pongezi kwa kusaidia kupunguza foleni!!! Wengine mfano huo!!
 
When it comes to important decisions regarding our beloved country, you always goofed. It's very rare for you to make the right decision.
 
My thing is,

1.Kama mnunuzi kashasaini mikataba yote wanaweza kumlazimisha aongeze kidau kisheria?

2.Inawezekanaje vichwa vya serikali vi-"goof" kirahisi hivi? Hapa kuna mazingira ya rushwa. Kuna mtu yeyote anafuatilia ni jinsi gani such a prime location (Karibu na kila kitu kuanzia Mirambo House, Holiday Inn, Kitega Uchumi,Bot Twin Towers, ex-Sheraton etc) imeuzwa kwa kiasi kidogo hivyo? Hivi hatuna watu wanaoweza kufanya evaluation? Nani alifanya hii evaluation na anawajibishwaje?
 
Pundit, ukiona mambo yanakuwa magumu inabidi waseme "We goofed up" heri lawama kuliko fedheha kaka..... Unakumbuka mambo ya COMESA, Richmond, ATC, TTCL...... and many more, it all came to "sorry I goofed up" game over.....
 
The sad thing is kukubali hiyo explanation at face value.With all the cover ups we have seen in the past somebody should vigorously investigate the whole deal. Isije kuwa watu walishapocket kitu kidogo halafu wanaishia kusema "We goofed".next time hawataogopa kufanya ufisadi kwa sababu wanajua in the worst case tutasema "We goofed" mambo yataisha.
 
Hadi kufikia hatua kama hii ni lazima walioshiriki kwenye ujinga kama huu wachukuliwe hatua na waanikwe hadharani. Hatuwezi kukubali kila kukicha kuficha wale wanaotuingiza kwenye mikenge na kuanza kulia chura.
 
Mimi matatizo yangu na hii dili iko katika pande tatu:
1. Sisi sio major players katika biashara ya almasi. Ili tuweze kuwa na kitu kinachoitwa Global Diamond Auction Centre itabidi producers kutoka nchi nyingine waje hapo wakijua kuwa wanunuzi wakubwa watakuwepo ili kununua bidhaa zao. Kwa sasa hivi duniani makao makuu ya biashara ya almasi yako Netherlands hasa katika mji wa Antwerp. hivi karibuni almasi kubwa iliyopatikana katika miaka 13 iliyopita imepigwa mnada huko Antwerp. Ukichukulia kuwa almasi hiyo ilipatikana Lesotho, unajiuliza kwa nini hawakwenda kuinadi Afrika ya Kusini bali walienda Antwerp? Jibu rahisi ni, ndiko huko unakoenda ukitaka bei nzuri maana wenye nazo wote wako huko. Sasa atakayeleta almasi yake kuuza Dar nani? Ndiyo maana naona hii auction centre ni kama kanya boya ili wapate kiwanja. Wakishapata kiwanja watakitumia watakavyo wao. Au watamuuzia mwingine aliyenazo. Miradi mingine kama huu ni ule wa Nyamagana. Ubabaishaji mtupu maana wanatujua tunavyoweweseka tunaposikia neno mwekezaji.
2. Hii ni conservation area kwa hiyo maendelezi yake yanapaswa kufanywa kwa makini ili yasiharibu mandhari ya eneo lenyewe. Tutakuja jutia hii kasi yetu ya kuvunja majengo ya zamani ya kihistoria na badala yake kujenga maghorofa yasiyo na maana na mvuto wa aina yeyote. Watu hawaendi Paris kutembelea La Defence kwenye maghorofa bali wanaishia kwenye mji wa kihistoria! Kwa bahati mbaya tukishayavunja hatutaweza kuyarudisha. Angalia nyumba aliyofikia Robert Koch (alikuja kushinda zawadi ya Nobel mwaka 1905) wakati wa utawala wa wajerumani akifanya research kuhusu magonjwa mbali mbali tuliishaivunja na kujenga maghorofa ya madaktari! Ingawa haiko katikati ya mji, sijui kama kuna mtu aliyenyanyua kidole kuinusuru nyumba ya marehemu Mwalimu Nyerere iliyopo Magomeni. Ilipoungua mahakama ya Kivukoni ambamo wa kina Nyerere walishtakiwa wakati wa harakati za uhuru, tulikuwa tayari kuivunja ili tuweke kitu cha kisasa. Tushukuru wafadhili waliyoinusuru kwa kusisitiza ijengwe upya kama ilivyokuwa awali. Tushukuru wake za mabalozi wa nchi za kigeni na watu wengine waliosimama kidete kuinusuru Botanical Gardens isidhulike na ujenzi wa Holiday Inn. Ikumbukwe kuwa hapa katikati, waheshimiwa wenye mji kuna wakati walikuwa wanataka majengo YASIYOPUNGUA ghorofa 12. Ukiweza hamsini, twende tu. Naombea Mungu kuwa sheria hiyo iwe imefutwa ama sivyo huu mji wetu utaharibika beyond repair.
3. Barabara na huduma nyingine katikati ya mji hazitoshelezi. Kwa vile jengo hili litakuwa na maofisi mengi litaongeza idadi ya watu wanaosafiri kutoka kwenye suburbs kuja kufanya kazi katikati ya jiji. Kama Morani alivyosema, itaongeza mahitaji ya parking n.k. Historia yetu ni kuwa hatupendi kuwekeza kwenye infrastructure ndiyo maana tunabaki kukazania Upanga, Oysterbay na Masaki ambako waliweka basic infrastructure wakoloni. Sisi tulizivuta tuu hadi Masaki. Utaona bado tunatumia jela walizotuachia wakoloni, mochuari walizotuachia wakoloni n.k. Nikirudi kwenye hili, kwa nini tusiongezee centre kwa kuwekeza nje ya city centre? hata hizo ofisi za serikali kwa nini tusizijenge nje ili kupunguza pressure katikati ya jiji?
 
Idea ya ku-decentralize ina akili.Kama kile kipande kutoka Sayansi na Teknolojia mpaka Mwenge pana potential ya kuwa ka-centre fulani hivi.Isitoshe itakuwa a shorter commute kwa watu wa Mbezi na huko ndiko mji unakopanukia.Tayari Celtel na watu wengine walishaanza kuweka ofisi pale.

Sio kila kitu kikae Samora Ave.

On a lighter note about this Antwerp Netherland business, dada mmoja wa kimarekani alikuwa anakazania kabisa kuwa Mexico iko kaskazini na Canada iko kusini mwa Marekani.

Usishangae ya Musa utaona ya Firauni.
 
Hii kali kwelikweli. Mi naomba tu kuuliza hawa ElHillal wana uzoefu gani katika masuala ya diamond?
Sasa tukizungumzia biashara ndo kabisaaa sijui watapata wapi!? Maana biashara kubwa ingekuwa kama De Beers mwadui wangekubali kuleta hapo diamonds zao. Hawa wachimbaji wadogo.. sijui!
 
Serikali yaingilia gogoro la Manispaa K`ndoni

2007-12-17 17:50:55
Na Abdul Mitumba, Kinondoni


Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, imeingilia kati mgogoro wa muda mrefu kati ya Manispaa ya Kinondoni na muwekezaji mmoja aliyejenga maghorofa eneo la Masaki kwa kuagiza uwepo wa mazungumzo ya nje ya mahakama baina ya pande hizo mbili.

Mgogoro huo, ni ule unaohusu ujenzi wa majengo yenye ghorofa saba badala ya tatu uliofanywa na muwekezaji badala ya tatu kama ilivyoidhinishwa na manispaa.

Imeelezwa kuwa lengo la agizo hilo, la Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, ni kurejesha imani kwa wawekezaji.

Aidha, agizo hilo limekuja wakati tayari muwekezaji huyo akiwa ameshaiandikia barua Serikali, akiomba kuondoa shauri hilo mahakamani ili lipate kuzungumzwa kwa majadiliano yaliyo nje ya chombo hicho.

Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Bw.Julian Bujugo ndiye aliyetoa maelezo.

Amesema baada ya kupokea maelekezo hayo, waliitisha kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani ili kuliweka wazi suala hilo kabla ya kuzingatia utekelezaji wake.

Akasema ni kweli kuwa muwekezaji huyo alivunja sheria kwa kujenga jengo la ghorofa saba badala ya tatu alizoidhinishiwa kisheria na mamlaka halali, lakini kwa upande wao, pia walichelewa kuhakiki ujenzi huo hadi ulipokamilika.

``Kwa ujumla Manispaa yangu imelipokea agizo hilo na kikao cha mwishoni mwa wiki kimelijadili kabla ya kulifikisha katika Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ya Manispaa kwa hatua zaidi kabla ya kulitolea tamko rasmi,`` amesema Bw. Bujugo.

Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Hassan Rajabu, amesema mara shauri hilo litakapowasilishwa kwake wakati wa vikao, umakini utahitajika zaidi kutokana na unyeti wa suala lenyewe.

``Muhimu kuliko yote katika hilo ni mtazamo wa serikali dhidi ya uwekezaji na wawekezaji wenyewe.

Kimsingi, Manispaa haitahusika na utoaji wa fidia kwa mwekezaji huyo kwa sababu hatua ya kuvunja jengo hilo ilizingatia sheria na haki na ndiyo maana muwekezaji huyo ameomba turudi mezani, ``akasema.

Bw.Rajab, ambaye pia ni diwani wa Kata ya Makurumla, akasema muwekezaji huyo amejenga nyumba hizo eneo la Masaki na wataalam wa idara yake waligundua kuwepo kwa udanganyifu wa ujenzi na ndiyo maana wakaomba idhini ya mahakama ili kuzivunja.

SOURCE: Alasiri

Hawa ndiyo aina ya wawekezaji waokuja Tanzania! Wasiwasi wangu ni kuwa hata huyu tunayemzungumzia sasa atatufikisha hapa hapa! Kumaliziana nje ya mahakama.
 
IMHO, the order is totally unconstitutional.The executive has no power over a matter that is currently in the hands of the judiciary.Isn't that a very basic issue of checks an balance?

Au Tanzania tume suspend checks and balance?
 
Haya WanaJambo wenzangu, hii nimeipata kwenye Thisday la leo..... Mh, nadhani hata ile statement kwamba "We goofed up" smells fishy...... halafu kuna wakubwa pia walipinga swala hili lakini mambo mbele kwa mbele, haya wajameni ndio mchezo wa "vimemo" na "vifonekoli" kutoka kwa walioshika mpini that ""assist"" hata kama ni bogus deals!!! Kaazi kwelikweli

Controversial govt property deal: Mum's the word, decides businessman involved


THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE private businessman behind the purchase of a prime piece of government property in Dar es Salaam earlier this year for a ridiculously cheap price has declined to comment on the hugely controversial transaction.

''I have nothing to say, since you have already written extensively about this matter in your newspaper,'' said Hillal Hamad Hillal, owner of El-Hillal Minerals (Tanzania) Limited, when sought out yesterday by THISDAY for his take on the tough new conditions given to him by the government for the deal to be finalised.

Hillal, who was recently elected to the ruling Chama Cha Mapinduzi's national executive committee (NEC) representing Shinyanga Region, had initially offered to buy the government land on plot number 162/38 at the junction of Mirambo Street and Samora Avenue in the city?s central business district for just 440m/-.

Surprisingly, the government accepted the exceedingly low offer for the property, made through the El-Hillal Minerals (Tanzania) Limited company and without following the government's own procedures and regulations which prohibit state-owned property from being sold to private companies unless by competitive tender bidding process or public auction.

El-Hillal Minerals paid just 440m/- for the property despite a valuation report commissioned by the Presidential Parastatal Sector Reform Commission (PSRC) just weeks before the sale putting the actual market value of the plot at 1.85bn/-.

Independent real estate experts interviewed by THISDAY said even the 1.85bn/- price tag was a conservative estimate of the property value, suggesting that the plot could fetch up to 5bn/- through a truly competitive public tender bidding process.

The government finally conceded last week that the PSRC had made a mistake in initially selling the property for just 440m/- to El-Hillal Minerals. According to the Minister for Planning, Economy and Empowerment, Dr Juma Ngasongwa, the buyer has now been instructed to pay the full amount of 1.85bn/-.

Following a series of investigative stories published by THISDAY on the clearly-dubious deal, the price tag has now been revised upwards and El-Hillal Minerals ordered to pay the extra 1.41bn/- for the plot, being the difference between the initial price and the real valuation.

Ngasongwa contended that despite the initial error of selling the property cheaply, the government was right to sell the plot to El-Hillal Minerals, since the company would develop a key project likely to create new jobs and significantly increase government revenue collection.

Among other things, the company has pledged to construct a 12-storeyed building that would house a proposed world diamond auction market and a bank of international repute in Dar es Salaam.

It is understood that Prime Minister Edward Lowassa met with El-Hillal Minerals owner Hillal Hamad Hillal sometime last year, and afterwards formally instructed the PSRC to ''assist'' Hillal as per existing laws and regulations after his previous attempts to buy the plot had come to nought.

In a recent public statement issued by his spokesman, PSRC executive chairman Ali Karavina announced that El-Hillal Minerals had been given until the end of this month to pay the additional amount of 1.41bn/- for the plot, short of which the government would repossess the property.

Several senior government officials are known to oppose the sale of the property on the argument that the state should use the land to construct its own building to house offices for various ministries and government agencies, hence saving the Treasury from paying billions of extra shillings to private landlords every month.
 
Naona wale jamaa waliodhani wame wini baada ya sisi ku "Goofed up" wameongea kama ilivyowekwa kwenye Thisday ya leo, 29 Feb 2008....... Kaazi kweli kweli manake mimi yangu ni haya:
1. Eti mauzo yalifuata sheria na taratibu zote za serikali, kama ni kweli kwa nini serikali ilikuja kusema wali "GOOF UP"?? Nani wa kulaumiwa ni yeye au??

2. Tender ya mauzo ya hili jengo ilitangazwaje? Na kama ilitangazwa kwa uwazi na ukweli na sasa Serikali imebadilisha mawazo na kupandisha bei ya mauzo takribani mara 4 hivi. Je kama kweli alikuwa na haki na kama sheria na taratibu zilifuatwa kwa nini yeye hakufikiria hata kufungua kesi kupinga uamuzi huo???

3. Huyu mtu aliyetoa maamuzi na kusaini hati ya mauzo, kisha ikagunduliwa kwamba kuna makosa akaenda kusaini tena hati ya makubaliano ya mabadiliko ya bei alipewa adhabu gani??

4. Uamuzi wa Serikali kupewa ofisi ya takriban 1300sq.m kwa kipindi cha miaka mitano ulifikiwa kwa kufuatia vigezo gani????

5. Huyu mkubwa wa Hillal anasema walikubaliana kulipa by 31 Dec 2007... Sasa anasema wamekubaliwa kuongezewa muda mpaka lini?? Na kutokana na delay in payment, kuna hatua gani atachukuliwa??

6. Anaposema kwamba ni Thisday ndiyo ilionyesha kuwa kuna makosa then bei ikapanda, sasa hii ina maana kama Thisday wasingesema PSRC ilikuwa ni business as usual au??? Hakuna aliyewajibishwa kule mahali kwa hili jamani???

Unless aseme kwamba alipewa jengo ikaonekana ni mchezo mchafu kisha wakakubaliana out of court ndio anaturudishai chetu sasa?

Naomba kuwakilisha..............

Article yenyewe ni:
Private buyer in prime government plot deal says: No hanky-panky involved at all

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

A LOCAL businessman behind the purchase of a prime government plot in the Dar es Salaam city centre, Hillal Hamad Hillal, has finally stepped forward to explain the controversy behind the deal, saying there was no hanky-panky involved in the transaction.

’’This was a clean deal, which followed all government laws and regulations. There was absolutely no corruption or any wrongdoing involved,’’ he declared yesterday in an interview with THISDAY in the city.

He said the government had initially agreed to sell the expensive real estate property to his company, El-Hillal Minerals (Tanzania) Limited, for 440m/- on the understanding that it would be allocated at least 1,300 square metres of office space, free of charge, for five full years after completion of the construction of a high-rise building on the property.

The plot in question with registration number 162/38, situated at the junction of Mirambo Street and Samora Avenue in the city’s central business district, is currently being used as a temporary parking lot for employees of the Bank of Tanzania (BoT).

Hillal however, admitted that, following complaints highlighted in a series of THISDAY reports to the effect that the government had sold the property far too cheaply, terms of the sale agreement were abruptly changed.
He said the now defunct Presidential Parastatal Sector Reform Commission (PSRC) had originally signed a sale agreement with his company on May 14 last year, in which he was to pay 440m/- cash and provide the government with rent-free office accommodation for five years as part of the deal.

But on September 24, PSRC Executive Chairman Ali Karavina informed Hillal by letter of the changes to the sale agreement, where he would now be required to pay up an extra 1.41bn/- in addition to the 440m/- that had already been paid.

He said he was told this would increase the sale price to 1.85bn/-, which was the true value of the property according to a valuation earlier commissioned by the same PSRC.

Hillal told THISDAY that although he was initially required to pay the outstanding balance by October 4 last year - and later given a deadline extension to December 31 - he asked for more time to pay the extra 1.41bn/- because of the short notice he had been given about the new conditions.

’’The government agreed to my request, and we assigned ’Addendum Number 1’to the May 14, 2007 sale agreement on December 21, 2007,’’ he said.

The addendum signed by Karavina and Hillal effectively extended the deadline for the property buyer to pay the remaining 1.41bn/- to June 30, 2009.

Hillal said since PSRC legally ceased to exist on December 31 last year, he would now be sending pay cheques to the state-run Consolidated Holding Corporation, which has taken over remaining operations of the defunct privatisation agency.

He reiterated that the transaction as a whole was ’’completely above board,’’ explaining that the initial 440m/- price tag plus the approximately $1.56m (around 1.8bn/-) worth of rent that the government would have been provided free of charge for five years was fair compensation for the currently-barren plot.

’’I would like to reiterate that this transaction was approved by all relevant government authorities and followed all procedures,’’ said Hillal, who is proprietor of El-Hillal Minerals (Tanzania) Limited.

The company runs a diamond mine in Shinyanga Region, near the Mwadui-based Williamson Diamond Mine owned by South Africa’s giant De Beers company.

Hillal confirmed the company’s plans to build an international market for raw diamonds on the Dar es Salaam plot in question. ’’My intention is to develop a high-rise building with 12 floors of office accommodation,’’ he said.

’’Apart from a diamond auction market, I have also reached an agreement with a highly-reputable international bank to open its branch in the same building,’’he added.

He said design work is already underway for the planned construction project, which is expected to cost in the region of $12m (approx. 15.6bn/-) in total. The construction work itself will commence once the company has received all necessary permits from the government and city council, Hillal explained.
 
Hii ndo Bongo,

You pay 440m to GoT, take some 500m to distribute among the government official responsible for the deal (valuers and decision makers), and you have the property for less than half the price. teh teh teh.

Kuna yule mchina alisema bongo ni sehemu ya rushwa poa.
 
1. Sisi sio major players katika biashara ya almasi. Ili tuweze kuwa na kitu kinachoitwa Global Diamond Auction Centre itabidi producers kutoka nchi nyingine waje hapo wakijua kuwa wanunuzi wakubwa watakuwepo ili kununua bidhaa zao. Kwa sasa hivi duniani makao makuu ya biashara ya almasi yako Netherlands hasa katika mji wa Antwerp. hivi karibuni almasi kubwa iliyopatikana katika miaka 13 iliyopita imepigwa mnada huko Antwerp. Ukichukulia kuwa almasi hiyo ilipatikana Lesotho, unajiuliza kwa nini hawakwenda kuinadi Afrika ya Kusini bali walienda Antwerp? Jibu rahisi ni, ndiko huko unakoenda ukitaka bei nzuri maana wenye nazo wote wako huko. Sasa atakayeleta almasi yake kuuza Dar nani? Ndiyo maana naona hii auction centre ni kama kanya boya ili wapate kiwanja. Wakishapata kiwanja watakitumia watakavyo wao. Au watamuuzia mwingine aliyenazo.
Fundi Mchundo, sijui kama uliandika hio point hapo juu kwa makusudi au ulikua unajibu hoja ya kiwanja. But I've picked up on it maanake kama ni mambo ya diamonds, kuna m-deal mmoja heavy sana ambao yatu wengi awakuushtukia na umezimwa zimwa chini chini ata magazeti sidhani kama yaliongelea. Kupata mwanga zaidi, kafwatilie lile sakata lote lililo ibuka kuihusu TANSORT sometime ago na utaelewa kwanini nime ku-quote hapo juu.
 
Back
Top Bottom