Govt has no plan to charge Warioba, says Justice minister | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Govt has no plan to charge Warioba, says Justice minister

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 17, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,601
  Trophy Points: 280
  2009-01-17 07:26:00

  Govt has no plan to charge Warioba, says Justice minister
  By Vicent Mnyanyika
  THE CITIZEN​

  The Government has no intention to arrest and prosecute the former Prime Minister and First Vice-President, Judge Joseph Warioba, Constitutional Affairs and Justice minister Mathias Chikawe has said.

  There have been widespread rumours that Judge Warioba would at anytime be arrested for graft charges linking him with Mwananchi Gold Company, a gold refinery which manufactures jewelry.

  Answering questions from reporters after he had convened a press conference to explain on the three-year success of his ministry, Mr Chikawe said his ministry had no idea on the widespread rumours.

  He said his office dealt with prosecution and not investigations on or arrests of suspects.He said the Government was neither aware nor had it sent anybody to threaten Mr Warioba that it was planning to arrest him in connection with embezzlement of funds at the Mwananchi Gold Company.

  "My ministry is more concerned with prosecution of cases, and not investigations nor arrest of suspects. These are functions of the police and PCCB; my ministry has no idea," he said.

  He added: "I have no reason to arrest Judge Warioba; my office is less concerned with the arrest and we have never sent people to threaten him."

  Early this week, Judge Warioba addressed a press conference to give his stand on the rumours. He said he was not afraid of being arrested, calling on the Government to hurry up and do so if there were such plans.

  Said he: "I am not afraid of arrest, in fact, if there are such arrangements they should hurry up. I am tired of the rumours as I have no peace of mind because many people and other well wishers keep on asking me about them and consoling me."

  Speaking on his ministry's success, Mr Chikawe said for the past three years, the Government has managed to speed up the prosecution process to reduce the piling up of cases and corruption in law courts.

  He said the program has involved the separation of the department of investigations and prosecution. Through this they have managed to reduce the piling up of high court cases.

  He added that that during the three years his ministry has managed to introduce the Registration Insolvency and Trusteeship Agency (Rita).
  It deals with the registration of births, deaths, weddings, divorces and oaths, he explained.

  Mr Chikawe said since its establishment in 2006 Rita has registered about 3.1 million births, 235,795 deaths, 58,295 weddings and 48 divorces.

  Also, considering family complaints, a special department has been established under Rita to deal with oaths in order to minimize them and family misunderstandings.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Jan 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kila mwenye akili timamu alifahamu kuwa hakuna kesi dhidi ya Warioba isipokuwa ni njama za Mafisadi ambao walitaka kuonyesha Umma kwamba sasa hivi serikali imekosa mwelekeo -Kila kiongozi wa zamani ni mshukiwa na fisadi hivyo kuhatarisha zaidi Usalama wa nchi...
  Hili lilikuwa pandikizi la mbegu mbaya ktk uchunguzi unaoendelea kuhusiana na Mafisadi na Warioba amefuta kabisa mzizi wa fitna hizo hivyo serikali ipate kuendelea na Operation yake..
  la muhimu kwetu wananchi na hasa wawakilishi wetu Bungeni kina Dr. Slaa tunaomba sasa hivi mfuatilie swala la Mwananchi Gold ilikuwaje iondolewe ktk mpango madhubuti wa kuwasaidia wananchi..
  Wananchi wapate kufahamu kuanzishwa kwake, kiasi gani cha fedha kilitumika toka fungu gani na leo hii Mwananchi Gold kama shirika la Umma linafanya kazi gani, lina Assets zipi, na Wakurugenzi wake wanalipwa vipi..
  Beside all that, WHAT went wrong!..
   
 3. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kula tano babake!
   
 4. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nilivyomuelewa Mh Chikawe

  Wizara yake haina jukumu la kumkamata au kumpeleleza Mh Warioba. Jukumu la Wizara yake ni kuendesha kesi.

  Kwa mantiki hiyo suala la Warioba bado halijafika kwa DPP ( au bado ni siri) lakini ni wazi kabisa kutokana na maelezo ya Mh Chikawe huenda suala la Warioba lipo kwenye mamlaka zingine zinazoshughulikia upelelezi. Ni muhimu kwa Warioba akakaa kimya ili asiingilie utendaji wa machinery hizi za kutoa haki ambazo nina hakika yeye ni mdau mkubwa katika wale waliozijenga hapa nchini.
   
 5. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  :eek:
  Sijui wenye kudai vinginevyo!
  Najua kuna wakuu humu mimacho imewatoka:eek:


  Maybe the Govt has plans to investigate itself, Mwananchi Gold!

  Kula Breki!!!
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Jan 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pundamilia07,
  Warioba hakusema wizara hiyo impeleke mahakamani hata kidogo isipokuwa waziri kajibu maswali ya waandishi wa habari ambao walitaka kufahamu kuhusiana na tetesi hizi.
  Kila kesi inayotakiwa kufikishwa mahakamani huwa kuna ushirikiano mkubwa kati ya ofisi zote za mamlaka ya mashtaka na ofisi za Mahakama hivyo kama zisingekuwa tetesi tupu kungekuwepo na ukweli fulani..
  Mkuu Warioba kafuta kabisa midomo ya waandishi na mwenye kueleza habari hizi sasa hivi giiii kwa sababu lengo halikuwa Mwananchi Gold zaidi ya wao kufikiria kwamba Warioba ana hisa ndani ya Mwananchi Gold!, hivyo tumzoe naye ktk kundi la Mafisadi kuharibu kabisa mwelekeo ya kesi hizi...
   
 7. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Jamani tusiwe majudge wa maneno. Mafisadi wapo, wanajijua, na siku zao ziko karibuni. Kuanzia wa Meremeta, Kagoda, IPTL na hata Mwananchi gold.

  Huwezi kuzuia tuhuma, kama zipo zipo tu.
   
 8. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mkandara,

  As long as Mwananchi Gold ilichota pesa za wavuja jasho ambao hawazifaidi vilivyo, tuna haki ya kudai maelezo. Katika kudai maelezo hatuangalii sura ya mtu, kwani wapo watu wakimya na wataratibu lakini mafisadi wa kutupwa. Tuna haki ya Warioba atueleze kwa kinaga ubaga. Swala la kupelelezwa kwa Warioba ni jambo la kawaida kabisa hasa pale panapokuwa na utata katika jambo fulani. Lengo la upelelezi si kumfikisha mtu mahakamani tu bali ni kupata facts. Endapo baada ya upelelezi itabainika kuwa kuna tatizo na anahusika ni wazi Warioba atapandishwa kizimbani Kisutu ili aweze kujitetea kwa mujibu wa sheria inavyomtaka na wala si vinginevyo. Enzi ya Kisutu kuwa ni mahala pa wezi wa kuku tu imekwisha, hata mimi na wewe tunaweza kufikishwa hapo endapo tutakuwa mafisadi.
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Jan 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pundamilia07,
  Maneno yako msumari kabisa...Sasa ikiwa hatuangalii mtu inakuwaje tunamvaa Wakili wa shirika badala ya Uongozi wa shirika.?...
  Tunafahamu nani mwanzilishi wa shirika hilo iweje Warioba ambaye ALIOMBWA kuwa wakili jina lake liwe mbele ya mashtaka!..
  Mkuu jiuliza hivyo badala ya kujenga tuhuma zaidi..Je, mnaogopa kutaja majina la hao waliohusika kuunda Mwananchi Gold - Mkapa ana the gang!..
   
 10. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,762
  Trophy Points: 280
  Naomba niliangalie hili swala kwa mtizamo mwingine kidogo,

  Kwa uelewa wangu mdogo waziri wa sheria ni mwanasiasa. Kwa nchi inayosema inafuata utawala wa sheria (as Tanzania claims) hawezi kuamua nani apelekwe mahakamani nani asipelekwe mahakamani. Kifupi katika nchi yetu waziri wa sheria siyo Chief Prosecutor. Kwa hiyo Chikawe ametoa kauli ya kisiasa kuliko ambavyo watu tunaweza kusema hapa. Kinachompeleka mtu mahakamani siyo Serikali bali ni Ushahidi uliopo dhidi yake.

  Swala la Warioba, mimi naona huyu mzee amekosa msimamo. Kitu ambacho angekifanya ni kukaa kimya. Kama DPP akiamua kumfungulia mashtaka kwamba anahusika na ubadhirifu (kama upo) hapo ndo angesimama akatoa maelezo yake na ni namna gani kampuni yake ilivyohusika katika swala zima la Mwananchi gold. Baadala yake huyu mzee anataka kulifanya swala la ufisadi liwe la kisiasa zaidi kwamba watu wanalipiza kisasi. Kumbe siyo hivyo. Ukweli ni kwamba pesa nyingi ziliibwa sana watanzania bila kujua. Hata existence ya Mwananchi Gold tumeijua juzi juzi tuu baada ya Dr. Slaa kupiga kengele! Otherwise siyo serikali wala WARIOBA..WOTE WALIKUWA KIMYA!

  Mbona kama alikuwa genuine hakauita press conference kabla na kuwaambia huu mradi unaendelea vipi? Iweje leo ndo ajitokeze baada ya Slaa kuianika Mwananchi Gold..na amejitokeza kwa sababu yeye ndo culprit mkubwa..as a lawyer and shareholder.

  I dont question the integrity of Mzee Warioba, lakini lazima wazee kama hawa wajue kabisa zama za kufanya kila kitu kiwe siasa zinahesabika-hata Tanzania. Ni huyu Mzee aliyesimama kidete kupinga hoja za ufisadi kwamba kiongozi wa nchi akituhumiwa ufisadi nchi itayumba, can you imagine? kwa hiyo RAISI AKIIBA TUKAE KIMYA KWA SABABU NCHI ITAYUMBA? GIVE ME A BREAK! Tumewasikia akina Kingunge wakibeza juhudi za kupambana na ufisadi...baaada ya siku leo wako kimya!

  Hapana Warioba....ukiangalia kwa undani..ana woga flani na alichofanya Chikawe, ni kutoa kauli za kisiasa. Lakini ukweli ni Kwamba Chikawe ni mwanasiasa hawezi kupanga nani apelekwe mahakamani, au nani asipelekwe. Atleast Katiba ya Jamhuri yetu haimpi mamlaka hayo. Ni kama Kikwete aamke asubuhi atangaze kwamba Lowassa au Sumaye (mfano) hawatashtakiwa..He can do it, lakini kisheria hapaswi kufanya hivyo. Hiyo siyo kazi yake. Sana sana anaweza kuwapa msamaha wakishahukumiwa!

  Kwa hiyo Mzee Warioba, kaa kimya. Kama ushahidi upo, utajieleza na wajuvi wa sheria wataamua nani mkweli kati yako na washataki wako. Lakini unachokifanya hapa ni kutaka kulifanya hili swala liwe la kisiasa zaidi upewe sympathy na wananchi. And YOU being the Former ATTORNEY GENERAL you should know better how the law works. Na Iam sure Warioba being the man of the system anajua kwamba there is something in the pipeline coming against him, atakuwa ameshaambiwa na vijana wake ndani ya system.. ndo maana ameamua kupiga pre-emptive strike.

  Kama wengine walivyosema, kwa nini watu kama akina Warioba waiogope sheria wakati ndo nyinyi wenyewe mliozitunga? Perhaps it is good for you to come to the other side of the fence, uangalie sheria ulizoshiriki kutunga zinavyofanya kazi in the real world!
   
 11. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkandara,
  Si nia yangu kuzidi kumjadili Mzee Warioba kwa kiasi hiki kwani ninachodai mimi ni maelezo ya kina na wahusika akina Polisi na TAKUKURU watafanya kazi zaidi kwa niaba yangu.
  Lakini cha msingi ni kuwa kama umesoma maelezo ya Mzee Warioba yeye huenda ni mmoja katika watu muhimu waliohusika katika uanzishwaji wa Mwananchi Gold. Sasa inategemea scope ya upelelezi ikoje, je unaanza kupeleleza katikati na mwisho bila ya kuanza mwanzo? Hapo tuwaanchie akina Manumba na Hoseah.

  Hivi unapotaja Mkapa and the Gang unamaanisha Warioba hayumo kwenye kundi hilo?
   
 12. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  I salute you, it is a very good analysis ambayo haijabeba hata chembe moja ya ushabiki.
   
 13. O

  Ogah JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ........thats the bottom line..........hakuna cha nini wala nini........
   
 14. O

  Ogah JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  swadaktaa Mkuu Masanja........lets call spade "a spade"....nothing less nothing more............
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Jan 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pundamilia07,
  Maneno ya warioba yanawauma nini hasa?..
  Nikinukuu maneno yake alisema hivi:-
  "Uamuzi wa kuanzishwa kwa Kampuni ya Mwananchi Gold ulitokana na nia njema ya serikali, serikali iliamuru BoT na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Kampuni ya MA-CE ya Italia kuunda kampuni hiyo. Baada ya uamuzi huo, serikali ilikuja kwenye ofisi yetu ya uwakili ya Nyalali, Warioba & Mahalu Law Associates ili tuisaidie kuipatia huduma ya kisheria kabla na baada ya kuundwa kwa kampuni hiyo.

  Kwa hiyo maamuzi ya kuunda shirika hilo hakuhusika na kama shirika lake lingekataa wangetafutwa mawakili wengine..
  Wapi kakosea ikiwa yeye kazungumza ukweli unaohusiana na kampuni hiyo.. Kwa nini akae kimya!.. nipeni reason ya yeye kukaa kimya kwani anaharibu kitu gani anapozungumza..

  Mkapa na his gang ni viongozi wote wanaohusika na Ufisadi..Warioba alikuwa atumiwe kama Bangusilo na kawahi mapema kusema ukweli sasa wanahaha hawana pa kutokea..
  Mkuu baada ya maelezo ya Warioba hutamsikia Hosea, Takukuru, Polisi wala mavi yake uchunguzi kuhusiana na Mwananchi.. trust me Warioba kafunua kawa ambayo haiukutakiwa kufunguliwa hadi wageni wa heshima wamefika.. sasa hivi harufu imefika hadi kwa majirani..
  Unless kina Dr. Slaa walifuatilie swala hili zaidi tena bungeni laa sivyo ndio limekwisha!..
  Maneno ya mwanzo ya warioba kuhusiana na Ufisadi yamechukuliwa out of context, kwa sababu alimaanisha tuwe makini sana tunapowatuhumu viongozi kwa kufuata sheria laa sivyo tunaweza kuhatarisha usalama wa nchi..hakusema waliotuhumiwa ni uongo au hakubaliani na tuhuma hizo ila tufuate sheria akiwa kama mwanasheria alijua madhara ya kuropoka ambayo yanaweza hatarisha hata masiha ya watu wasiohusika..
  Utakuja amini maneno yangu, mkuu ktk maswala kama haya naona mbali sana..
   
 16. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #16
  Jan 18, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Mkandara, naomba nikuulize.
  Given Chikawe ni mwana siasa, na wote waliofunguliwa mashitaka wamefunguliwa na judiciary ambayo iko independent...ungetegemea Chikawe mwana siasa aseme kwamba Warioba atashitakiwa? Huoni kwamba Chikawe amelikwepa swali ambalo si lake na kujibu kama mwanasiasa?
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Jan 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  MgonjwaUkimwi,
  Mh. Chikawe hakukwepa swali kwa sababu kaulizwa kama wizara yake ina taarifa za uchunguzi huo..Kama alivyosema Pundamilia hapo juu kuwa kazi ya uchunguzi sii ya wizara yake, hivyo kwa mjuzi utafahamu umebonyeza wrong number!..
  Tatizo la watu wengi sio tena Mh. Chikawe wala idara husika isipokuwa macho yao ni Warioba..inaonyesha kama vile watu hawaridhiki na maelezo ya Warioba au wamechukia Warioba kutoa ukweli mbele ya uchunguzi au lolote lile..
  As a fact, Warioba kama wakili wa Mwananchi Gold ndiye anatakiwa kuzungumza on their Behalf.. unajua tena sheria za huku majuu... Talk to my Lawyer!..
  Kisha kinachonishangaza zaidi ni kuwa toka lini lawyer akawa ktk kundi la Ufisadi kwa sababu tu ni wakili wa shirika ambalo linawapa wasiwasi kuanzishwa kwake na hata jinsi linavyoendesha kazi..
  Kumbuka mkuu miaka ya nyuma kabla ya uchanguzi niliwahi kusema Warioba anafaa kuwa President.. wakaja watu hawa hawa na kusema Warioba ni fisadi kwa kwa sababu ana hisa ndani ya Mwananchi Gold shirika la nje..kumbe ni shirika letu wenyewe tumelianzisha during transition period ya kuingia Kikwete wakati ambao scandal zote za EPA na kadhalika zilikuwa ktk kilele..Hii inanipa wasiwasi na siasa za Bongo!
   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Warioba ametufumbua macho
  Tanzania Daima


  [​IMG]

  [​IMG]
  JUZI Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, alisema kuna maneno yamekuwa yakisambazwa kuwa yeye ni mmoja wa viongozi watakaofikishwa mahakamani kwa makosa ya kutumia ofisi za umma vibaya, hususan kwa kuhusishwa kwake na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za Kampuni ya Mwananchi Gold.
  Kwetu sisi, maelezo ya Warioba kuwa hahusiki na ubadhirifu wa fedha katika kampuni hiyo, ni suala linalohitaji kufanyiwa uchunguzi wa kina na ikithibitika hivyo, hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake na kama ikithibika kuwa hahusiki, basi watu na vyombo vilivyohusika kumchafua vitapaswa kutimiza wajibu wa kumsafisha.
  Katika taarifa yake, Warioba zaidi ya kutoa ufafanuzi wake kuwa hahusiki na ubadhirifu huo, pia alitoa taarifa nyingine nzito kuhusu kampuni hiyo, ambazo sisi kama sauti ya umma tunaamini kuwa serikali inapaswa kuzitolea ufafanuzi wa kina.
  Alisema ‘Mwananchi Gold Company' ni kampuni iliyoanzishwa kwa uamuzi na ridhaa ya serikali ambayo ilikuwa ikitekeleza sera yake ya kuwasaidia wachimbaji wadogo wadogo ili waweze kusafisha dhahabu zao hapa nchini na kuziuza kwa bei halali.
  Alisema anasikitishwa na maneno ya kupotosha kuhusu uanzishwaji wa kampuni hiyo pamoja na uamuzi wa serikali kulikalia kimya suala hilo pasipo kueleza ukweli.
  Alieleza kuwa Kampuni ya uwakili ya Nyalali, Warioba & Mahalu, Law Associates, ambayo yeye ni mmoja wa mawakili wanaoimiliki, iliombwa na serikali kutoa huduma ya kisheria kusaidia uundwaji wa kampuni hiyo.
  Baada ya kazi hiyo, serikali iliamuru Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Kampuni ya MA-CE ya Italia kuunda kampuni hiyo, ambayo ilizinduliwa rasmi na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, Desemba mosi 2005.
  Kwamba kampuni hiyo ilianza kufanya kazi kwa kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo wa wilayani Geita, lakini baadaye serikali ilikataa kuendeleza mradi huo kwa sababu inazozijua.
  Kwamba mradi uliokuwa ukiendeshwa na kampuni hiyo, ungeisaidia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuhifadhi dhahabu hapa nchini na ungeisaidia serikali kujua kiasi cha dhahabu kinachopatikana nchini kuliko ilivyo sasa ambapo dhahabu inachimbwa na kusafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya kusafishwa, jambo linalosababisha taifa kushindwa kujua kiasi kinachochimbwa na wawekezaji katika sekta hiyo.
  Kwamba serikali sasa imeishinikiza BoT (iliyotoa pesa za uanzishaji) ijitoe kwenye kampuni hiyo na wiki tatu zilizopita BoT iliwasilisha rasmi kwenye bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo ya Mwananchi Gold kwamba imejitoa na hivyo sasa imebaki NDC peke yake. Aidha, aliwataja wanahisa wa Kampuni ya Mwananchi Trust, ambayo ipo ndani ya Mwananchi Gold Company Ltd kuwa ni Umoja Entertainment, VNB, WM Holding inayomilikiwa na Yusuph Mushi, na CCM Trust Company.
  Hata hivyo, serikali inapaswa kutueleza, ni kwanini ilianzisha Kampuni ya Mwananchi kwa nia njema kama hiyo kama alivyoeleza Warioba, halafu imeamua kujitoa? Kwanini ilichezea fedha za walipa kodi kuanzisha mradi ambao sasa imeamua kuuacha?
  Tunahoji usiri uliozingira suala zima linalohusu ubadhirifu wa fedha katika kampuni hii.
  Umefika wakati wa serikali kutupa majibu ya msingi, hasa juu ya busara iliyotumika ya kuacha kutekeleza mradi ambao ungelisaidia taifa.
  Viongozi wanafaidika nini kwa dhahabu kusafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya kusafishwa, wakati tayari kulishakuwa na uwezekano wa kuisafishia hapa nchini kwa kutumia Kampuni ya Mwananchi Gold.
  Pina tunahoji taratibu zilizofuatwa katika kutangaza na kupata wanahisa wa kampuni hiyo, ikiwemo CCM Trust.
  Tunahoji, CCM Trust ni nini? Ina uhusiano gani na Chama Cha Mapinduzi (CCM)? Tunataka majibu, kwani Warioba katufumbua macho.
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Jan 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jasusi,
  Ndio maana nawapenda Daima hawachelewi kuunganisha vitu...haya ndio maneno mkuu wangu.
   
 20. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #20
  Jan 18, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Ina maana Jaji anaogopa kivuli chake??hahhah kuelekea 2010 tutajifunza mengi sana kwenye utawala bora na wa sheria......
   
Loading...