Governor na noti mpya.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Governor na noti mpya....

Discussion in 'Jamii Photos' started by Rutashubanyuma, Dec 18, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,507
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Bank of Tanzania (BoT) Governor Prof Benno Ndulu displays samples of new banknotes to reporters ( not in picture), in Dar es Salaam on Friday. (Photo by Fadhili Akida)
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mbona hawajaweka PIC za Dr (5nr) au hajafanya vizuri upande huu!
   
 3. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watu wameshakula cha juu.....
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hiyo kawaida mkuu kila sehemu madalali wapo!
   
 5. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  BENKI KUU YA TANZANIA
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  TOLEO LA NOTI MPYA

  1. Benki kuu ya Tanzania imetoa toleo jipya la noti za shs 500, 1000, 2000, 10,000. Noti hizi zitaingizwa katika mzunguko tarehe 1 Januari 2011. Noti za zamani bado ni fedha halali na zina thamani sawa na zile mpya. Zitaendelea kutumika na kuwepo katika mzunguko sambamba na hili toleo jipya la noti mpaka hapo hizo za zamani zitakapotoweka taratibu na hatimaye kwisha kabisa kwenye mzunguko. Hivyo basi, wananchi wanashauriwa kuendelea kuzipokea na kuzitumia noti za zamani bila shaka au wasiwasi wowote kuhusu uhalali wake hadi hapo zitakapokwisha na kutoweka kabisa katika mzunguko. Vilevile ieleweke kuwa hakutakuwa na ubadilishaji wa kupeleka noti za zamani benki na kutaka kupewa mpya.
  2. Toleo hili la noti mpya lina taswira inayozingatia mandeleo ya uchumi na jamii. Tumefanya mabadiliko kidogo katika toleo jipya kwa kuweka picha za waasisi wa taifa letu. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anaonekana kwenye noti ya shilingi elfu moja na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kwenye noti ya shilingi mia tano. Noti tatu zilizosalia yaani elfu mbili, elfu tano na elfu kumi
  2
  zitaendelea kuwa na picha za wanyama pori ambao wanapatikana kwa wingi kwenye hifadhi na mbuga zetu za wanyama. Hata hivyo, kutokana na kupunguza ukubwa wa noti hizi mpya tumeweka picha za vichwa vya wanyama hao badala ya wanyama wazima kama ilivyo kwenye noti za zamani.
  3. Ili kupambana na uhalifu wa kughushi na kuongeza muda wa noti hizi kukaa katika mzunguko kwa muda mrefu kabla ya kuchakaa, toleo hili limeongezewa ubora kwa kuweka alama maalum mpya za usalama na kutumia taaluma mpya ya kuziimarisha. Alama mbali mbali za usalama zimeboreshwa na kwa mara ya kwanza kabisa alama ya “motion” ambayo ni rahisi sana kutambulika kwa macho imetumika katika noti hizi. Ili kuelimisha wananchi kuhusu alama za usalama zinazotambulisha uhalali wa noti zetu, tumetoa matangazo na vipeperushi ambavyo vitasambazwa sehemu mbali mbali za nchi. Taarifa ya alama za usalama za noti pia zipo kwenye tovuti ya Benki Kuu kwa anwani Bank of Tanzania (BOT): Home Page : Benki Kuu ya Tanzania
  4. Ni muhimu kwa umma kufahamu alama za usalama ili uweze kutofautisha noti halali na bandia kwa urahisi. Hata hivyo Benki Kuu inapenda kutahadharisha watu wawe waangalifu na kuzichunguza noti zote wanazopokea hasa kwenye giza ili kuhakikisha kwamba ni noti halali. Uchunguzi ufanywe kwa noti zote zilizopo kwenye mzunguko pamoja na za zamani. Endapo wana mashaka warejee kwenye mabango na vipeperushi vilivyotolewa na Benki Kuu au tawi lolote la Benki Kuu.
  Gavana
  Benki Kuu ya Tanzania
  17 Desemba 2010
   
 6. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  kwa nini hawajaweka picha Prof to be, Dr, Lt Col?
   
 7. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  sema uyo karume wamemuweka wa nini wakati wazanzibar wanatarajia kuachia ngazi?
   
 8. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Afadhali maana siajabu ningegomea mshahara

  Mi nilikuwa nangaja nione kama kutakuwa na noti ya 50,000/= na 100,000/= maana hii hali ya sasa ya kifedha inanipa mashaka miaka miwili ijayo
   
 9. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kweli ni kosa kubwa kutokutoa not za thamani kubwa zaidi ya 10,000.
   
 10. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2010
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Si lazima kila pesa mpya zinapotengenezwa kuweka picha ya Rais aliyepo madarakani
   
 11. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Sasa hizi tutumiazo zinakwama lini maana nna kijilaki kimoja huku mbali nimekiweka ili pandie taxi nikianguka bongo
   
 12. The Planner

  The Planner JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2010
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Regardless of the quality of our new notes Beno, what we need is the value of our currency!
   
Loading...