Government electronic Payment Gateway (GePG) Tanzania: Mapendekezo ya maboresho

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Pongezi lukuki kwa juhudi za Serikali-Mtandao, mfano mzuri ukiwa Government electronic Payment Gateway (GePG), mfumo wa malipo ya kielektroniki kwa serikali.

GePG imeleta maboresho makubwa kwa upande wa kuilipa serikali, kwani sasa hivi unaweza kuilipa serikali ya Tanzania uwapo popote Tanzania. Sasa unaweza kuilipa serikali na taasisi zake kwa njia za kielektroniki kutokea kwenye simu, kupitia kwa mawakala na hata kwa mabenki.

Yafuatayo ni mapendekezo kuboresha zaidi huduma hizi.


1. Business Process

Baadhi ya huduma zinazotolewa na serikali taratibu zake (business process) hulazimisha mtu kwenda kupata huduma ofisini. Huduma nyingine kweli pana umuhimu wa kwenda ofisini, lakini nyingine hazina umuhimu wala ulazima.

Kwa mfano,

(a) Baada ya kufanya malipo kwa GePG, ofisi ya umma inakuambia ulete uthibitisho wa malipo. Hii haina mantiki kwa vile kwa mfumo wa kieletroniki wao wanatakiwa waweze kufikia sehemu ya kiutawala ( backend) ya GePG kujua nini kimelipiwa au bado. Afisi za serikali zingekatazwa kudai uthibitisho wa malipo kwa kitu chochote kilicholipiwa kielektroniki. Ofisi hizo ndio ziseme kitu hiki kimelipiwa au la. Wadai uthibitisho pale tu panapokuwa na sintofahamu ya mtu kuwa amelipia na wao wanasema hapajalipiwa.

(b) Kuendana na (a) hapo juu, kila ofisi inayopokea malipo kwa GePG, iweze kutoa risiti za kielektroniki (self-service) kwa kila malipo. Risiti hizo zitumwe kwa barua pepe au ziwepo kwenye app ya simu na website ya GePG. Mtu atakayetaka kupata nakala ngumu, ndie ajipatie usumbufu wa kwenda ofisini kuomba nakala ya risiti.

(c) Kila mwananchi au mlipaji mwingine aweze kuwa na uwezo wa kujitengenezea ankara za malipo, kulipa, na kuwa na uwezo wa kujionea historia ya malipo mbalimbali aliyofanya kwa serikali.

(d) Helpdesk ya GePG iwekewe sehemu ya kujiandikisha ili kuitumia. Kwa sasa http://helpdesk.gepg.go.tz/ haina huduma hiyo.

(e) Pesa za kigeni -- sina hakika iwapo GePG inaweza kuzipokea. Kwa sasa baadhi ya huduma ni za kwa ajili ya watu walioko nje ya Tanzania. GePG iwezeshe watu kuilipa serikali kwa njia yoyote inayowezeckana. Mf. Visa na Mastercard, Paypal, Skrill, n.k., na kwa pesa kadhaa za kigeni, na hata cryptocurrencies. Kufikia hili, GePG inaweza pia kushirikiana na payment gateway za binafsi zitakazokuwa zikiongea na GePG. Mfano wa gateway hizo ni Directpay Online (https://www.directpay.online/online-payments-tanzania/) , Lipa (http://lipa.co.tz/) na hata paypal (www.paypal.com).

Uwezekano mkubwa huduma hizo tayari zipo, ila tu awareness kwa public bado.

End of Feature Requests.
 
Mlenge
Nadhani mfumo haujakamilika kwa namna fulani.
Kwa uliyoeleza kunakosekana '' link'' kati ya mtoa huduma(serikali) , Mlipaji (Mteja).

Kiunganisho kinachokosekana ni Bank (X) au mfumo mwingine wenye kiunganisho kati.

Malipo hayafanyiki kwenda Taasisi husika, bali hupitia bank(X) kufikia taasisi hiyo

Kama ni Tanesco, kuna account ya Tanesco bank X(Kataumeme1).

Mteja naye ana account#(Bill123) ambayo si ya bank bali account yake Tanesco( Hapa watu wasichanganye). Mita yako au Bill yako ndiyo account # yako( Bill123)

Halafu kuna account yako(mteja) ya Bank( acc. # Bnk0000.)

Mteja anahamisha pesa kutoka account yake(Bnk000) ya Bank kwenda account ya Tanesco ya Bank.(Kataumeme1)

Bank husika(X) inapewa account # za Wateja hapa ni (Bill123)

Kwahiyo Mteja anapolipa, anatoa pesa kwenye account yake ya Bank(Bnk000), analipa account yake ya Tanesco (Bill #123) iliyoorodheshwa Bank (X) ili malipo yaingie account ya Bank ya Tanesco(Kataumeme1) ndani ya Bank X kutoka kwa mteja(Bnk000)

Mfano huo utahusu wizara na Taasisi zote ambazo kila asubuhi zitasoma mteja mwenye account # abcd au kama ni wizara ya ardhi kiwanja 000tofali, amelipa kiasi Y kutoka account yake ya Bank X kwenda kwenye account ya Wizara F katika Bank X yenye orodha ya Wateja na ccount zao (Bill)

Mtu anapoambiwa akathibitishe ina maana Taasisi husika haujui kama malipo yamefanyika hata kama account inaonyesha kuingia kwa pesa. I mean Taasisi haijui nani kafanya malipo.

Sababu kubwa ni kukosa link kati ya Taasisi, Bank, na Mteja.

Mfumo wa kielektroni ni mzuri sana unarahisisha malipo, unaokoa muda, unapunguza wizi, na unazuia kubeba mabunda ya pesa bila sababu.
 
Mlenge
Nadhani mfumo haujakamilika kwa namna fulani. Kwa uliyoeleza kunakosekana '' link'' kati ya mtoa huduma(serikali) , Mlipaji (Mteja).
.....

Mtu anapoambiwa akathibitishe ina maana Taasisi husika haujui kama malipo yamefanyika hata kama account inaonyesha kuingia kwa pesa. I mean Taasisi haijui nani kafanya malipo.

Sababu kubwa ni kukosa link kati ya Taasisi, Bank, na Mteja.

Mfumo wa kielektroni ni mzuri sana unarahisisha malipo, unaokoa muda, unapunguza wizi, na unazuia kubeba mabunda ya pesa bila sababu.

Nguruvi3

Uliyoyaeleza ni valid kwamba ndivyo baadhi ya maafisa wanainsinuate. Katika hali halisi, GePG haitumii mabenki kama proxy as far as the user is concerned. Mabenki, etc, ni transparent to the user. Ndio maana siku hizi hawatumii tena account number, ila control number. Unaweza kuilipa serikali kwa kutumia control number, ukitumia simu (Mpesa, nk.,) au kutumia benki.

Wenyewe kule GePG wanajua control number hii ni ya kulipia nini, amount gani, na custodian ni taasisi gani. Final stop ya pesa ni transparent to the user, lakini anachoona ni kwamba malipo yamefanyika au la. Wameweka USSD code ya *152*00# ambako unaweza kuangalia control number yako ni ya nini, kiasi chake, na iwapo imeshalipiwa. Japo baadhi ya control number ukishalipia zinayeyuka kwa kusema control number is invalid. Sijui hii ni feature au bug.

Kizuizi kikubwa ni kwamba taratibu (business process) iliyozoeleka ni kwamba mteja anaambiwa alete photokopi ya deposit slip ya benki. Ukilipia kwenye simu ni vigumu kuja na hiyo hard copy. Ukimkuta mtumishi aliyezoea utaratibu wa fotokopi, halafu umwambie nishalipia, hakuelewi. Utakuta analazimisha (kalipie benki) ulete slipu. Tatizo kubwa nadhani ni haya makompyuta ni ya siku hizi, na baadhi ya watumishi au ofisi hawajaendana na kasi ya mabadiliko ya TEHAMA.

Isitoshe kwa whichever mamlaka is behind GePG kulazimisha taasisi za umma kutumia mfumo huo, bali iende extra mile kuwapa miongozo inayoelekeza, miongoni mwa mambo mengine, marufuku ya kumdai mtu hard copy au uthibitisho wa malipo, au hata kudai control number. Taasisi inatakiwa iseme yenyewe kitu hiki kimelipiwa au hakikulipiwa.
 
"Mlenge, post: 32564799, member: 450"]Wenyewe kule GePG wanajua control number hii ni ya kulipia nini, amount gani, na custodian ni taasisi gani
Haswaa
Kizuizi kikubwa ni kwamba taratibu (business process) iliyozoeleka ni kwamba mteja anaambiwa alete photokopi ya deposit slip ya benki.
Mazoea tu hakuna sababu za kitalaam. Watu wamezoea kuona photocopy hata kama ni ya kughushi
Ukilipia kwenye simu ni vigumu kuja na hiyo hard copy. Ukimkuta mtumishi aliyezoea utaratibu wa fotokopi, halafu umwambie nishalipia, hakuelewi. Utakuta analazimisha (kalipie benki) ulete slipu.
Hakufahamishwa mfumo unafanyaje kazi na haelewi details
Tatizo kubwa nadhani ni haya makompyuta ni ya siku hizi, na baadhi ya watumishi au ofisi hawajaendana na kasi ya mabadiliko ya TEHAMA.
Tatizo nadhani si kompyuta, ni maarifa ya kutumia. Mtumishi huyo anaweza ku google lakini hajui info za malipo zinapatikanaje kwa kompyuta hiyo hiyo
Isitoshe kwa whichever mamlaka is behind GePG kulazimisha taasisi za umma kutumia mfumo huo, bali iende extra mile kuwapa miongozo inayoelekeza, miongoni mwa mambo mengine, marufuku ya kumdai mtu hard copy au uthibitisho wa malipo, au hata kudai control number. Taasisi inatakiwa iseme yenyewe kitu hiki kimelipiwa au hakikulipiwa.
Na hili ni tatizo kweli kwetu kila siku tunatanguliza mikokoteni mbele ya farasi. Hao watu wa GePG walipaswa kutoa elimu kwanza, mfumo unafanyaje kazi ili watumishi waelewe.

Watumishi wetu nao ni tatizo, ilimradi kaajiriwa hana haja ya kujua mambo kuhusu kazi yake.
Sina uhakika hao wahasibu wanatoa elimu kuhusu matumizi ya mfumo

Hivi taasisi inalipwaje, na pesa zimeingia halafu taasisi hiyo hiyo haijui nani kalipa na kiasi gani!

Inatia kinyaa! kwamba, Mhasibu akikuta milioni 10 siku ya kwanza, milioni 15 siku ya pili wala hajishughulishi kujua nani kalipa.

Na hili si suala gumu kwa kutumia kompyuta, ni suala la weledi na utashi tu

Inaudhi sana mtu kalipa halafu afunge safari kwenda ofisini na photocopy au nyaraka za bank!!
It defies logic of TEHEMA. Kama ni hivyo si afadhali mtu abebe mabunda yake
 
Back
Top Bottom