Google wazuiwa kupiga picha karibu na kijijini kwetu cyber. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Google wazuiwa kupiga picha karibu na kijijini kwetu cyber.

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Richard, Apr 4, 2009.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Google wapo katika mpango wa kuchukua picha za barabara zote katika nchi nzima ya Uingereza, katika kujaribu kutengeneza tovuti (website) iitwayo kwa kiingereza Street View mapping.

  [​IMG]
  Gari la Google likipita kupiga picha

  Lakini walipofika karibu na kijiji nnachoishi cha Cyber, gari ya watu wa Google aina ya Opel Astra ilianza kuchukua picha kwenye kijiji jirani kiitwacho Broughton, ndipo wananchi waishio katika kijiji hicho waliposimama katikati ya barabara na kuzuia njia ili gari hio isipite na isifanye kazi yake ya kuchukua picha.

  Ndipo wananchi wote tuishio vijiji vya jirani tulipopata taarifa na kuunga mkono mgomo huo na baadae dereva wa gari hi alipogeuza na kurudi alipotoka. Mmoja wa wanakijiji akaita polisi na baada ya dakika chache polisi walifika eneo la tukio na kusikiliza madai yetu.

  Kwamba Google wanaingilia uhuru wetu wa faragha kiasi cha kuchukua picha za mitaa yetu bila ridhaa yetu wananchi na kuanika katika hio tovuti yao.

  Pili watu wa google wanarahisisha kazi kwa wezi kun’gamua ni wapi wanaweza kwenda kuiba kwa urahisi kwa kufuata hio “Street View” mapping.

  Tatu watu wa google wanasaidia kitendo cha wizi.

  Polisi waliposikiliza madai hayo wakaona kuna “sense” na wakamshauri mhandishi na dereva wa gari hilo aondoke katika eneo hilo.

  Hapo kabla kumekuwa matukio matatu ya wizi ambapo wezi wamevunja nyumba za watu na kukwiba na kuwepo kwa usaidizi wa tovuti hii kutasaidia wizi huo kuongezeka.

  Gari hilo la google lina mkonga ambao umening’inizwa “camera” ambayo ina uwezo wa kuzunguka nyuzi 360 na picha zinakuwa zikichukuliwa kila baada ya sekunde mbili chache kutoka kila eneo. Hii inawasaidia watu popote pale walipo duniani kuandika anuani ya sehemu yoyote ile katika tovuti ya Google kwa minajili ya kutafuta na kupewa majibu ndani ya sekunde chache tu. Pia picha za nyumba, bustani, majengo na vitu vingine muhimu vitaweza kuoneshwa.

  Kwa hio mtindo huu umekuwa ni maarufu kwa watalii na watu wengine lakini kwa sasa umezua mabalaa kwa kuonesha picha za waume za watu wakiwa wanatoka nje ya nyumba za vimada wao au kwa wake pia kuonekana hivyo hivyo kutoka kwa mabwana zao, wengine kuonekana wakiwa wanaumwa barabarani na hali hii imeonekana kuingilia uhuru wa faragha kwa wananchi.

  Kibaya zaidi ni kesi ya kuachana (divorce) ambapo mama anadai gari aina ya Range Rover la baba lilionekana limepaki nje ya nyumba ya rafiki yake wa kike wakati baba alisema amekwenda kwenye safari ya kibiashara.


  Watu wa Google wamejitetea kwa kusema kwamba picha zote huondolewa pale mtu anapohitaji hivyo.

  Mkuu Steve D na wengine mnaonaje kuja kwa Google latitude?
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkuu, kwanza kabisa, poleni kwa kuingiliwa kijijini kwenu na watu wa Google. Hata hivyo siamini kama google wana lengo lolote lililobaya, lengo lao kubwa ni kuunganisha information duniani kote na kuzifanya ziwe accessible and may be generate few billions on top of that from multinationals. Tatizo tunaishi kwenye jamii zenye kila aina ya watu, kuanzia kwa wale waliokuwa wahalifu wa kutupwa, mpaka wale wa kushinda kwenye kwenye sehemu ya kuwasujudu miungu wao.

  Katika swala hili, naamini kabisa kama tu vile Google maps zilivyokuwa indispensable, street view pia in the future if responsibly used inaweza kabisa kuwa invaluable tool to business and individuals alike. One important thing to bear in mind is that, no matter what kind of objection we put forth to suppress technological influenced processes such as this google's street view, always, and emphatically always, there will be another person/entity out there that will take over and carry out the same process, be it directly or indirectly. The big craze currently arising to fend off Google, in my opinion, i think is highly a judgmental case for loathe of the giants and the likely backing up of the underdogs, something peculiar nonetheless typical of the Brits.

  Rich, kubali kuwa at one point in the future phone cameras na handhelds nyinginezo zitaweza kabisa kufanikisha kile ambacho google wanataka kukifanya hivi sasa kwa kutumia mitambo mikubwa mikubwa. Isitoshe kuna project moja (kama sijakosea ni ya Microsoft) ambayo inafanya jitihada za kukusanya picha mbalimbali kutoka kwa watu wote duniani na kuziunganisha ili kupata 3D ya pahali popote pale ambapo picha mbalimbali zimepigwa na watu tofauti katika angle tofauti tofauti. So hata tukatae leo hii, baada ya muda, kuna Mchina mmoja huko Hunan au au Mhindi mmoja kutoka Mysore India, atakuja na kitu kama hicho hicho kwa kutumia mlango wa nyuma.

  Baadae mkuu,

  SteveD.
   
 3. K

  Kwaminchi Senior Member

  #3
  Apr 4, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nafikiri ni kazi bure kuwazuia. Watakuwa weshapiga hizo picha. Siku hizi picha hupigwa huku wapiga picha wapo mgahawani wanakunywa chai au kahawa. Ukweli ni kuwa wanapoombwa au kulalamikiwa wanakubali kuziondoa.
   
 4. SnEafer

  SnEafer Senior Member

  #4
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I also agree that its useless standing on the roads because they'll probably use their satellites and if the gov. agrees to them then thats the hardest part.
  But you still have free of speech so no one will shut you up ;-)

  But i think its a good idea having the street view way, i mean as you said, no theif will now need to walk around the street and start taking the victim's pictures, they could easily just use those. i mean it draws everything all needed is to print them out hehehe , ***ok that wasn't funny***

  cheers
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Labda sijawaelewa wakuu especially mleta mada, au pia sijaelewa aina ya picha ambazo Google wanataka kuzichukua. Lakini street views ninazozijua mimi zimenisaidia sana wakati nilipokuwa nchi fulani huko ugenini ktk kusaidia kufika sehemu nilizotaka kwenda.

  Kitendo cha kuwazuia Google kuchukua hizo street view nakiona kama ni kitendo cha kiswahili flani hivi, na sio cha kupongezwa hata kidogo.
   
 6. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapana.

  Baada tu ya kuzuiwa gari hili halijachukua tena picha na zile zilizopatikana ndizo hizohizo.

  Hivo kijiji cha Cyber hakipo katika tovuti ya Google mpaka sasa, kwa hio haya ni mafanikio ya mgomo wa wananchi, kwamba hatutaki picha zichukuliwe bila ridhaa yetu na hii imeeleweka kwa polisi.
   
 7. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280

  Mkuu Street View mapping alifanyika zamani sana na mpaka sasa tunatumia map books ambazo hupatikana madukani kwa bei rahisi tu.

  Halafu isitoshe kwa wale tutumiao GPS ambayo imo hata katika simu zetu za mkononi hii software ya GPS tayari imekuwa "fed" na "details" zote kuhusu "features" kama majengo ya umma, vivutio vya utalii, shule, na mambo mengine yanayolingana na hayo.

  Kinachopingwa hapa ni kitendo cha kuchukua picha halisi za sehemu mbalimbali ambazo haziusiani na hitaji la mtafutaji kama vile nyumba za watu hii ni kuingilia faragha za watu.

  Mwisho kuwazuia Google kuchukua picha si kitendo cha kiswahili fulani hivi bali ni haki ya msingi ya wale ambao wanaelewa kuhusu hizo haki ambazo kwa watu wengine hawazijui tangu wazaliwe mpaka wanakuwa watu wazima.

  Ni hayo tu mkuu.
   
 8. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  The protesters were angry for a good reason. Until this year, no one could recall a crime in Broughton. But the village sits on the edge of the Milton Keynes conurbation.

  In recent months, a huge housing development has opened up on what used to be farmland. The population of 60 shot up to 2,000. And that means richer pickings and easier access for criminals.

  Natutrally, no one can blame Google. But it rams home the need for greater security in a place like this. And Google can only undermine that security.

  I have no objection with Google portraying the way villages and towns look, but they are crossing the line when they show every detail of our homes.
   
 9. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  It is too late.

  Sioni ni jambo gani litawazuia Google katika mradi wao.
  Ni kawaida kabisa kwetu binadamu kuogopa Technolojia mpya.

  Mwizi atatumia Google kutaka kukuibia na wewe utatumia Google kumzuia asikuibie.

  Enzi za Farasi watu waliogopa ujio wa Magari.
  Watu waliogopa sana ujio wa computer.
  Watu waliogopa ujio wa simu za mikononi.

  Watu wanaogopa sana Nanotechnology.
  Watu wanaogopa sana Sterncell research.

  Technolojia ikipamba moto hakuta kuwa na haja ya Google kupita na gari na likamera juu yake.
  Watapiga picha wakiwa wamekaa kwenye viti vyao ofisini.
   
 10. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135

  Hilo si tatizo la Google hata kidogo.
  Ni tatizo la huyo jamaa na filimbi yake.

  Ungetokea moto au ajali yeyote hapo jirani na News Media kuja na kupiga mapicha gari la huyo Mzinzi lingepigwa picha.

  Hapo vipi angelaumu Moto au vyombo vya habari???
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Labda kama bado sijaelewa hiyo street view iliyokuwa inatengezwa, lakini nadhani some people are being overalarmed and creating a fuss for nothing at all. Hiyo simu yako yenye GPS na hizo map books, mimi niliye Tz kwa mfano nita-acess vipi? Au kwa sababu ni mtaani kwako basi unajipa hati miliki na kujifikiria wewe tu?

  Njia muafaka kabisa ni ya kutengeza street maps na street views ili hata mgeni aweze kufika na anaweza kuzipata online free of charge.

  Personally, hii huduma nimeitumia na imeweza kunisaidia kufika nilipotaka kwenda kwa kuangalia map ya ninapokwenda na street view yake na jengo lenyewe ninaloenda na front door ni upande gani etc, hivyo bado nashikilia kuwa hicho kitendo cha kuwazuia jamaa kuchukua picha ni cha kiswahili (samahani kama nimekukwaza)
   
 12. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Lol

  Hapana wala hujanikwaza, ushwahili si unajulikana mkuu? Mimi ni mtu wa pwani lakini si mswahili lol.
   
Loading...