Google: Watanzania hutafuta nini mtandaoni?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Watanzania hutafuta nini mtandaoni?

_92997886_41eb98f1-0b76-4c0d-a590-f875193d433d.jpg
Image copyright AFP/GETTY
Kampuni ya Google imetoa ripoti ya mambo ambayo Watanzania walitafuta sana mtandaoni mwaka 2016.


Maelezo waliyotafuta yameangazia masuala ya afya, biashara na fedha na pia burudani.

Pia, yapo masuala ya kijamii.


Walichotafuta sana mtandaoni ni matokeo ya darasa la saba 2016, zikifuatwa na Beka Boy, mtandao wa burudani.

Walitafuta pia Mkekabet, ambao ni mtandao wa kuweka dau kuhusu matokeo ya mechi za kandanda na mashindano mengine ya kimichezo.

Walitafuta pia habari kuhusu matokeo ya kidato cha nne 2016, pamoja na Raymond, ambapo walitaka habari na maelezo kumhusu mwanamuziki Hekima Raymond mzaliwa wa Moshi, Tanzania.

Walitaka kujua kufanya nini?
Watanzania walitaka sana kujua jinsi ya kuweka tone la dawa jichoni, ikifuatwa na jinsi ya kuwapata wawekezaji na wafadhili.

Walitaka pia kujua sana jinsi ya kukuza nyusi na pia jinsi ya kujua mwanamke atajifungua tarehe gani.

Huenda kukoroma likawa tatizo linalowasumbua wengi kwani, kwenye nambari tano, Watanzania walitaka kujua jinsi ya kuacha kukoroma.

Kujua maana
Katika maneno ambayo Watanzania walitafuta sana maana, nambari tatu kuna neno la kushangaza 'Bae'.

Ni ufupisho wa neno 'Babe', mtoto au mpenzi kwa Kiingereza. Pia ni akronimi ya before anyone else, kabla ya wengine wote.

Kuna wimbo wa Sauti Sol na Alikiba kwa jina Unconditionally Bae, ambao huenda uliwafanya wengi kutaka kujua maana ya 'Bae'.

Mambo yaliyotafutwa sana Tanzania 2016:
  1. matokeo ya darasa la saba 2016
  2. beka boy
  3. mkekabet
  4. salehe jembe juni 26 2016
  5. Malazi Arusha
  6. euro 2016
  7. matokeo ya kidato cha nne 2016
  8. yinga media
  9. muungwana
  10. Raymond
Walichotaka kujua sana kufanya:
  1. Jinsi ya kuweka tone la dawa jichoni
  2. Jinsi ya kupata wawekezaji/wafadhili
  3. Jinsi ya kukuza nyusi
  4. Jinsi ya kujua tarehe ya kujifungua
  5. Jinsi ya kuacha kukoroma
  6. Jinsi ya kufanya cd kuweza kuifungulia kompyuta
  7. Jinsi ya kuomba na ubani
  8. Jinsi ya kupika danish na croissant
  9. Jinsi ya kuanzisha kiwanda cha chokoleti
  10. Jinsi ya kujua iwapo mtoto amegeuka
Ni nini:
  1. Malengo ni nini
  2. Bae maana yake ni nini
  3. Elimu rasmi ni nini
  4. Ndoa ya wake wengi ni nini
  5. Hesabu ya jumla ni nini
  6. Matumizi ya pesa ni nini
  7. Soko la kubadilishana sarafu za kigeni ni nini
  8. Mfumo ni nini
  9. Ghala ni nini
Dah haya ndiyo watanzania wametaka kuyajua Google na wewe uko wapi?
 
[HASHTAG]#freemaxencemelo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#TunamtakaBenAkiwaHai[/HASHTAG]
[HASHTAG]#JusticeForLema[/HASHTAG]
[HASHTAG]#usirudiekosa2020[/HASHTAG]
 
Hapo kwenye beka boy na yinga media ni matokeo ya kusearch vitu vingine kabisa, unakuwa reffered huko na google yenyewe
 
Hapo kwenye beka boy na yinga media ni matokeo ya kusearch vitu vingine kabisa, unakuwa reffered huko na google yenyewe
Siku hizi watu hawahangaishi vichwa, hata majina ya watoto wanaingia Google...so akisikia jambo lolote lazima agoogle kwanza ndio madhara yake haya.
 
Aisee kwa kuwa jana kuna mtu
Alitoa post, Google: wakenya wanatafuta nini mtandaoni?

Sasa na nyie naona mmeamua kulipiza
Manyani nyie
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom