Google map . Kwa nn mikoa mingine ya tanzania haiko detailed...?

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,938
1,437
Yap wa kuu juwaa la teknolojia ni aje bajameni.......

Nilikuwa ninacheki google map ya tanzania lakini nikashangaa. Mnaweza kuisahihsia au unilekeza kama una kitu naoneana kutojua

  • Google map information za majina ya mitaa na bara bara za dar zilizokuwa published walizitoa au wanazitoa wapi ?
  • Mbona na wilaya nyingine za tanzania information zake haziko detailed kama ilivyo dar es saalaam ( mambo kama majina Bara bara, mitaaa ,nk)?
  • Nini kinatakiwa kufanyika detail hizi za mitaa na majina ya barabara za mikoa na wilaya nyingi zaidi ziingie kwenye gooogle map?
  • Ni wajibu wa nani kutoa detail hizo?
  • Je wizara ya ardhi au hata wizara ya utalii hakuna watu ambao wajibu wao wa kila siku unahusiana na Google map. kama hakuna hawalifikiria hilo?
Inashangaza hata ile mikoa kama Arusha, Mbeya Dodoma, Tanga, Mwanza nayo detail zake sio nyingi. Nomba kama mwenye ujuzi jinsi google inavyopta information za gmap na mwenye jibu hasa la swali nililoblue anipe

Nawasilisha
 
sina jibu halisi kuwa nani anapaswa au mhusika mkuu lkn ukiwa na account google na ukalog-in unaweza kuongeza majina ya mahali fulani ukiangalia kama dar au arusha na sehemu nyingine utakuta hadi hoteli zimewekwa kwa majina ila tatizo ukitumia google earth utaona baadhi ya maeneo picha zake zilichukuliwa hata zaidi ya miaka mitatu iliyopita. Huenda kuna gharama kubwa ktk kuweka ramani za miji au kuchukua taswira halisi.
 
thank you Never give up

Ndio maana nilipenda kujua kujua mfano kwa dar unana sehemu nyingi tu vyuo kama DIT . anadhani sheemu za huduma za jamii hawalipii sina uhakika na hoteli lakini nadhani somehow serikali inatakiwa kushiriki kutangza zile sehemu zenye manfuaa kitaifi. sasa Mikoani ndio kuna shemu chache sana.

Je hotel kama new africa wanalipa google. DIT wanalipa google?

mimi nikiingia na ku-mark sehemu fulani nitaziona wenye custom map yangu . Sasa nilitaka ujua tunatakiwa kufanya nini kam watanzania ili japo hata majina ya mitaa na barabarabara za mikoa na wilaya zingine amabayoo naamini ni bure tuyaingize kwenye Ramani ya dunia ya google .

kuna meya wa jiji la rio de jenairo Brazil aliwakoromea google sababu katika satelite picha moja walichukua eneo la slum viizuri wakaacha kuchukua eneo la uzunguni vizuri. huyu ni meya wa ikzazi cha sayansi na teknolojia. googe ilibidi warekeishe image zile ili kuweza ku balansi. Huyu meya wa rio de jenairo alisema kila baada ya siku chache lazima angalie google map ya jiji lake.

Sasa sisi watanzania je ni mameya wangapi wa majiji wanajua hata google map inaonyeshaje mji wake? viongozi wa Arusha, lushoto. kilimanjaro wanaelewa hata hao watali siku hizi googlemap imekuwa reference point muhimu.
 
Google Maps inamilikiwa na Google na wao ndo wanaoamua ni ramani za wapi wataziongeza kutokana na malengo yao ya kibiashara.
Kama unauchungu na hilo nakushauri uende OpenStreet Map OpenStreetMap hii ni Open Source map ambayo mtu yoyote anaweza kuchangia,so anza kuchora.
 
Kang

lakini kuna meya wa rio de jenairo aliwakorormea google kwa kutoonyesha vizuri ramani na picha za mitaa jiji lake. Mbona gooogle walirekebisha.

Kweli nina uchungu lakini nadhani ni jukumu la seriali kupitia wizara ya ardhi kuhakikisha ramani japo za mikoa yote zinakuwa detailed . kwa kuweka tu majina ya mitaa na majina ya barabara sidhani kama kuna cost kubwa.

nitaicheki hiyo site lakini nadhani gmap ndio first refence ya watu wengi kwa sasa.
 
mikoa gani hiyo...? au mkoa mpya wa ushetu?huo mpaka jk adaini na hivi yuko marekani atawaamvia google wauwekee details
 
mkuu google map kwa kiasi kikubwa huwa inatengenezwa na watumiaji wenyewe...watumiaji ndio tunanafasi kubwa ya ku update location na details mbalimbali za mahali husika...mtu anatakiwa kuwa na account ya google tu kufanya hivyo na kimsingi ni free isipokuwa kwa huduma nyingine chache zaidi za kibiashara ambazo huwa zinalipiwa ila kwa kiasi kikubwa ni free for normal adding of details. Google hawawezi kuzunguka dunia nzima kuweka details za kila mahali na hata hizo sehemu unazoona zimeelekezwa vizuri ni kwa sababu ya kuwa na watumiaji wengi wa huduma hii na wanachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza details za mahali...tatizo watanzania wengi hatufatilii hili...si wananchi wala serikali...na ndo maana kuna mikoa mpaka leo unakuta zina details ni za mwaka 47...
 
Sijui nini
Nimfeanyia utafiti majibu yako nimeona ni ya kweli . kumbe hizi detail hata watanzania tunaweza kuingiza kwa kutumia Googlemapmaker .Lakini ukifanya editing inachukua muda. Na sijui kama inaweza kukubalika. So nadhani serikali kupitia wizara ya ardhi Ingetaumia hata vijana wa mwaka waa kwanza wa chuo cha ardhi au vyuo vyao vingine kuwaambia waingize detail zaidi za majina ya bara bara, mitaa na sehemu za huduma za jamii za mikoa na wilaya zote .

Wizara ya ardhi kama wako makini wawasiliane na google ili wawape majina waatu maalum amabao editing watakazofanya zitakuwa populated na updated chap chap. na sidhani kama kuna cost kwa kuandika majina na urefu wa wa bara bara na mitaa , majina ya shule, hospitali ,vituo vya mabasi...

Kwenye a haka ka blog kangu ka mazoezi nimejaribu kuingiza jina la mtaa au bara barana ya Ally sykes mbezi beach dar es salaaam. Utauona nimeweka kwa rangi ya blue.

Lakini kwenye ramani ya google inayoonekana kwa watu wote duniani hizo changes wanasema ziko pending mpaka zitapokuwa reviewed na kukubalika. ndio hilo jina pia llitaonekana......

....
Changes pending approval
tiny_icon_orange.png
Road
Mbezi Beach, Kawe, Dar es Salaam, Kinondoni

Category: Road
Status:Pending

Sasa ni mambo kama haya yakifanyika. ndio yanatoa hata ooprtunities za watu wengine na wataalam kutengeneza apps kama za na GPS na aps kama za driving drirections za kitanzania tena za kiswahili...... Wizara ya ARDHIIIIIIIIII AMKENIIIIIIIII

Wakati wizara yetu ya ardhi ambao bo ni wahusika halisi wamelala watanzania tujairbu kuingiza details za wilaya na vijiji vyetu na hata majina ya bara bara , shule, hospitali na maeneo yanayotua huduma za kijamii.

mikoa gani hiyo...? au mkoa mpya wa ushetu?huo mpaka jk adaini na hivi yuko marekani atawaamvia google wauwekee details

Kigogo aksante kwa mchango wako lakini sioni hiii issue inahusianaje na JK. Sio lawama zote ni JK jamani. Hizi detail zinaweza kuingizwak ama wizara ya ardhi au hata ofisi za kila mikoa zinaweza kuajiri watu wa data entry kwa contract ya mwaka mmoja. wakafanya kazi hiyo.
 
ni kweli kwamba kuna baadhi ya sehemu mathalani mji wa morogoro karibia nusu ya mji haionyeshwi kwenye satellite view,maeneo kama chamwino,mazimbu,modeco,na kihonda yote ukifungua unaona ukungu wa kijani,je hii kampuni ya google haina wawakilishi hapa tz warekebishe hilo???
 
Picha za satellite ni gharama ndo maana Google sio rahisi kulipia picha kwa satellite kwenye eneo ambalo halina maana kwa biashara yao.
 
Google hawana business interest kubwa kwenye nchi zetu changa na masikini . Ni sisi wenyewe na hasa serikali yetu ndio ina nafasi nzuri na resouces kupitia wizara ya ardhi na vyuo vyake wanatakiwa wafanye mambo. Sio kuhubiri sayansi na teknoljia majukwaani wakati bado ramani za vijiji na miji wanahifadhi kwenye makabati. Ukitokea mgogoro ukienda ofisi ya mkoa au wilaya unaambiwa ramani imechanika na copy iko moja mpaka makao makuu . Sasa hii google map haichaniki

Picha za satellite ni gharama ndo maana Google sio rahisi kulipia picha kwa satellite kwenye eneo ambalo halina maana kwa biashara yao.

Kang
nachoongelea mimi kuna mitaa hata ya dar haina majina unaona miraba miraba tu. na hakuna vituo muhimu kama vya mabasi. Haya tunaweza kuingiza lakini wahusika wakuu ni wizara ya ardhi . Hizo ramani walizonazo makabatini kwa nini wasupdatet google map ipate nyama nyama na detail zaidi.

Pale tangi bovu kuna kituo cha BP ipo kweye gogle map na kanisa la lutheran lipo. Je hao wamelipia.....?
 
Hiii ni resposne kutoka kwa watu wa google kuhusu edit niliyataka kufanya kuongeza jina la kituo cha basi na taxi pamoja na jina la mtaa mmoja

Comment 11 hours 43 mins ago by Google Reviewer Uma
Hi, Please provide valid reason for the priority and popularity change of the feature. Thanks.

Kwa hiyo inawezekana na usumbufu unaweza kuwa mdogo kama serikali officialy ikiomba na kuwaadikia google majina ya eg 10 or 20 inidividuals ambao changes watakaazofanya zitakubaliwa haraka haraka bila kupitia scrutiny. na ni bure
 
Picha za satellite ni gharama ndo maana Google sio rahisi kulipia picha kwa satellite kwenye eneo ambalo halina maana kwa biashara yao.

Uhamiaji HQ kurasini pameanza kujengwa 2007 na 2010 wakaanza kutumia jengo lao lkn ajabu ukienda ktk satellite view pale mahali panaonyesha kiwanja tu, hii inaonyesha wkt mwingine hawana mpangilio maana kuna eneo langu la shamba kibaha kuna kibanda tu tena hakina hata mwaka lkn hili eneo limechukuliwa
 
Sidhani kama google wana ulazima wa kuweka details za sehemu ambayo mtu binafsi anaona umuhimu! Kama alivyosema mdau mmoja hapo juu, picha za sattelite ni gharama, na gharama hizo zinalipwa na google; na ni gharama zaidi kuweka street level details kwa sababu inahitakika timu ya ardhini! Na kama wangeacha wazi kwa mtu kuedit bila kureview na kuona ukweli na umuhimu wa info unayotaka kuingiza, usishangae Downing St imeandikwa Bibi Titi St. hahahaa
 
Amoeba
Ni kweli google hawana ulazima wa kuweka detail za majina tena sehemu ambayo wanajua hawawezi kupata faida. lakini google hao hao wametoa nafasi za watuamiji kuweka input za majina ya mitaaa ,bara bara na hata sehmu za public bure.

Nimechunguza hata mitaa ya kati kati ya jijii kuna majina ya waliochangia . Sasa itakuwa aibu kama katika hao wachangji hakuna muhusika wa wizara ya ardhi au wa TANROADS.

Mfano nenda hapa Google Map Maker

uki kuzoom jiji la dar maeneo ya kati utoon chini ya ramani kuna contrubutor . Kuna mjina kama Omar, Salim khatri, Sayed Jafar ,kidogo na wengineo

Kwa hiyo hata ukiona google map ya dar kati kuna majina kama zanaki street, jamuhuri street morogoro road inawezeana sio Juhudi za serikali wala vyombo husika ni juhusi za watu binafis kama kina Sayed. Sasa hapo tutasema serikali yetu iko makini na sayansi na teknolojia????

Kwa hiyo sio suala la gharama kama watu wanvyodai. Ramani za google zinaonyesha mitaa lakini mitaaa haina majina. Wizara ya ardhi na TANROAD wawape watu ajira wafanye entry ramani ya tanzania ishibe na iwe na data sahii. Tukitoka hapo wataalm watengeze app za uelekeo (Driving direction)

Kazi waliyofaya kina Omar Salim, khatri na kadogo kama sio wafanyakazi waliloipwa kwa kazi hiyo basi wnaahitaji pongezi kubwa

Na ulivysema review ni muhimu kweli kabisa sababu nimejaribu hapa kuingiza jina la mtaa mmoja naambiwa kuna vitu nakosea. Sikosei jina la mtaa bali a kuna vitu amabvyo kwa awataalam wa barabara kwao inaweza kuwa raihisi kujua.

huu ni ujmbe nimepewa
Hi, the segment usage added is inappropriate for this road. Kindly refer this link Special roads - Map Maker Help for details on segment usage. Also, the priority 'local road' seems more appropriate. Kindly refer this link Road priorities - Map Maker Help for more information on road priorities. As of now, I will approve and change. Thanks for mapping!

Uhamiaji HQ kurasini pameanza kujengwa 2007 na 2010 wakaanza kutumia jengo lao lkn ajabu ukienda ktk satellite view pale mahali panaonyesha kiwanja tu, hii inaonyesha wkt mwingine hawana mpangilio maana kuna eneo langu la shamba kibaha kuna kibanda tu tena hakina hata mwaka lkn hili eneo limechukuliwa

Yah kwa satelite image zao haziko update mimi sana sana nazungumzia ramani za mtaaa kwa mtaa na barabara. Yaani mapsio satelite. Laini vipi satellite ya ikulu. Je ikulu wanajua hata sisi wakigoma sasa tunaijua ikulu ilivyo au tunayoona ni ikulu pia ni ya mwaka 2007 ?
 
Kuna watu wanaitwa content providers, hao ndio walitumiwa na google mwanzo kabisa katika kutengeneza maps zinazotumiwa na google... Walifanya survey kuanzia serikali kuu mpaka serikali za mitaa pamoja na kuhoji wazawa pale ilipobidi... Baada ya kupata vivid proof walifanya data input za hizo maps.... Content providers walitoka nje na wengine wa bongo walikua subcontracted! Bongo kuna "map content providers" kama InfoBridge na wengineo ila sijui kama walitumika ktk initial stages... Naamini hata UCLAS watakua wametumika!

Baada ya kuweka zile preliminary (the important features) places and locations, zinginezo tumeachiwa sisi wamiliki wa maeneo hayo ili tuzijaze BUT as you know, bado hatujaweka uzito mkuu kunako jambo hili...
 
Kwa sasa naona Mitaa mingi wameongeza majina na si kama ulivyosema ni POSTA tu. Angalia hadi Mwananyamala wameshaanza kuandika mitaa. Wataweka soon hadi 3D kwenye mitaa.

attachment.php

Dar streets.jpg
 
Mpaka sada Google wanatumia picha za satellite walizochukua huku kwetu mwaka 2006.
wana update maeneo ya ulaya tu!
 
Hata kwao wenyewe Marekani kuna vijia vya Punda vya kwenye Grand Canyon havionekani kwenye Google Map.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom