Google kuunda magari yanayojiendesha

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
... GARI BILA DEREVA: Kampuni ya Google yatangaza leo kuwa itaanza kuunda magari yanayojiendesha yenyewe na kuachana na mpango wa kuboresha yaliyopo sokoni.
=============================


140106143640_google_car_512x288_0_nocredit.jpg

Magari bila Usukani
Kampuni ya Teknologia ya Google imesema itaanza kutengeneza magari yasiyohitaji madereva .
Kampuni hiyo ambayo imejijengea sifa kwa njia ya kipekee ya utendakazi wake katika sekta ya kiteknolojia imekuwa ikikarabati magari ya kawaida.
Gari hilo la kiteknolojia halitakuwa na usukani.
140528040448_vehicleprototypephoto.jpg

Magari bila Usukani
Litakuwa linaendeshwa kwa kubofya tu.
Google imesambaza picha ya gari hilo ambalo inasema ni la kutumiwa mijini na linapaswa kuwa chambo kwa wale ambao bado hawana imani na teknolojia hii ya hali ya juu.
140528040446_vehicleprototypeimage.jpg

Gari linalojiendesha
Muasisi wa kampuni hiyo Sergey Brin alizindua gari hilo la kipekee katika mkutano na wanahabari huko California.
Brin alisema kuwa teknolojia hiyo inauwezo mkubwa wa kuimarisha maisha ya watu .
Watafiti wa magari yanayojiendesha yenyewe bado wanajadili iwapo kuwepo kwa magari hayo mabarabarani yatakuwa na upungufu wowote ikiwemo dhana kuwa itachangia ongezeko la msongamano wa magari

Chanzo:bbc
 
Back
Top Bottom