Google Kutoa Simu Zinazotafsiri Lugha Tofauti Tofauti


jamadari

jamadari

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2010
Messages
295
Likes
12
Points
0
jamadari

jamadari

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2010
295 12 0
Google Kutoa Simu Zinazotafsiri Lugha Tofauti Tofauti Simu iliyotolewa na Google awali inayojulikana kwa jina la Nexus One Monday, February 15, 2010 3:16 AM Kampuni ya Google imesema kwamba iko mbioni kutoa simu ambazo zitakuwa na uwezo wa kutafsiri lugha tofauti tofauti. Fikiria kwamba unaongea kiswahili na mchina ambaye hajui kiswahili na wewe hujui kichina hata kidogo. Jaribu kufikiria kwamba Ubuguvu mmatumbi ambaye hajui kihindi hata kidogo isipokuwa kiswahili anajaribu kuongea biashara na mhindi Bhai ambaye hajui kiswahili hata kidogo, hapo tatizo la mawasiliano lazima litajiweka wazi, lakini kwa kutumia simu za Google ambazo zinatarajiwa kutolewa hivi karibuni lugha yoyote utakayoongea itatafsiriwa wakati huo huo na hivyo tatizo la lugha litakuwa limewekwa pembeni. Kampuni ya teknolojia ya Google inatarajia kutoa simu zinazotafsiri lugha zaidi ya 6000 zinazozungumzwa duniani ili kuwawezesha watu wanaozungumza lugha tofauti kuelewana. Google ambao awali walijiingiza kwenye biashara za simu kwa kutoa simu zao zinazoitwa Nexus One, tayari wanatamba na programu yao waliyoitoa ambayo inatafsiri maandishi katika lugha tofauti tofauti. Wiki iliyopita lugha ya Haiti "Creole" iliongezwa katika programu hiyo na hivyo kuzifanya lugha ambazo zinawezwa kutafsiriwa maandishi yake na programu ya Google kufikia 52. Hadi sasa Google imeishawawezesha watumiaji wa simu kutumia mfumo wa kutambua sauti kusachi vitu kwenye google kwa kuvitamka badala ya kuviandika. Google itaziunganisha teknolojia zake hizo mbili ili kuweza kutoa simu zitakazokuwa zinafanya kazi kama mkalimani. Kama ilivyo kwa watu wanaofanya kazi ya ukalimani, Simu hizo pia zitakuwa zikisiliza sentensi nzima mtu anayoongea ili kuelewa kinachosemwa kabla ya kuanza kuitafsiri. Mkuu wa huduma ya ukalimani ya Google, Franz Och, amesema kuwa wanachohangaikia kwa sasa ni kuuongeza usahihi wa kutambua sauti na kuweza kutafsiri kwa usahihi. Simu hizo mpya za Google zinatarajiwa kuingia madukani ndani ya miaka michache ijayo. http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=4077722&&Cat=2
 
Chamoto

Chamoto

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2007
Messages
2,563
Likes
1,827
Points
280
Chamoto

Chamoto

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2007
2,563 1,827 280
Hawa jamaa bwana kweli ni non stoppable na hii ndiyo andvantage ya kuwapa vijana maamuzi kuliko kuwa na chain of command yenye bureaucracy kama makampuni mengine
 
drphone

drphone

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2009
Messages
3,561
Likes
93
Points
145
drphone

drphone

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2009
3,561 93 145
hii imetulia jamani taaluma inazidi kukua mimi nilikuwa natafuta software ya kuprint maneno ninayotamka yenyewe iniprintie je nitapata
 
K

Kosmio

Senior Member
Joined
Apr 28, 2009
Messages
128
Likes
2
Points
35
K

Kosmio

Senior Member
Joined Apr 28, 2009
128 2 35
Google kiboko. Je, mnyakyusa akimpigia simu mjerumani wataelewana?
 
Raia Fulani

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Messages
10,217
Likes
109
Points
145
Raia Fulani

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2009
10,217 109 145
hizo lugha 52 kiswahili kimo?
 
V

Vumilia matola

Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
12
Likes
0
Points
0
V

Vumilia matola

Member
Joined Aug 18, 2009
12 0 0
Je? Mnatakawa wote muwe mnatumia simu za goolge? Mfano me nina google mwengine anatumia nokia inawezekana?
 

Forum statistics

Threads 1,237,666
Members 475,675
Posts 29,296,673