Google Kutoa Simu Zinazotafsiri Lugha Tofauti Tofauti

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Kampuni ya Google imesema kwamba iko mbioni kutoa simu ambazo zitakuwa na uwezo wa kutafsiri lugha tofauti tofauti. Fikiria kwamba unaongea kiswahili na mchina ambaye hajui kiswahili na wewe hujui kichina hata kidogo.
Jaribu kufikiria kwamba Ubuguvu mmatumbi ambaye hajui kihindi hata kidogo isipokuwa kiswahili anajaribu kuongea biashara na mhindi Bhai ambaye hajui kiswahili hata kidogo, hapo tatizo la mawasiliano lazima litajiweka wazi, lakini kwa kutumia simu za Google ambazo zinatarajiwa kutolewa hivi karibuni lugha yoyote utakayoongea itatafsiriwa wakati huo huo na hivyo tatizo la lugha litakuwa limewekwa pembeni.

Kampuni ya teknolojia ya Google inatarajia kutoa simu zinazotafsiri lugha zaidi ya 6000 zinazozungumzwa duniani ili kuwawezesha watu wanaozungumza lugha tofauti kuelewana.

Google ambao awali walijiingiza kwenye biashara za simu kwa kutoa simu zao zinazoitwa Nexus One, tayari wanatamba na programu yao waliyoitoa ambayo inatafsiri maandishi katika lugha tofauti tofauti.

Wiki iliyopita lugha ya Haiti "Creole" iliongezwa katika programu hiyo na hivyo kuzifanya lugha ambazo zinawezwa kutafsiriwa maandishi yake na programu ya Google kufikia 52.

Hadi sasa Google imeishawawezesha watumiaji wa simu kutumia mfumo wa kutambua sauti kusachi vitu kwenye google kwa kuvitamka badala ya kuviandika.

Google itaziunganisha teknolojia zake hizo mbili ili kuweza kutoa simu zitakazokuwa zinafanya kazi kama mkalimani.

Kama ilivyo kwa watu wanaofanya kazi ya ukalimani, Simu hizo pia zitakuwa zikisiliza sentensi nzima mtu anayoongea ili kuelewa kinachosemwa kabla ya kuanza kuitafsiri.

Mkuu wa huduma ya ukalimani ya Google, Franz Och, amesema kuwa wanachohangaikia kwa sasa ni kuuongeza usahihi wa kutambua sauti na kuweza kutafsiri kwa usahihi.

Simu hizo mpya za Google zinatarajiwa kuingia madukani ndani ya miaka michache ijayo.
 
jamani hii ni hatua nzuri mambo yanazidi kurahisishwa tecknolojia inazidi kukua
mimi natafuta software ambayo inaweza kuprint kile ninachoongea
 
Back
Top Bottom