Google Chrome na Mozilla Zimeifungia ‘KickAss Torrents’ Kama Mtandao Wa Udanganyifu

the great wizard

JF-Expert Member
Dec 21, 2015
1,482
882
Kama ulizoea kupakua mafaili yako tofauti tofauti kutoka katika mtandao huo kupitia katika browser za Google Chrome na Mozila Firefox kwa sasa mbinu zako zitagonga mwamba.
Mtandao huo umefutwa na Mozila pamoja na Chrome kiasi cha kwamba ukijaribu kuingia utapata ujumbe ambao unakwambia huwezi ingia katika mtandao huo.

Kuzuiwa huku ni kwa http://kat.cr na matokeo yote ya Google Search ya https://kat.cr kwa pamoja. Usiku wa jana nilikua na mpango wa kushusha mafaili kadhaa toka katika mtandao huo lakini kila nikiingia ilikuwa inanikatalia. Nipo hapo nilipofanya kautafiti kangu na kunadika makala hii.
chromekatdecept.png

Ili kuweza kuupata mtandao huo tena inakubidi kubadilisha kivinjari, yaani usitumie Chrome wala Firefox. Kwa mfano mimi baada ya hali ile kutokea nilifanikiwa kuingia katika mtandao kwa kutumia Kivinjari cha Edge kutoka Microsoft.

Kingine cha muhimu ni kwamba usiutafute mtandao huo kwa kutumia Google hata kama ukiwa unatumia kivinjari ambacho sio Firefox au Chrome kwani kuna hati hati mtandao huo ukagoma kufunguka pia.

Kwa hili mimi niliingia kwa kupitia kivinjari cha Edge na kisha nikaenda kwenye mtandao maarufu wa utafutaji wa Bing (ambao una nguvu kama google vile). Baada ya kufika hapo nikautafuta mtandao na nikaingi kilaini kabisa. Inavyosemekana muda huu ambao unasoma makala hii naweza nikawa napitia mafaili yangu niliyoyashusha kupita KickAss Torrent (KAT)
katffforg.png

Makampuni yote mawili ambayo yanamiliki vivinjari hivi yamejitetea kuwa yamefanya hivyo kwa makusudi kabisa na lengo lao kuu ni kuhakikisha wanalinda usalama wa watumiaji wao.

Kumbuka lakini hii sio mara ya kwanza kwa mtandao huu – au kama hii – kupatwa na majanga ya kufungiwa au kutopatikana kwa baadhi ya maeneo au vifaa.

Mitandao hii pia inapigwa vita sana na watu kwani watu wanapata vitu vingi sana kinyemela kwa kutumia hii mitandao. Vitu ambavyo kwa hali ya kawaida ilibidi wavilipie ili wavipate
[Maendelea mapya: Tayari team ya KickAss imesema imerekebisha mapungufu ya kiufundi na usalama yaliyosababisha kufungiwa kwao na tayari wanawasiliana na Google na Mozilla ili kuondolewa kwenye orodha ya mitandao isiyo salama. Hili lilishawahi tokea kabla miaka ya nyuma na wakarekebisha na kuachiwa. Inaweza chukua masaa hadi siku kadhaa.]
 
Hiyo site ukiingia bila AdBlocker ni majanga hasa kwenye Android.
ni kweli mkuu na sidhani kama chrome/firefox wameifungia hio site bali ni security za hizo browser zimedaka matangazo ambayo yanadhuru computer hasa yale ya flash.
 
nimetumia uc browser cheki inavyo niandikia
upload_2016-4-14_18-20-47.png
 

Attachments

  • upload_2016-4-14_18-20-47.png
    upload_2016-4-14_18-20-47.png
    26.2 KB · Views: 98
  • upload_2016-4-14_18-20-47.png
    upload_2016-4-14_18-20-47.png
    26.2 KB · Views: 75
Sasa kama hiyo iligoma si ungetafuta unachotaka katika website ya pirate bay
 
Haya mambo nakumbuka yalisha wahi kuutokea mtandao wa pirate bay pia iliwalazimu wabadili domain na kuuita thepiratebay ili kufanikiwa kurudi hewani. Labda wajukuu wangu mnambie nini haswaa madhara ya mitandao hii ya torrents??
 
Back
Top Bottom