GOOD NEWS: Ni Emmanuel OKWI ndani ya YANGA, asaini Miaka Miwili.

Aleyn

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
19,041
32,037
Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa kutoka nhcini Uganda
Emmanuel Arnold Okwi ambaye alikua akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.

Yanga SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki wengi kwa mkataba wa miaka miwili na
nusu ambapo kwa sasa ataitumika klabu yake mpya ya watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa
msimu wa 2015/2016.

Dirisha dogo la usajili nchini Tanzania limefungwa leo usiku Disemba 15, 2013 saa 6 usiku ambapo
mabingwa wa kihistoria klabu ya Yanga wamekalilisha taratibu zote za usajili ikiwa ni pamoja na kupata hati
ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.

Usajili wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji watano wa kimataifa
wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.

Uongozi wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki
kuwapa ushirikiano wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.

Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni katika kuimarisha kikosi cha Yanga ni mlinda mlango Juma
Kaseja ambaye alikuwa mchezaji huru na Hassan Dilunga aliyesajiliwa kutoka timu ya Ruvu Shooting.

Baraka Kizuguto Afisa Habari – Young Africans SC
Disemba 15, 2013.
 
Mbona kama siwaelewi cos simba bado wanadai pesa yao hawa yanga hawajitaki wanataka kunyang'anywa point haya ngoja tuone africa sio tanzania cos wamezoea kupindisha sheria tff kama walivyofanya kwa twite,yondan na ngasa ngoja tuone inakuwaje na kama wakifanikiwa basi kuna tatizo tena kubwa la kiufundi simba maybe hawajui sheria au wanapotoshwa
 
Yanga wamefanikiwa rasmi kupata saini ya emmanuel okwi kutoka sc villa ya uganda..
Source ni mimi mwenyewe.
 
Hii habari si nzuri hata kidogo kwa wale ndugu zetu wa pale karibu na roundabout ya kariakoo, tena itawakondesha baadhi ya watu.
 
Hongereni yanga kwa kupata sahihi ya okwi sisi tupo na vifaa kama Mwagane yeya.
mbeya city tupeni raha ngwe ya mwisho.
 
Last edited by a moderator:
Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa kutoka nhcini Uganda
Emmanuel Arnold Okwi ambaye alikua akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.

Yanga SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki wengi kwa mkataba wa miaka miwili na
nusu ambapo kwa sasa ataitumika klabu yake mpya ya watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa
msimu wa 2015/2016.

Dirisha dogo la usajili nchini Tanzania limefungwa leo usiku Disemba 15, 2013 saa 6 usiku ambapo
mabingwa wa kihistoria klabu ya Yanga wamekalilisha taratibu zote za usajili ikiwa ni pamoja na kupata hati
ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.

Usajili wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji watano wa kimataifa
wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.

Uongozi wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki
kuwapa ushirikiano wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.

Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni katika kuimarisha kikosi cha Yanga ni mlinda mlango Juma
Kaseja ambaye alikuwa mchezaji huru na Hassan Dilunga aliyesajiliwa kutoka timu ya Ruvu Shooting.

Baraka Kizuguto Afisa Habari – Young Africans SC
Disemba 15, 2013.

kweli??????maana saa hizi ni 4 kasoro usiku
 
Mbona kama siwaelewi cos simba bado wanadai pesa yao hawa yanga hawajitaki wanataka kunyang'anywa point haya ngoja tuone africa sio tanzania cos wamezoea kupindisha sheria tff kama walivyofanya kwa twite,yondan na ngasa ngoja tuone inakuwaje na kama wakifanikiwa basi kuna tatizo tena kubwa la kiufundi simba maybe hawajui sheria au wanapotoshwa

Yanga imejipanga na watu makini..hawakurupuki kama wanasiasa wa Simba..
 
Mbona kama siwaelewi cos simba bado wanadai pesa yao hawa yanga hawajitaki wanataka kunyang'anywa point haya ngoja tuone africa sio tanzania cos wamezoea kupindisha sheria tff kama walivyofanya kwa twite,yondan na ngasa ngoja tuone inakuwaje na kama wakifanikiwa basi kuna tatizo tena kubwa la kiufundi simba maybe hawajui sheria au wanapotoshwa
FIFA ilimruhusu Okwi kucheza SC Villa,Yanga wamemnunua Okwi kutoka SC Villa.Tunasema kila siku kamati ya usajili/Ufundi ya Simba kuna matatizo makubwa,jiulize kwa nini kila msimu wanafanya makosa
 
Mbona kama siwaelewi cos simba bado wanadai pesa yao hawa yanga hawajitaki wanataka kunyang'anywa point haya ngoja tuone africa sio tanzania cos wamezoea kupindisha sheria tff kama walivyofanya kwa twite,yondan na ngasa ngoja tuone inakuwaje na kama wakifanikiwa basi kuna tatizo tena kubwa la kiufundi simba maybe hawajui sheria au wanapotoshwa

wewe unaamini maneno ya viongozi wa simba?,pesa ilishaingia mifukoni mwao siku nyingi.Karibu yanga kwa mkopo kama ni mwanasimba hutakua wa kwanza bubu alishawafungulia njia mkuu.
 
Habari hii itakurahisishieni ile mission yenu ya kumtoa mwenyekiti wenu hamna haja tena ya kwenda bungeni.

Mkuu hapa ni full mchanganyiko; kuna mawili, inawezekana Sports Club Villa wameamua kuwa wajanja wajanja au Simba walilipwa hela na hawakutaka kuiweka kwenye account ya Club, lakini kama la pili ni kweli inakuwaje hadi uongozi wa TFF ukiongozwa na Kawemba waseme kwamba ni kweli Simba haijalipwa. Rage na watu wake wana maswali mengi ya kujibu.

Hii habari ni kutoka mwanaspoti na link yake hii hapa. Yanga yapewa masharti kumsajili Okwi - Soka - mwanaspoti.co.tz

YANGA na Azam kama zinamtaka straika wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ni fedha yao tu, lakini kuna sharti lazima walifanye.

Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) limetoa masharti na muongozo wa klabu zinazomtamani mchezaji huyo aliyesitisha mkataba na Etoile du Sahel ya Tunisia.

Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba aliiambia Mwanaspoti kuwa: "Hakuna kinachoizuia klabu kutaka kumsajili Okwi, cha muhimu wanatakiwa kuongea na Etoile du Sahel ya Tunisia, wakimalizana nao basi watamchukua, hivyo ni ruksa cha muhimu ni kufuata sheria na haki."

Okwi ameidhinishwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuichezea SC Villa ya Uganda kwa muda wa miezi sita huku sakata lake la Etoile likifanyiwa ufumbuzi.

Mchezaji huyo anaidai Etoile malimbikizo ya mishahara pamoja na dau lake la usajili huku Simba iliyomuuza kwa Waarabu hao nayo ikidai dau lake Sh 480 milioni.

Suala hilo lipo Fifa na Kawemba amewahakikishia Simba kwamba wasiwe na wasiwasi watapata haki yao.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom