Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa kutoka nhcini Uganda
Emmanuel Arnold Okwi ambaye alikua akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.
Yanga SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki wengi kwa mkataba wa miaka miwili na
nusu ambapo kwa sasa ataitumika klabu yake mpya ya watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa
msimu wa 2015/2016.
Dirisha dogo la usajili nchini Tanzania limefungwa leo usiku Disemba 15, 2013 saa 6 usiku ambapo
mabingwa wa kihistoria klabu ya Yanga wamekalilisha taratibu zote za usajili ikiwa ni pamoja na kupata hati
ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.
Usajili wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji watano wa kimataifa
wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.
Uongozi wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki
kuwapa ushirikiano wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.
Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni katika kuimarisha kikosi cha Yanga ni mlinda mlango Juma
Kaseja ambaye alikuwa mchezaji huru na Hassan Dilunga aliyesajiliwa kutoka timu ya Ruvu Shooting.
Baraka Kizuguto Afisa Habari – Young Africans SC
Disemba 15, 2013.