Good News: Mawaziri Kutoka Tanzania na Rwanda Wakutana Kuhusu Ujenzi Wa SGR, Dar Es Salaam

Itzmusacmb

JF-Expert Member
Jun 22, 2016
1,531
1,132
Leo January 20, 2018 Siku chache zilizopita Rais Kagame wa Rwanda alifanya ziara ya kikazi nchini na kuzungumza na President JPM juu ya ujenzi wa reli ya umeme, sasa GOOD NEWS ni kwamba Mawaziri watatu wa Tanzania na mmoja kutoka nchini Rwanda wamesaini mikataba ya awali kuhusu ujenzi wa reli ya umeme kutoka Isaka Tanzania mpaka Kigali nchini Rwanda.

ac0b4f5ebdffc8609994bf2c073fa35f.jpg


Akizungumza na Waandishi wa Habari, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema makubaliano hayo yanatokana na maagizo yaliyotolewa na Rais John Magufuli na Paul Kagame wa Rwanda baada ya kukutana January 14, 2018.

“Treni itakayopita katika reli hiyo itakuwa ni ya umeme, ambapo itakuwa kwa treni ya abiria itatembea speed ya Kilometre 160 kwa saa na treni ya mizigo itakuwa na speed ya Kilometre 120 kwa saa,”.– Prof. Mbarawa

Prof. Mbarawa amesema kutokana na ujenzi wa reli nyingine hasa ya kati itarahisisha usafiri ambapo kutoka Dar es Salaam hadi Rwanda inaweza ikachukua saa 12 badala ya siku 2

Uhuru Na Umoja
 
au unaeza ukawa uko ndani ya treni unakunywa kahawa ukashangaa umerushiwa fuko la mavi kupitia dirishani (flyn toilets). Kenya is not safe for our modern expensive bullet trains esp Nairobi.
Hahaha kule hakufai kabisa
 
au unaeza ukawa uko ndani ya treni unakunywa kahawa ukashangaa umerushiwa fuko la mavi kupitia dirishani (flyn toilets). Kenya is not safe for our modern expensive bullet trains esp Nairobi.
Hahahahhaha , sasa Si bola fuko La kinyesi mkuu!! Unashangaa Al shabaab wameteka Treni yote
 
Back
Top Bottom