chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,388
- 24,947
Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, alisema kuwa amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo hicho.
Golugwa amesema Jumamosi alikuwa naye Dodoma na akapiga naye picha, lakini alimuahidi leo amfuate Moshi ampe rambirami ya wafiwa wa ajali ya shule ya Luky Vicent,lakini jana alimpigiasimu akaomba akachukue rambirambi hiyo leo na akamtuma Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro na aliingia ofisini wakati anasaini cheki akasikia vibaya na kukimbizwa hospitali ya Rufaa KCMC.
Golugwa amesema wakati akisaini cheki hiyo ya Sh.milioni 3.5 alikuwa na Mstahiki Meya wa Jiji laArusha, Calist Lazaro ambaye ilikuwa akabidhiwecheki hiyo ili ailete kwa wafiwa Arusha.
Amesema ngumu kuamini kifo kimetokea ghafla , maana kakimbizwa hospitali KCMC na kuambiwa amefariki, sasa wanasubiriwa watoto wake ili kuufanyia uchunguzi mwili wake,kutokana na mazingira ya kifo kilivyotokea.
Amesema baada ya hapo Chama kitatoa taarifa rasmi ya kuondokewa na mkongwe huyo katika chama,baada ya kuwasiliana na wanafamiliya na wengine.
Golugwa amesema wakati hali hiyo ilipomkuta katika ofisi yake ya Keys Hotel, alikimbizwa hospitalini na dereva wake, mtoto wake mmoja na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro.
Chanzo : EATV