Suluhisho rahisi kwa wanaodhani wamepungukiwa nguvu, wanaosumbuka kurudia tendo au kuwahi kufika

Tized

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
4,025
5,955
Salaam sana Wakuu

Inavyoonekana siku hizi japo kweli kuna tatizo la upungufu wa nguvu za kiume haswa kwa mazingira ya mijini, Lakini hili tatizo linaonekana kukuzwa kuliko lilivyo hadi imepelekea woga mkubwa kwa baadhi ya wengi wetu.

Ndipo kwenye tafakari yangu nikaona NIANZISHE HUU UZI kwa machache tu kwa ufahamu mchache nilio nao, Ili NIWAALIKE wengi WENU kwa msaada zaidi wa mawazo kwa ndugu zetu wanaokutana na mfadhaiko huu. Nikiamini pia wengi wenu mna utaalamu na mnaoweza kuchambua haya makitu kwa ufanisi zaidi mkatatusaidia sana kwenye uzi huu. Yafaa sasa tujikite kwenye ufumbuzi kuliko kuripoti tatizo na kulaumu. Kadiri tunavyoendekeza kuripoti tatizo tunawaathiri hata wale waliokuwa wazima ambao kwa kuwa hakuna kipimo sawia kujua kipi ni kipi, nao wasiwasi unawafanya wanapoteza ujasiri wao na kujiona wana tatizo kumbe wapo imara sana kuliko mkuki.

Kwa kuanzia yafuatayo yaweza kusaidia kuboresha kulifurahia tendo la ndoa zaidi na kwa muda zaidi.

Kuuweka Mwili vizuri: Ni wazi kuwa tendo hili linachagiwa sana na mzunguko mzuri wa damu. Mwili ukiwa kwenye hali nzuri kiafya na tendo huwa linaenda ipasavyo. Na mwili ukiwa dhoofu basi tegemea tukio dhoofu pia. Hivyo ukitaka kuwa na matokeo mazuri kwenye ndoa yako, jitahidi sana kujiweka vizuri kwa kula sahihi na kufanya mazoezi mepesi mepesi tu kwa wale wanaoweza kuutumia muda vizuri wapiti pite Gym walau siku mbili na kuendelea kwa wiki.

Kufahamu kuwa kupumzika kwa uume baada ya baada kufika mara ya kwanza sio tatizo. Kwa wanaume walio wengi, baada ya mshindo wa kwanza hupumzika kidogo kabla ya kuendelea na awamu nyingine. Japo kuna ambao wana uwezo wa kuendelea moja kwa moja bila kupumzika (law ya use and misuse inahusika kwa wengine apa). Kwa hio kusinyaa kwa uume baada ya mshindo wa kwanza, isifahamike kuwa ni upungufu wa nguvu bali ni ajdustiment ya mwili wenyewe kutokana na kwamba mwanaume kabla ya tendo mapigo ya moyo huongezeka na huchangia damu kwenda kwa kasi, na kwa hali hio anakua yupo juu sana kimhemko, inapofikia anamaliza raundi ya kwanza mwili unakua unapoa /umesharudi kwenye hali yake ya kawaida, ndiko kunakosababisha hio maneno kusinyaa kwa wengi wakati mapigo ya moyo yanaporudi kawaida (MWILI KUPOA).

Maandalizi ya mwili. Wanaume tupo tayari muda wote… ila linapokua swala ya mwenza wako (kwa kuwa muda unaotumia kwa maandalizi na tendo una uhusiano wa moja kwa moja na satisfaction ya mwenzio)… unahitaji muda angalao nusu saa na kuzidi kujiandaa na mwenzi wako. Kama timu ya mpira inapoenda ugenini huhitaji muda kuzoea mazingira, ndio na mwanaume anavyohitaji muda kuzoea mazingira ya ugenini. Hili linakusaidia sana mwanaume kutoka kwenye mihemko na kurudi kwenye hali yako ya kawaida ambayo itakusaidia kuwa na muda mzuri zaidi wa kufurahia tendo. Jitahidi pia kuvuta pumzi nyingi ndani na uiachie polepole kukusaidia kukuweka kwenye utulivu mzuri.

Timing ya kuanza tendo: Kwa kuwa tendo linahusisha sana hisia za mwili, ukiwa umetumia muda unaotosha kuandaana, basi usiwe na papara mwanzoni, bali uwe na utulivu, pia jitahidi kuzungumza moja mawili wakati unaanza kuzoea mazingira mengine (core business) EPUKA UHARAKA na kuweka sana akili yako hapo, jinafikie mwenyewe kuwa its just a normal thing (mental pride)

Concetration/ Umakini uliopitiliza… Unapaswa kumfanya mkeo aweke akili yake yote hapo, na wewe unatakiwa katika kumuweka mkeo kwenye concentration uuharibu umakini wako (level of concentration). Ukiweka concentration ya juu sana kwenye tendo… haikuchukui dakika mbili umemaliza, na kuirudisha tena ile hali ya concentration uliokua nayo mwanzo itakuwia ngumu sana….. Usiweke sana akili yako hapo kama unataka kufurahia kwa muda zaidi. ila kama hutaki kudumu.. weka akili na umahini wako hapo woote.. just seconds or a minute you are done

MAZOEZI ya mwili ni muhimu sana sana sana sana sana kwetu wanaume. Kama huna muda wa kwenda jimu walau ukiamka piga ‘PUSH-UPS walau 50'' kila siku na ''SQUARTS'' . haya ni mazoezi mepesi lakini ni BORA zaidi kwa mwanaume. Kwetu sisi wanaume tunatumia sana misuli yetu wakati huu, kwa hio kuna ulazima wa kutafuta ustahimilivu wa misuli ''mussle strength n perseverance''. Hio kitu ni starehe na unatakiwa baada ya tendo uwe umekuwa refreshed na sio uwe unaumwa kila mahali na sijui joints zinauma sijui nini nini? ukijiona unakuwa hivyo baada ya tendo ujue mwili wako haujakaa fiti ipasavyo kimazoezi/kiafya

Pia Afya ya Akili inahusika sana, Japo inahitaji jitihada makhususi... lakini kila mtu ana uwezo wa kuchagua nini cha kufikiria na nini si cha fikiria(kupuuzia) na pia akienda hatua zaidi anaweza kupuuza kila kitu kwa wakati fulani kama unajua una huo uwezo na ukaamua kuutumia. Pia kuchagua kufikiri yale yaliopo kwenye uwezo na urefu wa kamba yako pekee; vitu usivyo na uwezo navyo utajisumbua tu bure na kujipa stress zaidi. Weka nguvu na jitihada zako kwenye kutafuta ufumbuzi wa changamoto zako, jifunze na acha kufikiria matatizo kwa maana hakubadilishi kitu na yataendelea kuwa hivyo n.k n.k................ Ukiwa na namna nzuri ya kuyachanganua mambo yako utasaidika sana kwenye afya ya akili yako na kuwa vizuri zaidi

Karibuni wadau kusaidia utatuzi wa hili jinamizi linalojizolea umaarufu kadiri siku zinavyokwenda kwenye jamii yetu.

Copy kwa msaada zaidi wa mawazo na uzoefu... BAK, watu8, utafiti, Mndengereko, Mr Rocky, Ntuzu, kabanga, OLESAIDIMU, Matola, Mtoto halali na hela, Excel, The Boss, Mtambuzi, sungura1980, Mentor, kiwatengu, Annael, Candid Scope, Kaizer, mwekundu, KakaKiiza, Freeland, Mapi, Sibonike, muuza ubuyu, Eli79, mzabzab, CYBERTEQ, na wengine wote ambao sijaweza kuwataja apa

Tz

Thanks Bro watu8
1. Kuwa makini na baadhi ya aina ya vyakula...
Chakula humfanya mwanadamu aendelee kuishi kwani hubeba nishati na virutubisho vya madini vyenye kupelekea uboreshaji wa afya ya mwili.

Wataalamu wa masuala ya ngono na vichocheo mwilini hupendekeza aina fulani fulani za vyakula ambavyo kama mwanaume akipendelea kula basi huongeza 'libido'.

Baadhi ya vyakula hivi ni kama komamanga, parachichi, mvinyo mwekundu, chaza na pweza, tikiti maji na mbegu zake, chokoleti, pilipili, tangawizi n.k

2. Kukosekana kwa lugha ya aina moja ya kimapenzi baina ya mume na mke...
Miili huwa inaongea haswa linapokuja suala la ngono baina ya mwanaume na mwanamke...
Si watu wote wenye uwezo wa kutafsiri lugha hii ingawaje kila mmoja wetu amejaaliwa kuwa na uwezo wa kutambua.
Kwa wanaume walio na uzoefu wa kutongoza kwa ishara ni wepesi sana kuwaridhisha wanawake kuliko wale wanaume wenye kutumia vitendo zaidi.
Kwa kawaida tongozo huwa halina ukomo haijalishi wewe ni mume au mke (yes namaanisha mwanaume aliyeoa au mwanamke aliyeolewa), ngono nzuri ni ile ambayo matokeo yake ni hutokana na mume au mke kumtongoza mwenzake.

3. Mazingira ya eneo la mpambano na usafi wa mwanamke...
Mazingira ya utulivu na usafi maridhawa ni jawabu tosha la matokeo ya ngono nzuri yenye utulivu pia.
Mwanaume huwezi kuwa na mawazo straight ya kingono katika mazingira ambayo bado unajiona ni stranger hata kama ni nyumbani kwako, mathalani unahofia jirani atakuja kugonga kuomba chumvi n.k

Pia usafi na matunzo ya mwili wa mwanamke kwa kiasi kikubwa huamasisha au hufifisha matamanio ya kingono.

everlenk, Asante sana kwa coment yako yenye msaada sana. Umeongea kitu cha msingi sana..Thanks; You have nailed it.
Kila asomaye na afahamu!!!!
Haya ngoja nichangie kidogo,ila mambo mengi karibu yote mkuu Tized na watu8 wamemaliza.

Kuna jambo dogo sana lakini wengi wanalipuuzia na linawaathiri wanaume wengi bila kujua nalo ni maneno ya vijiweni,kumekuwa na maneno mengi kwamba mwanaume aliyekamilika lazima aende sijui raundi 3 na kuendelea,mara aliyekamilika lazima awe na inch 6,mara sijui style hii mwanaume akifanya lazima mwanamke akuheshimu.

Sasa basi mwanaume anapokutana na mwanamke kimwili anakuwa na matarajio meng kichwani pake kutokana na yale maneno ya vijiweni alosikia anaposhindwa kutimiliza hayo huanza kujiona yeye hafai au labda ana tatizo,hofu hujengeka moyoni mwake tayar hapo ndo mwanzo wa tatizo,hana ujasiri anapokutana na mpenzi wake unakuta hata mshindo mmoja tu inakuwa tabu sana.

La muhimu kila mmoja ajielewe ana uwezo gani,wote hatujaumbwa kulingana,kama wewe uwezo wako ni kimoja kisha ndo upite muda ndo uendelee kubali hali yako boresha hiyo hali yako na mtu wako naye afurahi,yaweza kuwa single but heavy,kama wewe sijui inch 4 jikubali ulivyo boresha hali yako utaona mambo ni mazuri,jua style unazozimudu usisikie maneno ya mtaani,wote hatulingani kuna anayekimbia mita 100,200,400 na wengine marathon lakini siye wote ni wanariadha,kila mmoja aridhike na uumbaji aliopewa aboreshe mazingira yake atafurahia maisha.

Lingine la mwisho naona hapa mmekazia swala la usafi kwa mwanamke ni kweli kabisa ke anahusika sana,ila hata nyie baadhi yenu me ni wavivu sana kuoga,unakuta mwanaume katoka kwenye shughuli zake za mchana kutwa anafikia kukutana na mwanamke hata haogi moja kwa moja kwenye makamuzi,mwili hujapata hata refreshment hapo game likiwa mbaya anajiona mpungufu kumbe tu hajaruhusu mwili nao upate ahueni.

Brother Mtambuzi anatupa utambuzi wake apa:-
Tized ukweli ni kwamba nilishawahi kuweka uzi hapa kuzungumzia jambo hilo wakati fulani.
Mtindo wa maisha tunayoishi, vyakula tunavyokula, kujipweteka bila kufanya mazoezi kuiga mikanda ya porn wakati yale ni maigizo tu, na kutumia madawa makali ya hospitali bila kuwa muangalifu. nina maana kwamba Tusiwaamini sana wataalamu wetu wa afya kwani sekta ya afya imevamiwa na wafanyabiashara ambao kwao wanachojali ni fedha kwa hiyo kuandikiwa madawa makali bila kujali afya ya mtumiaji ni jambo la kawaida. Madawa makali yana mchango mkubwa katika kuathiri afya zetu na huwezi kufanya tendo kwa ufanisi kama afya yako ina mgogoro.

Binafsi nachagua vyakula, nafanya mazoezi ya kawaida, ya kutembea kilomita tano kila siku za kazi, natumia tiba mbadala, yaani isiyohusisha madawa ya hospitali na kama nitalazimika kutumia madawa ya hospitali, basi nitahakikisha nimefanya udadisi kwa wataalamu Zaidi ya wawili ili kuwa na uhakika sitaudhuru mwili wangu, SICHEPUKI, lakini pia tendo la ndoa mimi na mama ngina tunalifanya kama sehemu ya burudani na siyo la upande mmoja............
Asprin hujaalikwa pitia mbali hii maneno............
Dr Asprin, Zogwale, EMT, Tuko, Molembe, Jodoki Kalimilo, tpaul, na dada yangu Karucee, King'asti, Jawilat, Chujio KOKUTONA, First Lady, Kaunga, Ablessed, amu, black woman, Khantwe, Preta na wengineo wooote popote mlipo hekima zenu zinahitajita tafadhali

Mkuu BAK nimecheka sana aisee.. ila umeongezea kitu cha msingi sana Mkuu. Thanks
Mie naomba nisisitizie kula vizuri, kufanya mazoezi, usafi wa mwanaume na kujiepusha na uvutaji sigara na ulevi wa kupindukia. Kama walivyozungumzia wachangiaji wengine kula vizuri na mazoezi ni muhimu sana katika kuboresha tendo la ndoa. Usafi wa mwanaume nao ni muhimu sana sio unaacha vuzi limekaa miaka chungu nzima hata kuweza kulisuka rasta. Kuoga na usafi wa kinywa ni mgogoro, hivi havifanywi mpaka siku ya sikukuu. Ulevi wa kupindukia na uvutaji wa sigara ni adui mkubwa wa nguvu za kiume na wanaume wengi sijui kama wanalijua hili na kwa kutaka waonekane na wao ni wa MUJINI huvuta sigara pakiti hata moja kwa siku au zaidi na kilevi cha kutosha bila kujua hii life style inawapunguzia kwa kiasi kikubwa na kasi ya kutisha nguvu zao za kiume.

Mkuu Freeland anasema:-
Uangaliaji wa pornography pia una madhara makubwa katika performance ya mwanaume on bed....mara nyingi inaathiri saikolojia ya kujiona,kwamba maumbile yako hayatoshi....au kudhani,na kuiga performance ya kwenye pono ndio uhalisia.....mazoezi...vyakula...maandalizi na,mengine mengi ...kiufupi matatizo ya nguvu za kiume asilimia kubwa ni ya kisaikolojia

Mkuu 1st AID anachambua kiutalamu khs wale wanaume wanaotumika sana:-
Mkuu Tized nikushukuru kwa kuendelea kuufanya uzi huu maridhawa kuwa hai, ni jambo zuri hasa ukiangalia unyeti wake.

Umetaka kujua nini athari za kufikia mshindo kwa mara nyingi, hasa tukilenga wale wenzetu ambao wamekua na mahusiano yasiyo rasmi kwa idadi ya KE na kwa idadi kubwa ya magoli.
Kwanza niseme manii kwa kiasi kikubwa ni maji na kuna protien kidogo na madini ya zinc pamoja na magnesium.

Inaelezwa na watafiti kwamba kila mshindo 1 hupoteza mg 5 za ZMA (zinc+magnesium), ZMA huengeza homoni ya testosterone ambayo hutusaidia katika kupata usingizi mzuri na kuzuia Metabolic Syndrome and heart disease. Hapa kama nilivyo sema awali nimewalenga watu ambao hutupia nyavu tatu ndani ya masaa yasiyo pungua 24.

Somo hili ni pana na zuri nini kifanyike walau wasije kumbwa na madhara tunarudi kwenye aina ya vyakula kuna ulaji wa mihogo mibichi karanga mbichi na asali mbichi katika hivi tunacho jaribu kuongeza ni ZMA pia kuna shellfish kama oyster au pweza ambao huongeza sana ZMA na kuchochea msukumo wa damu. Tukizingatia hili na mengine mengi yaliyo semwa basi tutaongeza ufanisi. Tukumbuke kila kitu ni kwa kipimo sahihi ndio tunapata ubora wa kilichokusudiwa.
Execessive than required is illegal.

Ushauri wangu tusome vitabu na tutumie utandawazi kuongeza maarifa.

Kumbe kuwahi nako ni dili wakati mwingine!! kuchelewa nayo ni sheeedaaaa!!! Msome Mkuu EMT apa
Kuwahi (au kuchelewa) kufika
Nilishaandika kwenye threads nyingine kuwa kuwahi kufika inaweza kuwa na faida zaidi kuliko kuchelewa kufika. Kwa nini? Kwa sababu mwanaume anaweza kuji-control na hivyo kutofika mapema lakini ni vigumu kujilazimisha kufika mapema. Of course, kuwahi au kuchelewa kufika kuna faida na hasara zake kulingana na wahusika, madhumuni ya kungonoka, nk.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa baadhi ya wanaume wanaochukuwa muda mrefu kufika kileleni huwa wanapata shida kumpa mwanamke ujauzito.Tofauti na kuwahi kufika, kuchelewa kufika ni ngumu kutibika kulingana na sababu zilizosababisha tatizo hizo. Kuchelewa kufika kunaweza kusababishwa na vitu mbalimbali kama ilivyo kuwahi kufika. Mojawapo ni stress, anxiety na kutokuwa na sexual confidence pale mwanaume anapokutana na mwanamke. Pia inadaiwa kuwa malezi yanachangia kwa kiasi fulani hasa kama mwanamume alikuwa na makuzi ya "geti kali". Kuna wanaume wengine wana "controlling personalities" siyo tuu kwenye maisha ya kawaida bali pia kwenye kungonoka.

Baadhi ya wanaume wanaochelewa kufika wanaweza kuwa pia na tatizo la kutoonyesha emotions na kujiachia aka "letting it go" wanapokuwa kwenye 6X6. Sababu nyingine ni kuogopa kumpa mwanamke ujauzito, kuwa na hisia kuwa kikokojoleo cha mwanamke ni kichafu, kulelewa katika maisha yanayofuata dini au utamaduni wa aina fulani, ulevi na matumizi ya madawa ya kulevya, majereha ya ndani kwenye kwenye spinal cordial au kuonyesha dalili za mwanzo kabisa za ushoga.

Kama bado ni kijana unaweza usione kuchelewa kufika kama ni tatizo. In fact, unaweza kuwa maarufu sana kwa wadada wa mujini. Akina dada watafurahia ile mbaya kwa mwanaume kuchukua masaa mawili hadi matatu kufika kileleni huku wao wakiwa tayari wameshafika na kurudi mara sita na nusu! Tatizo linakuja pale mwanaume anapokuwa kwenye mahusiano ya muda mrefu na ya kudumu na mwanamke halafu ukute anataka mtoto. Weeeeeeee!!!

Wapo baadhi ya wanawake ambao hawawezi kuhimili kwa muda wote huo maana wote mnaweza kuishia kuchubuka na kuwa frustrated. Mwanamke atajisikia mnyonge, kudharauliwa kisa mwanaume kuchukuwa masaa kufika aendako. Pia wapo baadhi ya wanawake ambao mwanaume akichelewa sana kufika wanakuwa na wasiwasi sana kama kweli anampenda na akiwahi kufika hasa wanapongonoka kwa mara ya kwanza wanaamini kuwa wamemfikisha mwanaume mpaka ameshindwa kuji-control na kufika aendako fasta. Lakini ikiwa too much inaweza kuwa ni tatizo.

Mwanaume anaweza kuachwa na mwanamke kwa kuchelewa sana kufika na kutaka kuwa na mwanaume who can "come". Kuna baadhi ya watu huwa wanahusisha tatizo tatizo la kuchelewa kufika na umri kwenda mbele lakini ikumbukwe kuwa kwa kawaida wahusika huwa wanaanza kutafuta msaada wa kitaalam wakati wakitaka kupata mtoto kwa udi na uvumba.

Ukipima kati ya kufika mapema na kuchelewa sana kufika ni heri kuwahi kufika, kwa sababu tatizo la kuchelewa kufika linaweza kutibika au mwanaume anaweza kutumia njia nyinge ili mwanamke afike kwanza na yeye kumalizia. Wanaume wanaofika mapema wanaweza kutumia ulimi na vidole vyao. Ulimi ni mgumu sana kuliko mfupa na lazima utamfanya mwanamke afike kabla au hata zaidi yako. Wanasema "a tongue is hard than a double-edged sword". Ulimi ndiyo msuli pekee kwenye mwili unaofanya kazi kupita hata moyo na hata vikojoleo vikiunganishwa pamoja.

Bahati mbaya hakuna matibabu au njia mbadala ya mwanaume anayechelewa kufika. Inadaiwa kuwa hakuna dawa ambayo inaweza kumfanya mwanaume anayechelewa kufika mapema. Madhara ya kuchelewa kufika yanaweza kuwa makubwa na painful kuliko hata yale ya kuwahi kufika.

Kuna mdau mmoja alieleza hapa JF tatizo lake la kuchelewa kufika na jinsi lilivyokuwa linamletea shida kila anapokutana na mwanamke. Kwa maelezo yake inaonekana lilikuwa ni tatizo kubwa sana kwake kuliko hata wale wanaoanzisha threads wakilalamika kuwahi kufika.Kwa hiyo, wale wanaodhani kuwa kufika kileleni mpema ni tatizo, pia kuchelewa kufika nako ni tatizo tena ambalo linaweza lisiwe na tiba.

Tunakushukuru tena Mkuu EMT kwa vitu vya maana sana kaka. Many thanks
Wanaosumbuka kurudia tendo

Kwenye uzi wa Kilometa wa Inawezekanaje kuunganisha baada ya goli la kwanza?, niliandika hivi. Kwa wanawake ni rahisi (depending on your mood, of course) kuliko wanaume kuunganisha goli la pili baada ya goli la kwanza. Wanawake wanaweza kufika mara mbili au zaidi kwa sababu hawaendi kwenye refractory period kama wanaume.

Pia mwanamke anapofika kwa mara ya kwanza bado anaendelea kuwepo kwenye plateau stage kwa dakika kadhaa, kwa maana kuwa bado anakuwa aroused hata baada ya kufika. Ndo maana baada ya kufika tuu bado mwanamke anakuwa na nguvu ya ku-kisss, n.k. wakati a man would just want to be left alone.

Kuna baadhi ya wanawake wanafika kwa kuchezewa matiti tuu au sehemu nyingine za mwili kama shingo. So baada ya kuja mwanaume anaweza kuhamia the other sensitive parts na kuendelea kumwongezea magoli. Pia kama alivyosema LEOMini kwenye uzi husika umri nao una-matter sana. Walioko 20s and early 30s wanaweza kufika mara mbili na zaidi japokuwa wapo hata walio kwenye 40s wanakuwa na multiple-orgasms. Its just a matter of the woman or her man knowing her body.

Kwa sie wanaume wengi wetu tunadhani kuwa ku-orgasm na ku-ejaculate ni kitu kimoja. Hii ni kwa sababu huwa tuna-orgasm and ku-ejaculate kwa wakati mmoja. Sasa hapo sijui Kilometa alikuwa na maana gani kuhusu "kuunganisha mchezo baada ya goli la kwanza". Goli la kwanza kwa maana ya ku-orgasm au ku-ejaculate?

Vitendo vya ku-organism na ku-ejaculate ni vitu viwili tofauti kabisaaaa. Kwa hiyo kuna uwezekano wa mwanaume ku-organism bila ku-ejaculate and vice versa. Utawasikia baadhi ya vijana wanaji-boost humu kuwa wanapiga goli saba, kumbe walichofanya ni ku-ejaculate mara saba, huku wakiwa wame-orgasm labda mara mbili au tatu.

Pia wapo baadhi ya wanawake, kama mwanaume akiamua-ku-orgasm bila ku-ejaculate wanadhani he was faking. Some would even complain when we pull out tunapotaka ku-orgasm bila ku-ejaculate (maana tukiendelea kubakia humo uwezekano wa ku-ejaculate ni mkubwa). Hivyo basi, kitendo cha ku-orgasm bila ku-ejaculate kunamfanya mwanaume kubakia kwenye stage ya excitement na kuweza ku-orgasm tena kwa mara ya pili.

But that may be a tough thing to do na kuishia ku-ejaculate disaini ya aliyosema kaka km kwenye uzi husika. Kufanikiwa inabidi kuwa na PC muscle imara ambayo itasaidia ku-control muda wa ku-ejaculate. Lakini nadhani jambo la muhimu siyo ku-set target, bali kwa pande mbili husika kufurahia hiyo occasion. Kwa wengi quality ina-matter zaidi kuliko quantity. Refer everlenk hapo juu.

Kuhusu kufanya mazoezi itabiki tumtafute Tuko, miss chagga na wengine tujadili in detail suala zima la faida za mazoezi kwenye sita kwa sita. Wengi kama akina Sam Love tunashauri kufanya mazoezi bila kufafanua kisayasi yanasaidia vipi kwenye sita kwa sita?

Kwa mfano, kwa faida ya wengi kuna umuhimu wa kujadili kisayansi uhusiano uliopo kati ya kufanya mazoezi na kuongezeka kwa nitric oxide mwilini, uhusiano wa kula matunda matunda fulani na mbogamboga na kuongezeka kwa nitric oxide mwilini, uhusiano wa nitric oxide mwilini na mishipa ya damu, uhusiano wa nitric oxide na kuongezeka kwa nguvu za kiume na pia na faida nyingine za nitric oxide mwilini.

Siyo tuu mtu ashauriwe ale matikimaji au juice ya mkokomanga bila kuambiwa kisayansi zinasaidiaje mwilini katika kuongeza nguvu za kiume. Na madaktari wetu wengi hawafanyi mazoezi, hawali vyakula vyenye afya so don't expect them kukushauri kwenye hizo anga. Kwa mfano, kuna wataalamu wanadai kuwa mwanaume hatakiwi kula popcorn tuu wakati akitazama sinema. Inadaiwa kuwa popcorn zina faida kwa mwanaume mpaka kitandani ila hakikisha tuu huweki mafuta na chumvi nyingi.

Hii ni kwa sababu Popcorn ni baadhi ya vyakula ambavyo vinaongeza nitric oxide mwilini (kama unajua umuhimu wake kwenye mwili wa mwanaume - just think jinsi viagra na madawa mengine yanavyofanya kazi), ina-maintain testosterone na pia zinasaidia kuongeza madini kama zinc na magnesium. Ila hakikisha popcorn unazokula siyo genetically modified na usile popcorn zilizotengezwa kupitia microwave. Zile za kwenye sinema zinatengenezwaje sijui.

We need a detailed and scientific explanation juu ya faida ya kuwa na nitric oxide mwilini na jinsi ya kuipata. Kuna mdau mmoja alielezea hili kwa Kiswahili na kwa lugha rahisi hapa JF lakini nimetafuta post yake sijaipta. Hopefully, nitaipta.

Wapo wanaosharu kula chakula kama unavyokula dawa. Huli dawa hivi hivi tuu. Lazima kuwe na sababu. Hivyo hivyo kwa vyakula na vinywaji. Kabla ya kula jiulize unakula hicho chakula kwa sababu gani hasa zaidi ya kushibisha tumbo? Je, pamoja na kuwa chakula ni kitamu kinaweza kuwa na madhara yoyote mwilini mwangu? FOOD AS A MEDICINE: A PRACTICAL APPROACH TO HEALTH EATING

Je mtu akifanya mara nyingi sana kuna madhara yeyote? Mkuu 1st AID anajibu
Mkuu Tized ...naomba nikushukuru sana kwa kuipokea michango ya watu kwa uzito wake.
Niliposema unaweza pata athari kwa kufikia mshindo mara tatu au zaidi ndani ya masaa 24 nikusudia upoteaji wa ZMA kwa wingi na hivyo kuleta madhara katika mfumo mwili kama nilivyo elezea hapo juu.

Sasa turudi kwenye kiini, swali je nitawezaje kula tunda na nisiathirike kiafya ....yaani mara ngapi kwa siku, wiki au mwezi? Na ipi ni idadi isiyo na madhara kwenye kula tunda?. Kwanza naomba niweke sawa hapa kwamba ulaji huu unamaana zaidi ya kupata watoto (naongelea walio na mahusiano rasmi) kupiga papuchi kuna unganisha wenza na kunaondoa msongo wa mawazo.

Je nitapata athari gani kupiga match nyingi zaidi, kwanza kama unasaka mwana tunashauriwa kula papuchi mara kadhaa kabla ya mama kufikia upevushaji. Hii inasemwa kwa kufanya hivyo ubora wa mbege katika manii huboreka na hivyo chance ya mama kunasa mimba ni kubwa (kumbe manii zikikaa muda mrefu kwenye korodani huathirika). Lini hasa kama nasaka mtoto siku sahihi? Siku tano kabla ukianza mpaka siku ya upevushaji ni jambo sahihi ingawa idadi ya mbegu itapungua na maji kuongezeka katika manii (manii kuwa epesi) .......angalizo hii haithiri ubora wa mimba.

Uwezo wa ulaji unategemea na mtu na mtu, ingawa tafiti huonyesha wanandoa hucheza mechi 112 kwa mwaka sawa na mara mbili kwa wiki, lakini hii inategemeana na umri. Katika hili swali taasisi ya Kinsey imejibu As just one example, 18-29 year olds have sex an average 112 times per year, 30-39 year olds an average of 86 times per year, and 40-49year olds an average of 69 times per year. Still, averages mean that there are some people above and some people below given number. Averages don't help decide the question of what is right for an individual person.

Tuangalie ukifanya ngono sana nini pia athari zake, hii iko wazi umri unaongea kama utakuwa umesoma vizuri kwamba kadri unavyo kuwa vipaumbele vinabadilika. Stress zinaweza kupungua na kuna wakati walio na umri mkubwa sana hukutana mara moja tu kwa mwaka ua hakuna kabisa.

Kama nilivyo sema awali somo hili ni pana, kuna msawala mengi mfano kwanini mtu hupoteza hamu ya tendo la ndoa na hii ni tofauti na uwezo wa uume kusimama, na tumejikuta tunahangaikia uume kumbe tatizo ni hamu. Somo ni pana na litaendelea kuza mjadala ila ili tusitoke nje ya maudhui ya uzi naomba niishie hapa.

Thanks ICHANA, umetukumbusha vitu mihimu sana pia kuhusu kujikubali, kujali wakati na ahadi, Kuwa na shukrani n.k,

Mkuu Tized asante sana kwa hii mada nimejifunza mengi...

watu wengi tumekuwa WATUMWA wa maneno ya watu..kwanza tujikubali wenyewe kuwa wenye vibamia emolo or mguu wa mtoto wote ni saawa kwenye tendo la ndoa na wanauwezo wa kumfikish mtu kilelen

huu utamaduni wa coppy n paste eti wmwanaume lijali lazima agonge goli sijui tatu or saba achan nazo..tunatakiwa tuangalie SATISFACTION...Mapenzi ni utundu wa kujua mwenzio anatka nni na sio kukariri eti lazima umshike hapa kila siku na nimp three goals nani kakuambia magoli ndo kumtosheleza..watu wanapiga one shout heavy na mtu anakuwa ameridhika wengine saba watu wanaishia kuchubuka tu,.msome mwenzio anataka goli ngapi kwa muda gan...anapenda uunganishe two in one or vipi.MFANNYE MPENZIO RAFIKI

kuna jambo dogo ila lina maana sana baada ya tendo kuzungumza kwa upole na kushukuru..mpe pongezi kama kakukuna palipo.hasa wasichana sie tunapenda hyo,.human being unapompa sifa unamwongezea confidence zaid...kuna watu wakializa hawaongei na wala hajui mwenzie anapenda style ipi

usafi wa mwili na eneo husika huongeza hamu ya tendo.watu tujiswafi hasa wanawake ili kuleta raha kweye tendo ..kitanda...na nguo pia

suala la MUDA hasa kwa ambao hawako kwenye ndoa una mihadi na mwenzio be on time sio mwenzio anafika wewe uanampa sound or nakuja mara folen mara niikuwa na kazi unakuwa tayari ushamwndolea mwenzio hamu na hta kam unaona upo far to excuse mapema...tujitahid kutumia sweet word kwa maana mwanaume most of tyme yupo ready kwa sex ila mwanamke mwandae kiakili may be by chating pia akifika eneo husika msiwe na papara kuku wako manati ya nni..mwandae kimwili hadi unone dalili zote za yey kuwa na utayari

kauli zetu nazo zinachangia watu kutokufika kileleni.mwanaume anahitaji utulivu wa kiakili kauli za madharau tuache jaman.ulimi mwenye sukari na saut hutoa nyoka pangoni.lazima mtu ajiachie na awe huru ili aweze kufika kilele

Mkuu Zogwale tunakushukuru kwa mchango wako makini, hakika umeshekheni!!!
Mkuu Tized ninashukuru sana kwa kunialika katika kuchangia uzi huu muhimu sana ambapo suala la kungonoka kati ya wawili wapendanao limekuwa ni tatizo sana. Tena mbaya zaidi hata vijana ambao hata 40s hawajatimiza lakini wana tatizo kubwa sana. Matokeo yake wamekuwa wakiishia kununua madawa ya kichina au hata kupost humu kuwa wanahitaji msaada. Uliyoyasema hapo kwenye post yako ni haswa habari yenyewe na hakika hata kama umri umeenda lakini kama utazingatia life style na mengine basi hata siku moja hutashindwa kumridhisha mke au mpenzi wako. Mimi kama Zogwale ambaye kiumri niko mbali lakini maisha ya ndani si tatizo kabisa japo siwezi kuwa sawa na wakati ule nikiwa katika 20s na 30s. Cha msingi:
(a) Epuka kuwa na wapenzi wengi kwa kuwa at times unaiikuta nguvu zako kimapenzi zinapungua due to overdose/use.
(b) Epuka magomvi kati yenu na kama ikitokea kuhitilafiana basi kabla hamjaingia kulala yamalizeni tena kama hali inaruhusu malizia na penzi la aina yake. Hapa hamtakaa mchokane,
(c) Mazoezi wewe na mwenzio, kama hajitumi andaeni programme ya mazoezi pamoja. Wote hapa mtakuwa active sana.
(d) Chakula ni dawa na ni sumu!!!!!! kwa nguvu za mapenzi!!!! Epuka vyakula vya kuunga sana!!! Prefer mchemsho. Kula whole grain - kwangu tunakula dona limechanganywa soya, karanga, ulezi, mtama i.e ni lishe tunapikia ughali.
(f) Matunda, mboga za majani na maji mengi.
(g) Pombe natumia occasionally na wine on and off. Kwa hapa wenzangu wa umri wangu walevu wanaonekana wazee mno.
(h) Epuka red meat, kula protein za nafaka na white meat.
(I) Karanga na jamii yake, water melon na mbegu zake, boga na mbegu zake!!!!

Kwa hayo na mengine huna sababu ya Viagra au madawa ya kichina.
Nawasilisha mkuu. Nilikuwa off JF kwa muda kidogo.Sorry for late response.

Mtaalamu wa tiba asilia Mkuu MziziMkavu anatupa vitu vipya hapa:-
Nijuavyo mimi ukitaka kuchelewa kuwahi kufika mapema wewe kama mwenzako inabidi uwe unafanya mapenzi kwa wiki japo mara 3 au mara 4 hiyo itakusaidia wewe mwanamme kuchelewa

kuwahi kufika mapema golini kabla ya mwenzako. Mbinu ya pili ukitaka uwe na nguvu kwenye tendo la ndoa usile chakula masaa 6 kabla ya kufanya tendo la ndoa utakuwa na nguvu za kiume imara. Kwani kula chakula kunasababisha wewe Mwanamme ufike haraka golini na kufunga goli mapema kabla ya mwenzako naye hajamaliza utakuwa wewe umekwisha maliza.

Ushauri wangu: Kama ni Mlevi acha kunywa pombe, kama ni mvutaji sigara acha kuvuta Sigara,kama ni Mlaji wa mirungi acha kula mirungi, kama ni mpigaji wa Punyeto acha kupiga Punyeto, kama ni muangaliaji wa video chafu za matusi acha kuangalia hizo video pia zinasababisha mtu kupiga Punyeto. Ukitaka Dawa kuchelewa kuwahi na dawa ya kuongeza au kurudisha nguvu zako za kiume uwasiliane na mimi bonyeza hapa.Mawasiliano
Anazidi kukazia ndugu MziziMkavu
Kutokula kunasaidia wewe kuwa na Stamina ya nguvu za kiume na kutomwaga mapema. Ukiwa umeshiba kisha unafanya tendo la ndoa unakuwa hauchelewi kumwaga mapema na unakuwa huna nguvu za kiume. Na ukiwa unafanya tendo la ndoa kwa wiki japo mara 3 au mara 4 itakusaidia kuweza kuchelewa pia kumwaga mapema na kukufanya uweze kulizoea tendo la ndoa . Na itapendeza wewe wakati upo kwenye uwanja wa tendo la ndoa mawazo yako usiweke hapo kwenye tendo la ndoa mawazo yako yaweke mbali pia itakusaidia kuchelewa kumwaga mapema.

Mkuu mwakabhuta anafafanua zaidi kuhusu vitambi na virutubisho.
naona katika AFYA ya mwili umegusia zaidi mazoezi na kuuweka mwili fit. Pia wadau msisahau suala la chakula bora hasa hasa protein na aina kadhaa za vitamins. Ndio maana kienyeji mnasikia ukitumia supu ya pweza, karanga etc inasaidia kufanya uwe vizuri kitandani. Chakula bora na mzunguko mzuri wa damu. Kuna jarida moja la kitaalamu watafiti wanasema kutokea kitambi kunahusiana na kujaa mafuta kwenye tumbo na inapunguza kiwango na msukumo wa damu kwenda chini ya kiuno. Hii ina madhara fulani kwa yule bwana mkubwa. Tujitahidi kuondoa vitambi. Pia kwenye suala la chakula bora nina virutubisho vizuri sana vya kutumia kila siku vimetengenezwa kutokana na mimea hasa hasa mizizi ya mmea uitwao Maca kutoka Amerika ya kusini. Virutubisho hivi ni vizuri sana vinaamsha hata nyoka aliyezidiwa na usingizi. Ukihitaji nakuletea hadi hapo ulipo. Nitupie private message tuongee vizuri, nikujibu maswali yako.

Hivi kuchelewa kufika kileleni kwa mwanaume kunaweza kuchangia kutopata mtoto.
Dr EMT anasema (Dr. - PhD ya heshima kutoka kwa Tz)
The most sexual problems in men are (1) premature ejaculation, (2) importance and (3) delayed ejaculation. Delayed ejaculation linaweza lisiwe tatizo baina ya wapendanao hadi pale wanapotaka mtoto.

Baadhi ya malalamiko ya wanawake: Anyone experience Delayed Ejaculation? | Mumsnet Discussion

Kuna aina mbili za delayed ejaculation: primary and secondary. Primary delayed ejaculation ni ile hali ya mwanaume kutowahi kabisa ku-ejaculate wakati wa kujahimiana.

Secondary delayed ejaculation ni ile hali ya mwanaume ku-ejaculate mara moja au zaidi katika kipindi fulani cha maisha yale lakini hawezi tena ku-ejaculate au huwa ana-ejaculate lakini kwa shida sana.

So, wawezakuta wakati mwanaume amebahatika ku-ejaculate, mwanamke hayupo kwenye zile siku za kupata ujauzito.

Ni jinsi gani kuchelewa kufika kileleni kunasababisha tatizo la kutopata mtoto inatagemeana na sababu za kuchelewa kufika.

Sababu zinaweza kuwa za kibaologia, kisaikolojia, kimahusiano na hata za kijamii.

Zinaweza kuwepo sababu za kisayansi, lakini pia hebu fikiria zaidi ya saa moja bado hajafika, huyo mwanamke si ataishia kusepa, let alone kuzaa nae?

Je? Kupiga masturbution {punyeto}kunaweza kusababisha kuishiwa nguvu za kiume?
EMT anasema;-
Hii ni debatable kwa sababu karibu kila mtu huwa anajifanya ni mtaalamu kwenye hili suala.

Hoja za watu wengi zime-base kwenye myths. Inawezakana labda masturbation inaweza kupunguza nguvu za kiume kwa maana ya idadi ya mbegu za kiume na wingi wa shahawa.

Hata hivyo, mwanaume ana kiwanda cha kutengeneza mbegu za kiume na sidhani kama masturbation itasababisha kiwanda hicho kufa.

Kitaalamu, inadaiwa kuwa masturbation haina madhara. Inakuwa na madhara tuu pale inapokuwa ni addiction au inapoingiliana na maisha yako ya kila siku au kama inatumika kama mbadala wa kujahimiana.

Otherwise, masturbation haiathiri uwezo wa mwanaume kuzalisha mbegu za kiume. Kwa kawaida, mwanaume hawawezi kuishiwa na mbegu za kiume kwa sababu mbegu hizo huwa zinazalishwa 24 hours a day, 7 days a week.

Baada ya mwanaume kufika kileleni, itamchukua muda kabla ya kufika tena kileleni. Hii ni kawaida na haina maana kuwa kuna kitu chochote kibaya na mbegu zake za kiume.

Tafadhalali tofautisha hili na ubora/afya ya mbegu za kiume ambalo ni suala tofauti kabisa na halina uhusiano wa moja kwa moja na kupiga punyeto.

Kwa walioathirika na PUNYETO /MASTERBATION.... Mtaalamu wetu MziziMkavu anatoa hekima zake kwa namna kuacha hilo tatizo.
Shukrani sana Kaka Mkubwa.
JINSI YA KUACHA KUPIGA PUNYETO HATA KAMA UMEZOEA VIPI HAPA UTAACHA HII NI KWA WAREMBO WANAOPENDA KUJICHUA PAMOJA NA WAKAKA WANAPOPENDA PIGA PUNYETO.

Kujichua ni tabia ya kingono ambayo inapofanywa kwa kiwango kikubwa inaleta matatizo ya kiumbo na kisaikolojia kwa anayefanya tendo hilo. Na katika kipindi cha zama hizi ambazo majarida, vipindi na hata mitandao mingi inaonyesha picha za ngono ndio kunaifanya tabia hii kushamiri kwa kiwango kikubwa. Kwani vijana wengi wanaingia katika mchezo huu wa kujiridhisha wenyewe bila kujua madhara yatakayokuja baadaye.

Waelimisha rika wengi wamekuwa wakiwaambia vijana kwamba kujichua ndio njia salama ya ngono kwani hatari ya kupata magonjwa kwako haipo na wanaongezea kuwa wafanye kwa kiwango kidogo pale wanapojisikia hamu ya tendo.

Lakini wanasahau kuwaeleza madhara yake pindi inapofanywa kwa kiwango kikubwa na pia wanajua wazi kuwa mara mtu anapoanza tabia hii kuitawala kwa kiwango inakuwa ngumu.

Baadhi ya madhara ambayo unaweza ukayapata ukifanya kwa muda mrefu:
1.Maumivu ya mgongo kwa chini;
2.Kupoteza nywele;
3.Kupungua nguvu za kiume;
4.Kuwahi kumaliza wakati wa tendo;
5.Kupoteza uwezo wa kuona vizuri;
6.Maumivu ya kende;
7.Maumivu ya nyonga;
8.Kuchoka sana;
9.Msongo wa mawazo;
10.Kupoteza kumbukumbu kwa haraka

Dhumuni la makala hii ni kumsaidia yule mtu ambaye tayari anafanya mchezo huu atambue madhara yake na pia afahamu namna ya kujinasua kabla mambo hayajawa mabaya. Kwa wewe muhusika unatakiwa kuwa na hakika kuwa unaweza ukajinasua katika tatizo lako hili.

Wengi wanaume kwa wanawake waliojaribu kujisaidia kuondokana na hili tatizo wameweza, hata wewe kwako ni hivyo hivyo ikiwa utajitambua tu.Kujitambua ni hatua ya kwanza katika safari yako ya kuacha. Unatakiwa uamue kuwa sasa unaacha na pindi unapoweka uamuzi huo utakuwa unasaidia kujipunguzia ukubwa wa tatizo.

Lakini inatakiwa uwe na zaidi ya tumaini au tamanio la kutambua kuwa uamuzi wa kuacha ni muhimu kwako. Ni uamuzi tu.
Ukiweka kweli kabisa mawazo yako katika kuliondoa hili tatizo utakuwa na nguvu ya kuweza kuliondoa kabisa na kujiweka pembeni na vishawishi vya kukurudisha katika hiyo tabia.

Utakapo kuwa ushafanya uamuzi wa kuacha anza kufanya yafuatayo:

1.Usiguse wala kuchezea maeneo yako ya siri kwa muda mrefu labda uwe unajisafisha wakati wa kuoga.

2.Tengana na rafiki au marafiki zako ambao unajua wazi kabisa kuwa nao wana tabia hizo kwani usijidanganye kuwa mtaacha wote kwa pamoja kwani mara nyingi kuacha ni juhudi na maamuzi binafsi.

3.Unapokuwa unaoga usikae muda mrefu maeneo hayo jifute na utoke haraka.

4.Lala na nguo inayozifunika sehemu za siri kiasi kwamba sio rahisi kwa wewe kuzigusa mpaka uivue hiyo nguo, hapa itakusaidia kupata muda wa kutafakari kabla hujafanya tendo lolote.

5.Endapo upo kitandani na mawazo ya tendo hilo yakakujia ,nyanyuka na ujaribu kutembea tembea ili kuyapoteza hayo mawazo kichwani mwako.

6.Usisome majarida ya ngono, na kuangalia picha za ngono kwani vitakuchochea urudi katika tatizo.

7.Anza kusoma majarida na makala za mambo mazuri na yenye kuelimisha na itakusaidia kuulisha ubongo taarifa nzuri.
Mathalani unaweza ukaanza tabia ya kusoma vitabu vya dini itakuasidia sana.

8.Sali, lakini wakati wa kusali usiwe mara kwa mara unalifikiria hili tatizo kwani utaendelea kuliweka mawazoni mwako.
Mtazamo wa mtu mwenyewe ndio unaosaidia kuliondoa hili tatizo kwa haraka.

Ukiweza kutambua kwanini umeingia katika hii tabia, na kuyafahamu mazingira yanayokuchochea wewe kuingia huko unatengeneza uwezo wa kuishinda kwa haraka. Tabia hii ya kujiridhisha mwenyewe itakufanya uwe mtu kwa kujisikia na hatia kila mara, kutojiheshimu mwenyewe na kukufanya uendelee pindi unapopatwa na msongo wa mawazo. Na inapelekea unaanza kujiona mdhambi hata kuhudhuria nyumba za ibada kwako inakuwa ngumu.

Tunakushukuru sana Mkuu giyamo kwa mchango wako, Ukiwa na details na michango zaidi, Tutashukuru kukusikia tena. asante
Kuna aina 2 ya vyakula ambavyo vimefanyiwa utafiti na kubaini kuwa ni moja ya vyakula vinavyosaidia kuongeza nguvu za kiume na havina madhara katika engezeko la nguvu za kiume, katika vyakula hivyo vyenye uwezo wa kuongeza nguvu za kiume kiasili ni:
1. TANGAWIZI
- Tangawizi ni moja ya chakula kinachoweza kurejesha nguvu za kiume, unaweza kuichemsha tangawizi na ukatumia kwa kuinywa kama chai Asubuhi, mchana na jioni pia Tangawizi unaweza ukaitumia katika mchanganyiko wa kiasili kwa kutumia habat soda,asali,kitunguu saumu na tangawizi yenyewe. JINSI
YA KUTUMIA MCHANGANYIKO HUU: Chukua tangawizi na kitunguu saumu vitwange kisha vichanganye na asali pamoja na unga wa habat soda na uwe unakunywa mchanganyiko huu kwa kutumia kijiko cha chai kimoja kutwa mara 3 kwa muda wa wiki moja na utaona mabadiliko.
2. TIKITI MAJI:
-Chakula kingine kinachosaidia katika upande wa kuongeza nguvu za kiume ni tunda la Tikiti Maji, unaweza ukachukua tikiti lako ukalikata na kutengeneza juice ya Tikiti kisha unakunywa ila sio lazima utengeneze Juice hata lenyewe tu unaweza ukalila. Ila jitahidi kutumia tunda hili hata kila siku kwani linasaidia sana kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume.
 
Mkuu umebainisha vyema kwa kuongezea kuna mambo yafuatayo:

1. Kuwa makini na baadhi ya aina ya vyakula...

2. Kukosekana kwa lugha ya aina moja ya kimapenzi baina ya mume na mke...

3. Mazingira ya eneo la mpambano na usafi wa mwanamke...
 
Last edited by a moderator:
Chakula bora, mazoezi, kupumzika, na kuepuka kutumika ovyo, usafi wa mwanamke, mvuto kwenye mapenzi na ujuvi wa mambo! unaweza kuwa na stamina zako lakini mwanyewe akawa hana mvuto na hatii hamasa! wengine huwa tunasimamia show mpaka unaamua kuacha tu!

Vijana wa sku hizi wanapita kumwagamwaga mbegu zao kila sehem mwisho nguvu kwishnei, hata manii zinakuwa nyepesi kama maji!
 
Mazoezi ni muhimu sana, sio unakurupuka alfsjiri then job then bia halafu usiku unataka mzigo u cant.

I ussually play football on weekends na nikitoka huko shemeji yenu shughuli yake anaijua. Ila ikitokea nikapuuzia for some weeks basi perfomance hushuka sana. piga tizi walau vipushups tu asubuhi
 
Mkuu issue kubwa ipo kwenye hii hoja yako:

Timing ya kuanza tendo: Kwa kuwa tendo linahusisha sana hisia za mwili, ukiwa umetumia muda unaotosha kuandaana, basi usiwe na papara mwanzoni, bali uwe na utulivu, pia jitahidi kuzungumza moja mawili wakati unaanza kuzoea mazingira mengine (core business) EPUKA UHARAKA na kuweka sana akili yako hapo, jinafikie mwenyewe kuwa its just a normal thing (mental pride).

Yote yana umuhimu lakini hili huwa nalichukulia kama linaweza kubeba hayo mengine kwa namna moja au nyingine au kwamba mengine yakifanyika bila hili, hamna shida itakuwa iko pale pale. Tatizo la nguvu za kiume mara nyinyi lipo kichwani mwa mhusika.
 
Asante sana Mkuu kwa hekima zako, Umeeleweka vizuri, Ikikupendeza mkuu naomba uzipe maelezo kidogo point zako kwa msaada zaidi kwa wengine wetu.

Labda mtu azingatie vyakula gani apunguze/aache vipi, labda unaposema kukosekana ka lugha moja unamaanisha nini na pia unapozungumzia mazingira ya mpambano (unamaanisha labda kuzoeleka kwa mazingira au usafi wake au uzuri wake)

Many thanks
Mkuu umebainisha vyema kwa kuongezea kuna mambo yafuatayo:

1. Kuwa makini na baadhi ya aina ya vyakula...

2. Kukosekana kwa lugha ya aina moja ya kimapenzi baina ya mume na mke...

3. Mazingira ya eneo la mpambano na usafi wa mwanamke...
 
New points!!! Asante Mkuu CYBERTEQ.

Vipi kwenye hapo kwenye RED, Umenikumbusha hoja muflisi iliopo mitaani kuhusu ''law of USE and MISUSE'' wakimaanisha kwamba kadiri mtu anavyotumika anapata uzoefu na ujuzi zaidi na anawezea zaidi.... unaizungumziaje hio hoja kwa msaada zaidi kwa hawa vijana wetu mkuu?

Shukrani sana Kaka.
chakula bora, mazoezi, kupumzika, na kuepuka kutumika ovyo, usafi wa mwanamke, mvuto kwenye mapenzi na ujuvi wa mambo! unaweza kuwa na stamina zako lakini mwanyewe akawa hana mvuto na hatii hamasa! wengine huwa tunasimamia show mpaka unaamua kuacha tu! Vijana wa sku hizi wanapita kumwagamwaga mbegu zao kila sehem mwisho nguvu kwishnei, hata manii zinakuwa nyepesi kama maji!
 
Nashukuru Mkuu Sibonike kwa mawazo ya msingi sana. Vipi mkuu kuna mbinu zadi ya kusaidia apo labda!!!
Asante!!!!

Mkuu issue kubwa ipo kwenye hii hoja yako:

Timing ya kuanza tendo: Kwa kuwa tendo linahusisha sana hisia za mwili, ukiwa umetumia muda unaotosha kuandaana, basi usiwe na papara mwanzoni, bali uwe na utulivu, pia jitahidi kuzungumza moja mawili wakati unaanza kuzoea mazingira mengine (core business) EPUKA UHARAKA na kuweka sana akili yako hapo, jinafikie mwenyewe kuwa its just a normal thing (mental pride).

Yote yana umuhimu lakini hili huwa nalichukulia kama linaweza kubeba hayo mengine kwa namna moja au nyingine au kwamba mengine yakifanyika bila hili, hamna shida itakuwa iko pale pale. Tatizo la nguvu za kiume mara nyinyi lipo kichwani mwa mhusika
 
Last edited by a moderator:
Asante sana Mkuu kwa hekima zako, Umeeleweka vizuri, Ikikupendeza mkuu naomba uzipe maelezo kidogo point zako kwa msaada zaidi kwa wengine wetu. Labda mtu azingatie vyakula gani apunguze/aache vipi, labda unaposema kukosekana ka lugha moja unamaanisha nini na pia unapozungumzia mazingira ya mpambano (unamaanisha labda kuzoeleka kwa mazingira au usafi wake au uzuri wake)

Many thanks

Mkuu nikipata wasaa nitarudi tena hapa kueleza kwa kirefu...
 
Nashukuru Mkuu Sibonike kwa mawazo ya msingi sana. Vipi mkuu kuna mbinu zadi ya kusaidia apo labda!!!
Asante!!!!

Mkuu suala zima lipo kwenye mental pride kama ulivyoainisha - kujiweka katika hali ya kuona kuwa tendo ni la kawaida. Naunganisha hilo na signature yako ''Happiness doesn't result from what we GET, but from what we GIVE'' Dr. Ben Carson.

Nasema hivyo kwa sababu mara nyingi kwa kwa kutojua mwanaume huwa selfish kwenye tendo lenyewe. Anamaliza yeye bila kujali mwenzake kama kafika au la. Mwanamke asiporidhika anaweza kumtangazia mwanaume kuwa hana uwezo na akijua anakosa confidence. Tayari inaingia kichwani kuwa hawezi na anabaki na hali hiyo. Suluhisho? kumridhisha, kuliko kujiridhisha kwanza!
 
Yoote yaliyoelezwa ni ya msingi sana lakini kwa kukazia tuu, swala la mazoezi ni muhimu zaidi pengine kuliko yote hapo.

Siku hizi vijana wamekuwa wavivu sana kufanya mazoezi ndio maana mikiki mikiki kadhaa tuu mtu limi nje kama jibwa.
Alafu fasta unakimbilia kumtafuta mzizimkavu akuelekeze dawa za kuongeza nguvu na kunenepesha uume.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom