Goli la Everton dhidi ya Man United kwenye mechi ya leo ni ‘offside’?

MalcolM XII

JF-Expert Member
Mar 19, 2019
5,236
14,205
Naona watu wengi wanabishana baada ya kutoka kibanda umiza kwamba goli la Everton la dakika ya 90+ ni OFFSIDE.

Kwa kifupi ile ni offside ya wazi kabisa kwa wale wanaojua sheria za mpira.

Sheria ya Offside inaeleza kuwa Mchezaji akiwa amezidi kuelekea kwenye lango la timu pinzani hatakiwi kujishughulisha na mpira ili kuvunja Offside. kinyume chake ni kweli.

Kwa maana hiyo, Gyfy Sigurdson hakutakiwa kuinua mguu wake kuukwepa mpira, kwani kitendo cha kufanya hivyo nimemfanya yeye ajihusishe moja kwa moja na mpira hali ya kuwa amezidi.

Alipaswa akae vile vile.

FULL STOP.
 
Na huo ndo uhalisia.Bila kutoa miguu mpira ule usingeingia wavuni.Halafu anaonekana kwa makusudi kabisa anainua miguu na kuupisha mpira uende hilo ndo limemkost.Labda lingekuwa goli kama mpira ungekuwa katika high speed ukamgonga ukaingia ila yeye anaukwepa kabisa ule ni uhuni.
NB:Benitez kala umeme.

Sent using Jamii Forums mobile app
Benitez yupi mkuu?

Ni Ancelotti braza
 
Hiyo sio sababu ya kukataa offside. Inaangaliwa wakati mpira unapigwa mchezaji wa mwisho alikuwa wapi!
Kawaida mpira ukimgusa mchezaji wa timu pinzani kbl ya kukufikia wewe hata kama ulikuwa kwenye offside pisition hiyo inakuwa sio offside tena, so hata kama Sigurdson alikuwa kwenye offside position, but kitendo cha mpira kumgusa maguire kbl ya kupishwa na sigurdson ile sio offside tena, na hata km sigurdson angeugusa km ulimgusa maguire mwanzo nayo pia sio offside.

Pale refa kashindwa kutafsiri sheria ndiyo maana everton wanalalamika, ni kweli walinyimwa goli halali kwa VAR.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
No.

Huujui mpira; mpira ukipigwa kipa akaucheza halafu mchezaji wa timu pinzani hata km akiwa kwenye offside position akiuwahi akafunga goli linakuwa halali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa case yako hiyo uko sahihi (kipa akiokoa mpira na ukamkuta mshambuliaji aliyekua offside).

Kwa case ya leo msingi mkubwa uko hapa; je
1. Maguire aliupiga mpira kwa makusudi (deliberately kicked the ball so as to save)
2. Mpira ulimgonga (It was a deflection)

Kama jibu ni namba moja hapo juu, basi atakua amevunja offside ya Siggurdson na hivyo goli lile kuwa ni halali.

Kama jibu ni namba mbili hapo juu, basi Siggurdson anabaki kuwa ameotea na hivyo goli lile sio halali.
 
Kawaida mpira ukimgusa mchezaji wa timu pinzani kbl ya kukufikia wewe hata kama ulikuwa kwenye offside pisition hiyo inakuwa sio offside tena, so hata km sigurdson alikuwa kwenye offside position, but kitendo cha mpira kumgusa maguire kbl ya kupishwa na sigurdson ile sio offside tena, na hata km sigurdson angeugusa km ulimgusa maguire mwanzo nayo pia sio offside.

Pale refa kashindwa kutafsiri sheria ndio maana everton wanalalamika, ni kweli walinyimwa goli halali kwa VAR.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni sawa ila unatakiwa kujua kwamba offside inaanza kuhesabika wakati mchezaji wa mwisho wa timu yako alipougusa mpira.
Kwahiyo endapo sigurson asingekuwa kwenye eneo la offside wakati mchezaji wa timu yake alipouwa anapiga lile shuti
Basi isingekuwa offside.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa case yako hiyo uko sahihi (kipa akiokoa mpira na ukamkuta mshambuliaji aliyekua offside).

Kwa case ya leo msingi mkubwa uko hapa; je
1. Maguire aliupiga mpira kwa makusudi (deliberately kicked the ball so as to save)
2. Mpira ulimgonga (It was a deflection)

Kama jibu ni namba moja hapo juu, basi atakua amevunja offside ya Siggurdson na hivyo goli lile kuwa ni halali.

Kama jibu ni namba mbili hapo juu, basi Siggurdson anabaki kuwa ameotea na hivyo goli lile sio halali.
Navyojua mpira ukimgonga/kumgusa mpinzani iwe bahati mbaya au vingine hapo offside inakuwa imekufa, vyema uweke hiyo sheria hapa kama unayo tuione.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni sawa ila unatakiwa kujua kwamba offside inaanza kuhesabika wakati mchezaji wa mwisho wa timu yako alipougusa mpira.
Kwahiyo endapo sigurson asingekuwa kwenye eneo la offside wakati mchezaji wa timu yake alipouwa anapiga lile shuti
Basi isingekuwa offside.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni sawa unaposema "offside inaanza kuhesabika" ila pia ukumbuke "offside hubadilika muda wowote" kutegemeana na movement za wachezaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lile ni goli halali kabisa! Halima Gwaya aliugusa mpira na kuivunja offside.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sheria ya offside haitoi msamaha kwa offside kama mchezaji wa timu inayoshambuliwa akiugusa mpira.
Inatoa msamaha huo pale tu ambapo kuugusa mpira huo kutakua ''kwa kuokoa'' (hiki ni kitendo cha kusudi).

Mpira ukimgonga beki (bila kuwa na kusudio la kuuondoa) unakua umemgusa lakini haufuti offside.

Kwa madai yako wewe ni kwamba katika scenario zote mbili hapo juu offside inakua imefutika. (Sijui unatumia sheria gani, kama ipo nitatamani uiambatanishe hapa).

Busara ya kuweka kipengele au masharti hayo juu ya mchezaji wa timu inayoshambuliwa kuugusa mpira iko hapa.... Naomba nieleze kwa mfano kwa kuwatumia wachezaji wawili wa Barcelona (Messi na Suarez) na mmoja wa Madrid (Ramos).

Endapo Messi anao mpira na wanaishambulia Madrid, lakini Suarez wakati huo yuko offside, Messi angeweza kutoa pasi kwenda kwa Suarez (aliyepo kwenye offside position) kwa kum-babatiza Ramos na mpira (Ramos atakua ameugusa) na hivyo kufuta offside ya Suarez.

Ili kuondoa hila za namna hii, sheria ya offside inaitambua scenario ya namna hii kama ni offside, vinginevyo, itafutika pale tu ambapo Ramos atanasa pasi ya Messi kwenda kwa Suarez na katika kuokoa mpira huo ukamfikia Suarez akiwa offside position. Hapo offside inakua imekufa kifo chema.

Karibu kwa mjadala tuelimishane zaidi kama hili halijaeleweka baada ya maelezo hayo hapo juu.
 
Back
Top Bottom