Golden Sanga atangaza nia Ruvuma ya kugombea kiti kwa tiketi ya CCM

beyanga

Senior Member
Jul 17, 2012
183
22
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Golden Sanga (Sanga One), ametangaza nia ya kugombea uenyekiti wa chama hicho wilaya ya Songea katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari juzi mjini hapa, Sanga alisema ameamua kugombea nafasi hiyo, ili kurudisha heshima ya chama hicho mjini hapa.

Alisema kila kukicha mvuto wa chama hicho miongoni mwa jamii umekuwa ukipungua kutokana na matendo maovu yasiyokuwa ya kimaadili yanayofanywa na viongozi wake ambayo yamekuwa yakiwakatisha tamaa wananchi na wanachama wa chama hicho.

Alieleza kuwa hali hiyo imesababisha kata 6 kati ya 21 kuchukuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.

Alieleza zaidi kuwa amejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na viongozi wenzake watakaochaguliwa kushika nafasi mbalimbali ndani ya chama kukijenga chama na kuleta ushindi stahiki katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2015.


 
nape huwa ansema kuwa ccm ni imara haina migogoro ia wanachama wengi itatawala milele hata wote wakiisha yeye hatoki ni vuvuzera haswa
 
Back
Top Bottom