Godson: Mchungaji kiboko ya wezi, matapeli Hedaru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Godson: Mchungaji kiboko ya wezi, matapeli Hedaru

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Msongoru, Sep 23, 2008.

 1. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2008
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Na Miki Tasseni

  MKAZI mmoja wa Dar es Salaam mwenye umri wa kati, hivi karibuni alijikuta akiwa Hedaru, mkoani Kilimanjaro usiku wa Jumamosi akitokea Arusha.


  Basi la mwisho kutoka Moshi kwenda Dar es Salaam ambalo liliondoka Moshi saa 11:00 jioni liliishia Hedaru, hali ambayo ililazimisha abiria kadhaa kutafuta usafiri mbadala. Huwa kuna malori yanayochukua abiria kama yana nafasi za kuketi.


  Wakati mkazi huyo akiwa anasubiri kupatikana kwa usafiri kama huo, alijiuliza kama kweli ana haraka ya safari kiasi cha kuwania kudandia lori! Aliona ni heri angebaki pale na kutumia nafasi hiyo kumtembelea na kumshukuru mwombaji na mtoa dawa za ukimwi aitwaye Nakundwa Mbonea, ambaye baadaye alifahamishwa kuwa ni mwinjilisti katika Kanisa la Bethlehem SDA la mji huo mdogo.


  Alichoshangaa sio kumwona dada huyo, mwenye umri wa miaka 30 na ziada kidogo, ambaye alikuwa gumzo la wakazi wa eneo hilo, bali mchungaji mstaafu, Godson Elieneza wa kanisa hilo, au kama wengi wanavyomwita, Pastor Godson.


  Yeye na mwinjilisti Nakundwa ni watu maarufu sio katika usharika huo tu, bali mkoani humo, nchini na nje ya nchi, hasa kwa wafuasi wa Kanisa la Sabato.


  Nje ya kanisa hilo huwa hawatajwi sana. Mwinjilisti Nakundwa ni mpwa wa Pastor Godson, na alipata maono kwa tukio tofauti, siyo kupewa au kurithishwa vipaji na mchungaji. Jambo la kusisimua kuhusu Pastor Godson, ni jinsi ambavyo jamii nzima katika eneo hilo imekuwa ikitegemea maombi yake ili kudhibiti maovu, na hasa wizi au utapeli.


  Watu wamegundua kwa miaka mingi kuwa maombi yake yana nguvu kubwa, hivyo wengi wanachelea kufanya kosa halafu suala hilo lifikishwe kwake, kwani hakuna suala la kuonewa au vinginevyo.


  Suala likifikishwa kwake, mhusika au wahusika wataitwa na kuulizwa kama wanatambua madai yaliyotolewa. Wakikataa, hufuata rai ya 'tuombe,' na hapo, kama aliyetenda kosa atabakia vile vile na sala ikafanyika, inamdhuru. Kumetokea visa kadhaa hivi karibuni kuhusiana na maombi ya Pastor Godson, ikiwa ni pamoja na kurudishwa fedha au gari lililopotea, kwani aliyechukua anakosa raha na kumlazimu kudisha alichoiba.


  Katika tukio moja la wizi wa ng'ombe, wakazi ambao walipoteza mifugo hiyo zizini walielekezwa kuwatafuta kaskazini, yaani kuelekea Same, Lembeni au Mwanga, kwa sharti kwamba wakiwakuta wasiwapige.


  Waliwakuta wezi wa ng'ombe wakiwa wamelala maeneo ya Lembeni, hivyo wakarudisha ng'ombe, hawakuwagusa kabisa, kama walivyoelekezwa. Mtu mmoja anaelezwa kwamba alikuta mfuko wake wa 'rambo' wenye Sh9milioni umetoweka katika basi, akauliza akaambiwa mwanamke mmoja alishuka nao Hedaru, hivyo akarudi kuulizia kama kuna mtu kama huyo.


  Alipoanza kuulizia akaelekezwa kwenda kwa Pastor Godson, na alipomhadithia, akamhakikishia kuwa ni fedha zake halali kabisa, alimwombea. Yule mtu akaenda zake lakini akaacha mtu wa kuulizia kama mhusika alishuka hapo na kama anafahamika, kazi ambayo haikuchukua muda.


  Yule mwanamke alikuwa amenunua lori moja la mawe na kokoto kujenga msingi wa nyumba, akawa hana raha, na huyo mpelelezi alipofika tu akawa wa kwanza kuanza kumweleza anachotafuta. Alikuwa amekwishatumia Sh milioni moja. Msharika Kiondo Kisaka (37), ambaye ni Mkurugenzi wa kanisa hilo anasema wachungaji hao wanawafanyia maombi watu wengi, na hata kwa njia ya simu kama ambavyo msafiri huyo aliwahi kusikia kwa jamaa zake waliougua na kupata msaada wa dawa na maombi kutoka Hedaru.


  Ni watumishi na watoa huduma ambao hawachukui hata senti tano ya malipo, iwe ni kwa dawa au kwa maombi, na wakazi wa eneo hilo wanasema Pastor Godson kwa jumla anawategemea wana wa familia walioko ng'ambo, si maombi. Anaeleza Kisaka kuwa hata polisi na mahakama, yaani serikali, mara nyingi wanaomba huduma zake pale wanapokabiliwa na kesi au madai ambayo wanaona ni magumu kuyashughulikia. Kwa mfano, katika kesi za kukopeshana fedha au kulipana bila stakabadhi, kukabidhiana mali au mizigo, kuna kila aina ya mifarakano ambayo haina ushahidi ni nani kafanya nini, hivyo madai hayo yanapelekwa kwa Pastor Godson. Endapo mtu atakataa kwenda kwenye maombi hayo, basi ina maana anakiri hatia na polisi wanaweza kumkamata na kumfungulia kesi. Wengine wanaowahafamu watu hao mashuhuri pale Hedaru na eneo lote la Upareni au Wilaya ya Same wanaeleza kuwa ilikuwa vigumu hasa kwa mwinjilisti Nakundwa kufikia kutambuliwa rasmi kama kiongozi wa kanisa na mwinjilisti kwa kazi yake hiyo.


  Wengi waliona kuwa Mkristo hawezi kupata maoni ya kuonyeshwa dawa za ugonjwa wa ukimwi, kwani hiyo ni sawa na kuwa mganga wa kienyeji.


  Wapo wengine ambao pia wanakosoa shughuli za uponyaji au mara nyingine kurudisha misukule makanisani, wakisema hiyo inakaribia kabisa ushirikina; wengine wanasema mtu akifa basi apumzike tu.

  Kwa vile Pastor Godson anasali tu na kusoma mistari ya Biblia, bila kushika dawa ya aina yoyote, tatizo la kuhusishwa na ushirikina halipo, lakini alikuwa na upinzani wa aina yake. Lakini wapo wanaosema inaweza kusomwa tena na tena, bila madhara yoyote. Kutokana na kuchelea kufikishwa kwa Pastor Godson kwa maombi, vibaka wamekatisha kabisa shughuli Hedaru, lakini hali hiyo huenda ikabadilika pale mzee huyo mwenye umri wa miaka 84 atakapocha huduma yake rasmi, au kufariki dunia.


  Sasa hivi kuna jitihada zinafanywa kutafuta misaada kununuliwa vinasa na vipaza sauti, na mashine zake ili Pastor Godson asipate shida kuzungumza kwa sauti ya juu katika mahubiri Jumamosi.


  Watu wanafurika kutoka sehemu tofauti kuja kumsikiliza ingawa ni mchungaji mstaafu, na washarika wana hamu ya kuhakikisha kuwa Pastor Godson haachi kuhuburi kutokana na kukosa vifaa vya kutawanya na kukuza sauti, ambayo inahitajika. (NB: Picha zimeambatanishwa, anazo Natasha - features, The Citizen) (Mwisho)
   
 2. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hii thread ingepelekwa kwenye mambo ya dini au matangazo ya biashara.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huyu mchungaji atusaidie pesa zetu za EPA na vyote mafisadi walivyokwapua virudishwe kwa Watanzania, IPTL, Richmond, BOT Twin towers, etc etc....
   
 4. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Bwana asifiwe sana. Tafadhali tunaomba namba za simu za huyu pastor kwani wengine tuko nje ya nchi na tunahitaji msaada wa maombi.
   
 5. L

  Lione Senior Member

  #5
  Sep 23, 2008
  Joined: Dec 1, 2007
  Messages: 115
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sasa Anasubiri nini kuwafanya kina lowasa na wenzie wasirudishe vijicent vyetu?kufanya wakoloni walioiibia africa wakaona aibu na kurudisha amali zetu?tunamsubiri kwa hamu sana.
   
 6. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tafadhalini naomba za simu za huyu mtumishi wa mungu. Ninahitaji msaada wa maombi.
   
 7. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mwenyezi Mungu azidi kumbariki Mchungaji Godson Elieneza na Mwinjilisti Nakundwa Mbonea
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Sep 29, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Serikali ifanye mpango wa kumpeleka aidha muhimbili akasaidiane na madaktari wa magonjwa sugu, yakiwemo ukimwi na ndugu zake... au awe psychic wa serikali. Kama vile wanavyowatumia wamarekani kwenye baadhi ya kesi zenye kuleta utata.

  Mlioko huko muulizeni kwani hawezi kuwatatulia wabongo matatizo yao... kuanzia Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar mpaka ile issue ya East Afrika... lol!

  Kaaaazi Kweli... kweli...!
   
 9. Mkanya

  Mkanya JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 600
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  yaani wewe mdhaifu sana yaani kama hauna chakuchangia ungejikalia kimya tu kama mimi yaani unaonyesha kabisa unakejeli.
  Shame on you.
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Sep 29, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Pole kijana, sasa wewe inakuuma sana kwa yeye kuombwa awasaidie wabongo wenzake kuondokana na matatizo yaoo? Wewe mbona una roho mbaya hivyoo...!?
   
 11. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  hii ni habari njema sana naomba kupata namba yake ya simu kama ipo
   
Loading...