Godlisten Malisa ajitolea kuchangisha hela kwaajili ya bima ya afya ya watoto 59

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,143
22,112
Habara wanaJF
Leo nimesoma andiko la mwanaCHADEMA ndugu Malisa GJ na kufarijika kwa hatua aliyochukua ya kuendeleza alichokuwa kaanzisha Mheshimiwa mstaafu Makonda. Huyu kijana ni hazina ya taifa. Yuko tofauti sana na misimamo ya baadhi ya wakubwa wengine wa chama chake waliojaa chuki. TAFADHALI soma alichoandika kisha kwa pamoja tuchangie jambo jema lililoasisiwa na Mh Makonda.

Kaandika Malisa Gj;
1618405542380.png

Jana shule zimefunguliwa bada ya likizo ya Pasaka. Nikajulishwa kuwa mtoto niliyejitolea kumlea katika kituo cha Watoto Wetu kilichopo Mbezi mwisho, Resty anaumwa. Nikamfuata shuleni kumpeleka hospitali. Kufika nikakuta wenzie wawili nao ni wagonjwa wameletwa hospitali na matron wa kituo.

Nikamlipia Resty, lakini kwa bahati mbaya fedha ailiyokuja nayo Matron haikutosha kulipia watoto wengine wawili aliokuja nao. Nikaongezea, kuhakikisha wanapata matibabu wote watatu. Baadae nilipomuuliza Matron kuhusu bima za afya akasema hawana bima kwa sasa.

Mwaka 2018 aliyekua RC wa Dar, Paul Makonda aliwakatia bima watoto wote kituoni, ambapo ziliisha muda wake baaada ya mwaka mmoja. Baada ya hapo hawajawahi kupata tena bima za pamoja. Unless mtu ajitolee kumlea mtoto amlipie na bima. Kwabiyo kuna watoto 6 wana bima ambazo wamelipiwa na walezi wao, wengine wanatibiwa kwa cash.

Nilipofuatilia nikaambiwa bima zao zinagharimu kiasi cha TZS 50,400/= tu kwa mtoto mmoja, ambapo wanapata assurance ya matibabu kwa mwaka mzima. Nikagundua pesa tuliyotumia kumtibia Resty na wenzake ingetosha kuwakatia bima wote watatu wakapata uhakika wa matibabu kwa mwaka mzima.

Idadi ya watoto waliopo kituoni ni 28, waliopo shuleni (boarding) ni 37 ambao umri wao ni chini ya miaka 18, jumla 65. Ukitoa 6 wenye bima wanabaki 59. Ili wapate bima inahitajika TZS 2,973,600/= tu, wawe na uhakika wa matibabu kwa mwaka mzima.

Naomba tuwe na challenge ya saa 24 tu kutafuta 3M kwa ajili ya bima ya watoto hawa. Kama ukiguswa kumlipia mtoto mmoja itakua jambo heri zaidi. Piga simu kituoni utapewa details za mtoto, utamkatia bima na kuipeleka kituoni itakapokua tayari.

Kama huwezi kumlipia mtoto mmoja basi unaweza kuchangia chochote iwe jero, buku, 5K, 10K au zaidi ili kufikia malengo ya kila mtoto kupata bima ya afya hapo kituoni.

Tuma mchango wako kwenda kwa msemaji wa kituo (MPESA) 0752 247200, Ndahani Mwenda.

#GiftedHearts #RudishaTabasamu #LetLoveLead #MalisaGJ
 
Tatizo umeingiza Makonda.. mbali na kuendeleza huyu Malisa GJ ni akili kubwa. Anasaidia watu wengi sana labda kama leo ndio umemfahamu. Hashiki pesa yeye ni kuhamasisha
Sijaingiza mimi. Malisa mwenyewe kaandika kuhusu Makonda.
 
Hakuna kuchanga, Ye ka kaamua kusaidia asaidie tu, na Sisi Pia tunasaidia watu pasipo kumwambia yeye
 
Habara wanaJF
Leo nimesoma andiko la mwanaCHADEMA ndugu Malisa GJ na kufarijika kwa hatua aliyochukua ya kuendeleza alichokuwa kaanzisha Mheshimiwa mstaafu Makonda. Huyu kijana ni hazina ya taifa. Yuko tofauti sana na misimamo ya baadhi ya wakubwa wengine wa chama chake waliojaa chuki. TAFADHALI soma alichoandika kisha kwa pamoja tuchangie jambo jema lililoasisiwa na Mh Makonda.

Kaandika Malisa Gj;

Jana shule zimefunguliwa bada ya likizo ya Pasaka. Nikajulishwa kuwa mtoto niliyejitolea kumlea katika kituo cha Watoto Wetu kilichopo Mbezi mwisho, Resty anaumwa. Nikamfuata shuleni kumpeleka hospitali. Kufika nikakuta wenzie wawili nao ni wagonjwa wameletwa hospitali na matron wa kituo.

Nikamlipia Resty, lakini kwa bahati mbaya fedha ailiyokuja nayo Matron haikutosha kulipia watoto wengine wawili aliokuja nao. Nikaongezea, kuhakikisha wanapata matibabu wote watatu. Baadae nilipomuuliza Matron kuhusu bima za afya akasema hawana bima kwa sasa.

Mwaka 2018 aliyekua RC wa Dar, Paul Makonda aliwakatia bima watoto wote kituoni, ambapo ziliisha muda wake baaada ya mwaka mmoja. Baada ya hapo hawajawahi kupata tena bima za pamoja. Unless mtu ajitolee kumlea mtoto amlipie na bima. Kwabiyo kuna watoto 6 wana bima ambazo wamelipiwa na walezi wao, wengine wanatibiwa kwa cash.

Nilipofuatilia nikaambiwa bima zao zinagharimu kiasi cha TZS 50,400/= tu kwa mtoto mmoja, ambapo wanapata assurance ya matibabu kwa mwaka mzima. Nikagundua pesa tuliyotumia kumtibia Resty na wenzake ingetosha kuwakatia bima wote watatu wakapata uhakika wa matibabu kwa mwaka mzima.

Idadi ya watoto waliopo kituoni ni 28, waliopo shuleni (boarding) ni 37 ambao umri wao ni chini ya miaka 18, jumla 65. Ukitoa 6 wenye bima wanabaki 59. Ili wapate bima inahitajika TZS 2,973,600/= tu, wawe na uhakika wa matibabu kwa mwaka mzima.

Naomba tuwe na challenge ya saa 24 tu kutafuta 3M kwa ajili ya bima ya watoto hawa. Kama ukiguswa kumlipia mtoto mmoja itakua jambo heri zaidi. Piga simu kituoni utapewa details za mtoto, utamkatia bima na kuipeleka kituoni itakapokua tayari.

Kama huwezi kumlipia mtoto mmoja basi unaweza kuchangia chochote iwe jero, buku, 5K, 10K au zaidi ili kufikia malengo ya kila mtoto kupata bima ya afya hapo kituoni.

Tuma mchango wako kwenda kwa msemaji wa kituo (MPESA) 0752 247200, Ndahani Mwenda.

#GiftedHearts #RudishaTabasamu #LetLoveLead #MalisaGJ
Akifanya mambo kama haya anakuwa hazina. Ila akizungumza ugoro wenu anakuwa mbaya?
 
Back
Top Bottom