Godfrey Zambi katika sura mbili: Ya bungeni na ya jimboni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Godfrey Zambi katika sura mbili: Ya bungeni na ya jimboni!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lukolo, Apr 27, 2012.

 1. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Baada ya kuona jina la Zambi katika list ya majina yanayopigiwa chapuo juu ya uwaziri, ilinibidi nifanye ufuatiliaji kidogo kwa wenyeji wa hapa Mbozi kwa kuwa nipo huku. Na majibu niliyopata ni kama haya:

  Godfrey Zambi hatakiwi Mbozi kwa taarifa yako. Huyu jamaa ni corrupt sana
  tofauti na anavyojitambulisha bungeni. Zambi hupata ubunge kwa rushwa ya kusaidiwa na wafanyabiashara Wakinga wa Vwawa na Mloo. Wafanyabiashara hao humsaidia kwa imani kuwa atalinda interest za wakaazi wa Mbozi ambao si Wanyiha.

  Na politics zinekuwa hivyo tangu wakati wa mbunge Halinga, ambaye hapo nyuma alionekana kuwanyanyasa wakaazi wa Mbozi ambao si Wanyiha. Zambi ndiye amekuwa kimbilio la hawa wakaazi kwa matumaini ya ulinzi.

  Nakuhakikishia akipewa uwaziri yataanza kuibuka madudu ya rushwa yakitokea Mbozi mashariki. We subiri tu. Sana sana tukio hilo litamuongezea kijana Mwampamba wa chadema nguvu zaidi ya kushinda 2015. Nipo hapa.

  My take: Sehemu kubwa ya wabunge wa CCM wanaojifanya kupiga kelele bungeni ni wanafiki. Kama Zambi anashinda kwa rushwa anawezaje kusimama kuipinga rushwa kwa dhati? Huyu akipewa kitu kidogo si anafunga mdomo au hata kugeuza mwelekeo kabisa? Na akipewa uwaziri je, anawezaje kujitenga na wizi na dhuluma ilhali na yeye ni uzao wa dhuluma?
   
 2. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Kuna mshikaji wangu alimkimbiza sana 2010, nahisi alichakachuliwa...

  Ila naona bado anapiga jaramba!!
   
 3. Mwanyasi

  Mwanyasi JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 5,785
  Likes Received: 1,921
  Trophy Points: 280
  Alipotangazwa mshindi Kule Mbozi, wananchi walimfuata nyumbani kwake ili wachome nyumba yake lakini walizuiliwa na polisi, wananchi wakatangaza kuwa mbunge wao atakua Silinde ambaye ni mbunge wa Mbozi West mpaka 2015! Hivo huyo jamaa hatakiwi kabisaa!
   
 4. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Now I am getting the real picture. Unajua mimi sikuwa nafahamu historia yake ya huko Mbozi. Nilikuwa naamini kwamba vile anavyopiga kelele bungeni ndvyo anavyokubalika huko kwao. Sasa kama yeye ni mwizi, anawezaje kuwapinga wezi wenzie? Ni kwa vipi shetani amhukumu shetani mwenzake?
  Vipi huyo mpinzani wake hakuamua kwenda mahakamani?
   
 5. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ehee, Mwanyasi, wananchi wanasema sababu zao ni nini hasa.
  au ndo hizo rushwa kwenye uchaguzi?


   
 6. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,659
  Trophy Points: 280
  Kafulila aliwahi kumbamba akipokea rushwa live huko mkoani Tanga na kumsema bungeni! Hadi leo spika hajatoa ufafanuzi pamoja na kuombwa na Zambi kumtaka Kafulila athibitishe!!
   
 7. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Dah, umenikumbusha hii kitu. Nilisahau kabisa, na kujiona nikimsifia Zambi kwamba ni mmoja wa watu anyeweza kuwa kiongozi mzuri wa nchi katika nafasi ya uwaziri. Kwa hoja ya wananchi wa Mbozi plus habari hizi napata kumwelewa vema Zambi katika picha yake halisi. Na kwa ukweli huu, ni wazi kwamba JK, hana man power ya kuipa uwaziri iwapo atalivunja hili baraza lililopo. Maana wote ni wale wale tu.
   
 8. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mimi natokea jimbo la Mbozi Mashariki, ni kweli kabisa Zambi hakupita kihalali kiasi kwamba nyumba yake ilivunjwa vioo vyote baada ya kutangazwa mshindi kwa hira. Miezi sita ya kwanza ya ubunge wake alitumika akiwa uhamishoni Dare es salaam, kwa sababu wanyiha walitangaza kumua, mara kadhaa gari yake ilshambuliwa kwa kusudi hilo. Lakini kukwepa mtego wa wananchi alikuwa akitumia gali tinted la bwana mmoja aneitwa ugali wa kijiji cha Ichesa.
   
 9. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,544
  Likes Received: 10,475
  Trophy Points: 280
  kifupi Zambi hatakiwi kabisa mbozi. sababu ni kwamba majimbo yote mawili mbozi mashariki na magharibi chedema ilishinda vizuri sana.tatizo ni kwamba ccm iligoma kuachia majimbo yote mawili zaidi wenyewe walikua wanataka jimbo la mh. Devid silinde ambalo ndio lenye vyanzo vingi vya mapato ikiwa pamoja na kastamu. Lakini kulingana na ujasiri wa vijana wa tunduma walishindwa kuchakachua maana damu ingemwagika vibaya sana hivyo wakaona bora wachukue hilo la zambi..na sidhani kama tokea achaguliwe amewai kukanyaga jimboni kwake aliapa kwamba hawezi kurudi baada ya wananchi wenye hasira kuvamia nyumba yake.
   
 10. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Pamoja na hayo Zambi anatumia nafasi yake ya ubunge kuwalinda wafanyabiashara wadanganyifu wa bei za kahawa wanaowanyonya wakulima wa kahawa Mbozi. Mtakumbuka kuna kampuni la Lima linalolipa bei nzuri, linapigwa vita na Zambi lisinunue kahawa ya wakulima Mbozi.
   
 11. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,592
  Likes Received: 1,676
  Trophy Points: 280
  Tatizo yule spika mama kiroboto anafunika sana nakumbuka hili liliripotiwa na kafulila na lileta balaa sana bungeni, sijuhi limeishia wapi lakini nakumbuka kulikuwa kuna uchunguzi unaendelea!
   
 12. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Je wananchi wa Mbozi wanaujua huu ukweli? Lakini ni kwa vipi yule mgombea wa CHADEMA hakuamua kufungua kesi ya kupinga matokeo?
   
 13. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Ni ukweli usiopingika kwamba Zambi amenunuliwa na wafanyabiashara malaghai wa kahawa wa Mbozi ndiyo maana watu Mbozi hawakumchagua kuwa mbunge wao uchaguzi wa 2010. Mfano ni kwamba kabla ya mambo kupoa kule Mbozi, Zambi alikuwa huru kutembelea kijiji cha Ichesa tu kwa bwana Ugali mnunuzi laghai wakahawa.
   
 14. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,544
  Likes Received: 10,475
  Trophy Points: 280
  maneno ya mtaani yanasema kuna namna ilifanyika.lakini ukweli anaujua mgombea mwenyewe wa chadema.
   
 15. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  He?! Sasa ndo uongozi gani huo wa kufosi! Hili tatizo la ajila jamaani?
  Si atafute tu kazi ingine ya kufanya. Em fikiri hata wewe...watu unaotakiwa kuwaongozi unajificha wasikuone.
  Halaf ndo huyo Kikwete anataka kumpa uwaziri? Mbona hii kama haijakaa vizuri.
   
 16. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Wao Wana Magamba sisi tuna Mungu Mkuu.
   
 17. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #17
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  Ndyali ee,

  hivi Ichesa pana significance gani katika jimbo,
  kufanikisha ufadhili wa mtu hatakiwi kwingine kote?

  Mbona ni kama nasikia mtetezi hasa wa zambi
  ni mji wa Mloo na Vwawa?
   
 18. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mkuu Idawa, kiukweli baada ya mambo kupoa angalau ngalau anapita lakini kwa mawenge mawenge kama mbwa mwizi hasa kwa kutumia gali ya bwana ugali
   
 19. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mkuu, kijiji cha ichesa pekee waliompigia kura nyingi Zambi kwa shinikizo lamwenyekiti wa kijiji ambaye ni tajili sana kijijini hapo bwana ugali au Fuata upotee, akiwa pia ni mwenyekiti wa kijiji hicho huwadhibu wafuasi wa vya upinzani kwa kuwanyima mbolea za ruzu. Mlowo unpopasema waliwahi kuvunja vioo vya gali la Zambi alimanusra yeye hakuwemo ndani ya gali hilo bali dereva wake. Vwawa walimvunjia nyumba vioo vyote na thani za ndani
   
 20. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Du. Maneno hayo!
   
Loading...