Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Godbless Lema, Mbunge anayeongoza kwa utoro bungeni.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless, akiongea na Mwananchi juu ya kutajwa na Spika kwa kuongoza kuwa na mahudhurio hafifu bungeni; amedai kuwa hahudhurii vikao vya Bunge kwa sababu ya kutofautiana na Wabunge wa CCM katika majukumu ya kisiasa: "Pengine Wabunge wa CCM wanaweza kuwa na mahudhurio mazuri sana kuliko sisi Wapinzani kwa sababu tunatofautiana majukumu kisiasa katika ujenzi wa Taifa letu."
Jana Spika wa Bunge, Job Ndugai alimtaja Lema kuwa ndiye Mbunge anayeongoza kwa utoro bungeni, akizidiwa tu na Waziri wa Mambo ya Nje, Dk. Mahiga. Lema amehudhuria vikao vya Bunge kwa asilimia 7.8%.
Kulingana na Spika, top ten ya Wabunge (sio Mawaziri) wasiohudhuria bungeni, imetawaliwa na Wabunge wenye asili ya Kiasia, huku Wabongo pekee wakiwa Godbless Lema, David Mathayo na John Mnyika (wote wakiwa wazee wa Kaskazini).
Wabunge walioongoza kwa mahudhurio mazuri bungeni na ambao hawajawahi kukosa Kikao, wote wanatoka CCM nao ni: Justin Monko (Singida Kaskazini); Felister Bura (Viti Maalum) na Omary Kigua (Kilindi). Waliohudhuria kwa asilimia 99% wako Sita na wote wanatoka CCM.
Hali hiyo inashangaza sana ukifikiria jinsi ambavyo Wabunge wa Upinzani wamekuwa wakijitanabaisha kuwa wanawatetea wananchi. Sasa, inakuwaje wanawatetea wananchi wakati hawahudhurii hata vikao vya Bunge?
Je, Lema naye ana biashara gani za kumfanya awe na shughuli ya kupotezea midalali ya kila siku wanayopokea Wabunge?