barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,726
- 32,818
Mbunge wa Arusha Godbless Lema ameunguruma toka Nairobi,anasema anashangazwa na Spika Ndugai kutokutoa ushirikiano wa matibabu ya Mbunge Lissu kwa gharama za bunge na serikali kama yeye alivyotibiwa India kwa miezi mingi alivyokuwa anaumwa.
Mh.Lema anasema,Spika Ndugai wakati wa ugonjwa wake,haukufanyika mchango wa wabunge kama ule wa send off,bali bunge na serikali vilitoa pesa kwa ajili ya matiabu yake,lakini kwa Mh.Lissu,Spika Ndugai ameishia kuchangisha tu pesa na hakuna juhudi za bunge wala serikali kusaidia gharama za Lissu kama wabunge wengine.Idadi ya mapigo ya risasi,haikuhitaji watu kujiuliza juu ya matibabu nje ya nchi.
M.Lema anashangaa kwanini Lissu hakupewa ulinzi wa polisi wakati alishatoa taarifa za kufuatiliwa?Wakati ugomvi wa Juliana Shonza bungeni unafanya mpaka sasa ate,bee na asakri wa ulinzi aliopewa na Spika?
Lema anasema atarudi nyumbani na kufunguka,watu wanazungukazunguka,lakini yeye atasema moja kwa moja.Amemkumbusha Spika juu ya ugonjwa wake,na kumwambia hapa duniani na pa kupita,hata kama serikali ndio iligharamia matibabu yake India,basi asijipendekeze sana kiasi anasahau utu na ubinadamu.Mh.Lema anashangaa,inakuwaje tofauti ya idadi ya risasi anazotaja Ndugai na Mh.Kubenea,isababishe Kubenea kuitwa kwenye Kamati ya Bunge ya Maadili?