Godbless Lema: Pesa aliyolipwa Bilionea Laizer ni pungufu sana, ungefanyika mnada angelipata karibia mara kumi ya alicholipwa

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,680
22,685
Pesa iliyo lipwa kwa madini ya Tanzanite kilo 9.27 na kilo 5.8 iliyo ungana ni pesa kidogo sana, kelele na mbwembwe zitapata sifa kwa wasio elewa. Haya madini ya ukubwa huu kwa biashara ya kimkakati (Auction), yanaweza kulipwa pesa mara 10 ya hizi.

Ukitafakarimuda/gharama za uchimbaji zaweza kuwa nusu au thamani ya pesa anayo lipwa, Mh Dotto nachunguza hizi kelele zina maana gani?Uzalendo kwa sasa pelekeni hayo mawe mnadani jueni thamani kisha mpeni thamani halisi ya ushindani, halafu Serikali iyatumie kwa maonyesho.

Unique pieces kama hizi zilipaswa kushutua kwa bei, kwani thamani yake haipangwi kwa gramu isipokuwa upekee. Kuna rules katika biashara hizi, rules hizo hazihitaji Degree wala PHD isipokuwa Wall Street thinking, nani ataona value ya Tanzanite tena? Biashara sio kelele ni strategy.

Unique pieces kama hizi bei zake hazipangwi kwa gramu isipokuwa upekee. Kuna rules katika biashara hizi, rules hizo hazihitaji Degree /PHD isipokuwa Wall Street thinking. Nani ataona thamani ya Tanzanite kwa kilo 9.27/ 5.28 kuuzwa sawa na saa ya Mike Tyson? na mnunuzi ni Serikali?

Kwa kukosa uelewa mmeshusha thamani ya Tanzanite kwa hali ya juu sana, piece ya kilo 9.27 na 5.28 ni unique pieces ambazo kwa bei mnayo pigia kelele sio zaidi ya USD 3.5 milioni. Najiuliza sasa ni pieces gani nyingine zitapata thamani kuonyesha upekee wa madini haya?
 
Biashara ni makubaliano, BOT/Serikali wamewekeza mtaji wao lazima faida itapatikana ili hii nchi ifaidike kuendelea kuleta maendeleo yenye tija kwa Watanzania.

BTW Lema amekuwa mtaalam wa madini, mbona hakusema bei yake basi tufahamu na kutueleza hiyo bei ni pungufu kwa kiasi gani? Ndio majungu yenyewe na Propaganda hizo.
 
Back
Top Bottom