Godbless Lema: Naipinga serikali kwa kuwakopesha wabunge pesa za kununulia magari ya kifahari

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (CHADEMA) amesema fedha alizokopeshwa na serikali kwa ajili ya kununulia gari atazitumia kuanzisha taasisi ya kukopesha wanawake ili kuwawezesha kuinuka kiuchumi.

Aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wananchi waliojitokeza kujiandikisha majina kwa ajili ya safari ya kwenda kupatiwa tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile, katika Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale, Loliondo, mkoani Arusha.

Alisema ataanzisha taasisi hiyo hivi karibuni kwa kiasi cha shilingi milioni 50 kati ya 90 alizopewa na serikali kwa ajili ya kununulia gari.

Mbunge huyo wa Arusha Mjini alikuwa mbunge wa kwanza kutamka na kupinga hadharani hatua ya serikali kuwapa wabunge kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kununulia magari huku ikishindwa kuwapatia wananchi mahitaji muhimu kama magari ya kubebea wagonjwa hospitalini ambako serikali imetoa Bajaj kwa ajili hiyo.

Akizungumzia hatua yake ya kuwasaidia wananchi wake kufika kupata dawa kwa "Babu" alisema kuwa suala hilo ni la imani, hivyo baada ya kuona wananchi wanaamini wakienda kule wanapona ila hawana uwezo wa kifedha ndipo akaona ni vema awawezeshe kufika huko.

Lema aliwaomba na watu wengine wenye uwezo kujitokeza kuwasaidia wananchi hao ambao walikuwa wamejitokeza kwa wingi kujiandikisha mbele ya jengo la ofisi za mkuu wa wilaya zilipo ofisi za mbunge huyo ili waweze kwenda Loliondo ambapo alisema kuwa kipaumbele ni watoto na wagonjwa, hasa wenye vyeti vinavyothibitisha ni wagonjwa.

"Matajiri mnaweza kusaidia hili ni suala ni la kibinadamu zaidi, changieni wananchi kufika Loliondo kwa babu kupata "kikombe" mnaweza hata kupunguza idadi ya viwango vya bia mnavyotumia kwa siku, tukashirikiana kuwawezesha ndugu zetu wakatibiwe".

Nauli ya kufika Loliondo kwa babu kwa kutumia magari aina ya Land Cruizer ni wastani wa kati ya shilingi 100,000 na 150,000 huku nauli ya mabasi ikiwa wastani wa shilingi 30,000 na 70,000 ambapo hata hivyo bado watu wengi wanaonekana wakipanda magari kuelekea huko.

CHANZO:Tanzania Daima.( 17/03/2011)
 
Historia ni mwalimu mzuri.

Sifa moja ya viongozi walaghai ni kutokuogopa/aibu ya kula matapishi yao ya kisiasa.

Tukiangalia nyuma tunaona makosa mengi tumetafanya mojawapo ni kulaghaiwa na wanasiasa wanaotumia siasa kama biashara.

Nature itapambana na vyama vilivyojengwa kwa misingi ya kilaghai ndiyo maana CHADEMA kwa sasa kinahangaika na nature.

Mpanda ngazi hushuka na hata chama cha kilaghai hakita kuwa na uwezo wa kuhimili nguvu za ukweli.

Historia haitaishia kwenye mnara wa Babeli peke yake bali hata kwa viongozi walaghai kama ukweli unavyotamalaki kila siku.

Tukisema CHADEMA imejengwa kwa misingi ya kilaghai kupitia viongozi wake kama Godbless Lema kuna watu hawatuelewi.

Mwenyezi Mungu ana ufunuo wake. Mwenyezi Mungu ameanza kuwafunulia pia wananchi wengine ili watambue true colour ya hawa matapeli wanaojiita wakombozi kupitia CHADEMA.

CHADEMA siyo chama cha siasa ndani ya demokrasia kwa manufaa ya demokrasia bali ni private-owned enterprise through political project.

Chama kilichojengwa kwa misingi ya kilaghai hata uendeshaji wake utakuwa niwa kilaghai.

Mwl. Nyerere alishawahi kusema, mtu akikuambia upumbavu na anajua anachosema ni upumbavu na wewe ukakubali huo upumbavu basi atakudharau kwa maana hiyo, inawezekana huyu mwanasiasa anawadharau sana wapiga kura wake wa Arusha.
 
Mbona hiki chanzo kama kimechacha hivi mwaka 2011 dah?Enzi hizo dola 1 sawa na 1400 tsh.
Ila lema ameongea sorry aliongea la msingi.
 
Sasa yameanza kujikopesha baada ya kukwiba na kumaliza rasilimali zote za taifa hili, yaani hii mi-ccm hii ***##** kabisa!
 
Huu mtindo uliozuka wa UTETEZI wa CCM unaonesha kitu kimoja tu KWAMBA CCM IMEFIKIA UKOMO WA KUFIKIRI. CCM wakishauriwa wapunguze matumizi kwa kutonunua magari ya kifahari UTETEZI wao mbona KUB naye anatumia gari la kifahari. CCM wakishauriwa waboreshe huduma za Afya baada ya kutumia mabilioni ya pesa kutibia viongozi wa kitaifa nje. UTETEZI wao mbona hata Wabunge wa upinzani wanatibiwa huko nje. CCM wakishauriwa waboreshe Elimu ili Watanzania wapate elimu bora. UTETEZI wa mbona hata watoto wa Mbowe na Lissu wanasoma nje. Jamani hivi kweli haya yanaweza kuwa maelezo ya chama tawala chenye maono ya kuwaongoza Watanzania? Be the juror yourself.
 
Mmmh,
Lema anahamasisha tena watu kwenda huko huko kwa babu;
Kweli hii nchi ina watu na vituko.
Wanasiasa kama Godbless Lema ndiyo think tank ya iliyokuwa CHADEMA ambayo kwa sasa imejificha kwenye kikundi cha UKAWA kuepuka maswali ya ndani ya chama kuhusu zoezi la uchaguzi wa viongozi wa chama.

Kile anachokisema leo anakitenda kesho kinyume chake.
 
Huu mtindo uliozuka wa UTETEZI wa CCM unaonesha kitu kimoja tu KWAMBA CCM IMEFIKIA UKOMO WA KUFIKIRI. CCM wakishauriwa wapunguze matumizi kwa kutonunua magari ya kifahari UTETEZI wao mbona KUB naye anatumia gari la kifahari. CCM wakishauriwa waboreshe huduma za Afya baada ya kutumia mabilioni ya pesa kutibia viongozi wa kitaifa nje. UTETEZI wao mbona hata Wabunge wa upinzani wanatibiwa huko nje. CCM wakishauriwa waboreshe Elimu ili Watanzania wapate elimu bora. UTETEZI wa mbona hata watoto wa Mbowe na Lissu wanasoma nje. Jamani hivi kweli haya yanaweza kuwa maelezo ya chama tawala chenye maono ya kuwaongoza Watanzania? Be the juror yourself.
Je, huu ushauri wake ameufanyia kazi?.
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (CHADEMA) amesema fedha alizokopeshwa na serikali kwa ajili ya kununulia gari atazitumia kuanzisha taasisi ya kukopesha wanawake ili kuwawezesha kuinuka kiuchumi.

Alisema ataanzisha taasisi hiyo hivi karibuni kwa kiasi cha shilingi milioni 50 kati ya 90 alizopewa na serikali kwa ajili ya kununulia gari.
 
Hivi kweli inakuja akilini kama inasemekana aliwahi kuwa jambazi na kuua watu kwa ajili ya pesa leo atoe kusaidia jamii?

Huu ni ule muendelezo wa ulevi wa kutafuta kiki ya kupatia umaarufu hasa kwa wanasiasa wa kariba ya lema ambao mungu kawajalia vichwa vikubwa akawapa ubongo mdogo kwa ajili ya kutembelea tu
 
Halafu wewemlaghai na mzandiki Mwana diwani kuja hapa utueleze Ulaghai wa mwenyekiti wako ambaye mnamwita Rais kutudanganya wananchi kwa maelfu eti atatuletea maisha bora kwa kila mtanzania Maisha hayo bora yako wapi gamba wewe

Mnabaki kuweweseka na kamanda Lema kanakwamba mkimwandama Lema ndo ilani yenu MFU itatekelezeka kaeni kimya sisi tunajua tulicho ahidiwa na kipi tulucholaghaiwa na mlaghai wetu tunamjua, tutakutana 2015 kwenye sanduku la kura

BACK TANGANYIKA
 
Je, huu ushauri wake ameufanyia kazi?.

MwanaDiwani: I know wewe una punje ya reasoning sio kama akina MSALANI, LIZABONI, ABAKORAKAMO etc, ndio maana huwa sijisumbui kabisa kuwajibu achilia mbali kusoma threads zao. CCM imechaguliwa na Watanzania against other political parties, kwasababu Watanzania wana/walifikiri kwamba CCM ina cha ZAIDI kuliko vyama vya UPINZANI. Tatizo ni pale ambapo sasa CCM imeifanya CHADEMA kama YARD STICK yake. Kama YARD STICK YA CCM ni CHADEMA kwanini basi Watanzania waendelea kuichagua CCM? Si bora wachukue yard stick yenyewe. Make no mistake two wrongs do not make a right. Huu UTETEZI wa CCM kwamba ni halali CCM kufanya makosa kwakuwa CDM nao wanafanya ni UTETEZI wa chama ambacho kimefikia ukomo wa KUFIKIRI!
 
Ndugu Bobuk,

Hakuna kauli yoyote ya CCM kama chama inayojenga mazingira yanayoakisi kuwa, CHADEMA ndiyo kipimio cha siasa za CCM.

Kauli za mwanaCCM haziwezi kuwa ndiyo kauli za chama, vivyo hivyo, utendaji wa mwanaCCM haina maana kuwa huo ndiyo utendaji wa CCM.

Chama tawala hakiruhusiwi na mazingira kutenda kwa kutumia akisi la vyama vya upinzani kwa sababu wapinzani wamesimama kwenye siasa za maandishi ( theoretical) wakati CCM inafanya siasa za kutenda ( practical).
 
Lema anatakiwa kwanza akamilishe ahadi zake za kujenga Machinga Complex na Hospital ya kina mama.
 
Ccm hawana jipya ni kusubiri kulimwa kadi nyekundu2015
Ndugu, huu ni mtazamo wako lakini kumbukumbu za chaguzi ndogo za Udiwani na pia ubunge wa Kalenga na Chalinze hivi karibuni zinatueleza na kutoa angalizo tofauti na mtazamo wako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom