Godbless Lema na John Mrema wameizungumzia vizuri sana hii ishu ya Mikopo na Ndugai

Ukiangalia wanasiasa wetu nao wa ovyo ovyo kabisa! Hata Chadema kwanini mlimfukuza Dr Slaa na kumweka Lowassa?
Yaani nyie ndo tatizo haswa maana hamna misingi endelevu imara ya kichama,
Yaani leo hii Ndugai manesema ni tatizo akisema nahamia Chadema, ni dhahiri shahiri mnampa urais!
 
Watu hawajamuelewa ndugai,
Mi nafikiri alimaanisha kwamba,
Hatuwezi kuepuka kukopa,kwa sababu nchi Haina mapato ya kujitosheleza,
Na serikali ilipojaribu kuleta tozo Ili kupunguza ukopaji,bunge ilibidi lipitishe kwa sababu "deni "la Taifa linatisha na wakiamua kuendelea kukopa bila kutafuta njia mbadala za mapato,nchi itapigwa mnada hii

Aliongea lugha ambayo unadhani tunapata shida kuielewa hadi utueleweshe alichomaanisha?
 
Kwa akili zako hizi hautoshi kujua uwezo wa Ndugai. Mtu ambae hata huelewi kanuni za msingi za kiuandishi unawezaje kumpima Ndugai?


Ni kweli ulichosema kuhusu uandishi wa huyo mdau, lakini Ndugai hana akili hizo, ndio maana anatumia nguvu nyingi kuliko akili. Kwa bahati mbaya unadhani Ndugai ana akili sana maana ni spika. Ingekuwa hilo bunge linajitambua, mtu kama Ndugai sio tu kuwa spika, bali hata kuwa mbunge ni aibu.
 
Ssh haijengi Dom kwafujo hata hapendi kukaa hiyo kitu inamchoma ndugyai...pia alitamani yeye apewe kiti baada ya msiba lakini wapi!!! Ameanza kubutua mipira hovyo
 
Watu hawajamuelewa ndugai,
Mi nafikiri alimaanisha kwamba,
Hatuwezi kuepuka kukopa,kwa sababu nchi Haina mapato ya kujitosheleza,
Na serikali ilipojaribu kuleta tozo Ili kupunguza ukopaji,bunge ilibidi lipitishe kwa sababu "deni "la Taifa linatisha na wakiamua kuendelea kukopa bila kutafuta njia mbadala za mapato,nchi itapigwa mnada hii
Very good point,na hiyo ndiyo maana halisi ya maneno ya mzee Ndugai.Sisi tunao kwenda mbele zaidi ya hayo, ni udadavuzi batili.
 
Hoja ya John Mrema naona ndio ina mashiko, ya Lema ina mapengo.

Lema anataka Samia asaidiwe kwenye vita yake na Ndugai kwa nini? kwamba Lema anapendezwa na nchi inavyozidi kukopa kila siku?

Lema asitumie udhaifu wa Ndugai kwenye masuala mengine kama sababu ya kumuunga mkono anayekosea sasa, kukopa sio sifa.

Tuliambiwa tozo zitajenga madarasa, iweje waende nje tena wakachukue mkopo wa kujenga madarasa? haya ndio mazoea Ndugai anayoyakataa.

Nashangaa pamoja na madhaifu yote ya serikali ya CCM chini ya Samia aliyoorodhesha Lema, bado anamuunga mkono Samia dhidi ya Ndugai, naona hizi ni siasa za kujipendekeza.

Tanzania kuna wapinzani uchwara sana, ndio maana wanaendeshwa sana na matukio kesho likitokea jingine tu utawaona wanavyo dandia.

Hawaeleweki ajenda yao hasa ninini, nahizi ni dalili za kukwama, sasa wanaangalia namna yoyote ya kujipendekeza tu ili wapate tension kwa mama.
 
Tatizo la ndugai ,uwezo wake ni mdogo sana alifika pale kwa bahati,alitakiwa kufanya kazi huko mbugani kulinda viboko na tembo na sio kuongoza watu
Haya mambo huwa tunasema ONLY IN TANZANIA!
Ndugai kasomea taaluma ya kusimamia Wanyama Pori pale MWIKA WILDLIFE MANAGEMENT.....Leo unampa kazi ya HUMAN RESOURCES MANAGEMENT....wapi na wapi?? Ndiyo maana WABUNGE WOTE iwe upinzani au CCM anawa treat kama Wanyama......Nonsense!
 
Anaandika Godless Lema:

“Tofauti yetu kubwa na Mh Rais SSH iko ktk madai ya Uhuru wa Kisiasa, Demokrasia, Katiba mpya na Haki za Wafungwa wa Kisiasa akiwemo Mkti Mbowe. Lakini kama kuna ugomvi kati ya Job Ndugai na Rais SSH , bila shaka anayepaswa kusaidiwa ni SSH. Ndugai ni mzigo mzito sana katika Nchi.”

Anaandika Jon Mrema:

“Huyu ni Spika wa Bunge,ambaye analalamika wakati Bunge linatakiwa kuisimamia Serikali, anasema nchi itapigwa mnada Kwa sababu ya deni kubwa la Taifa. Kuna hoja iliwahi kutolewa Bungeni kuwa CAG afanye ukaguzi Maalum juu ya deni la Taifa kwanini asikubaliane na hoja hiyo? Gang!!!!”

Akili kubwa kubwa hizi, Shida kubwa anayopata Samia ni kuongoza watu wengi wenye upeo mdogo wa kufikiri ambao wamejaa ndani ya Chama chake anachokiongoza.
Na sio tuu ndani ya chama chake bali sehemu kubwa ya jamii ya Tzn ina watu wenye akili kisoda kabisa.
 
Back
Top Bottom