Godbless Lema: Mrisho Gambo(RC) hakuogopa kuwa muongo madhabauni eti aliniita mimi rafiki yake

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Ktk Ibada ya kusimikwa Askofu,Mh Rais aliongea neno la Mungu kuhusu Amani na Haki.Bila shaka demokrasia na haki vitashamiri tena.Askofu Amani yeye akasisitiza ushirikiano kisiasa bila kubaguana.Mrisho Gambo(RC) yeye akuogopa kuwa muongo madhabauni, eti aliniita Mimi rafiki yake.

lema.jpg
 
Hawa ni wataalamu wa kupindisha ukweli
CUF haijawahi kushinda uchaguzi Zanzibar
Nondo alijiteka
Mhariri wa Guardian alilewa
Tundu Lissu amepigwa risasi na watu wasiojulikana lakini ni marufuku kuwasomea albadir
Mara zote nikiona comments zako lazima nikupe salute kimya kimya.........
 
Ni Huyu Huyu Lema hivi karibuni alitaka Wanasiasa wa Arusha kurudisha uhusiano ili kujenga Ushirikiano Na Maendeleo!

Kuitwa Rafiki ni neno la kawaida sana Kwa busara ya kiwango cha chini sana alipaswa kuchukulia kawaida hasa Kwa Wanasiasa
 
Chadema bado wachanga sana kisiasa.
Hakuna uchanga kwenye kuuwana,hakuna uchanga kwenye kumuweka ndani mtu miezi sita bila dhamana wakati kosa linadhaminika,kukaa miezi hiyo sita mahabusu sbabu ya tofauti za kisiasa ni sawa na kifungo.

Ukomavu unaousema huo wewe ni upi?Unataka ukomavu wa kinafiki wa kukimbia na masanduku ya kura?Unataka ukomavu huo wa kuwinda wenzako na SMG kama digidigi?Jana yake tu Gambo mbele ya Rais kwenye uwanja wa mpira ametoka kumnanga Lema,halafu kesho yake anasema rafiki na unataka Lema akubali??Wacha unafiki wewe

Unakuwa rafiki unanunua madiwani na kuleta fitna ktk jimbo?Unakuwa rafiki unasema unataka uufute upinzani mkoa wa Arusha kwa namna yoyote ile?Hizo mnazosema siasa za kistarabu mbona nyie hamuwi wa kwanza kuzitenda??

Safi sana Lema,hujawa mnafiki,tunakumbuka jinsi Gambo alivyotaka kuharibu mchango wako kwenye uzinduzi wa Hopsital ya Mama na Mtoto,tunakumbuka maelekezo yake ili unyimwe dhamana,sasa huyo kwanini aseme uongo mbele ya madhabahu kuwa wewe ni rafiki yake?
 
Kuna mambo yanachekesha sana bahati mbaya siwez cheka maana nina wasiwasi my name leo haiwez kosekana kwa naibu .....
 
Hawa ni wataalamu wa kupindisha ukweli
CUF haijawahi kushinda uchaguzi Zanzibar
Nondo alijiteka
Mhariri wa Guardian alilewa
Tundu Lissu amepigwa risasi na watu wasiojulikana lakini ni marufuku kuwasomea albadir
 
Lema always ni mtu wa kulalamika. Iwe kwa baya au kwa zuri. Ingependeza amuone mtaalam wa maswala ya saikolojia.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom