Godbless Lema: Kuna siku mtavililia vyama vya Upinzani viwasemee hamtavipata

Chadema hii ya sasa IFE tu, hamna atakayeililia. Kwanza ndio watanzania tutasherehekea kifo cha upinzani feki.

Watu walipania CHADEMA wakidhani inawatetea, ghafal bin ghafla 2015 wanakabadili gia angani na kugawana noti. Leo Lema bila haya anaongelea CHADEMA wakati anajua moyoni alivyocheza dili. Nakusalimu Dr Slaa.
 
Lema amesahau wakati kukiwa na chama kimoja kulikuwa na majaribio takribani nane ya kupindua serikali ?

Hata wote leo mkihamia ccm bado watakuwepo tu wengine wasio penda upuuzi na watafanya jambo

Ila upande mwingine Watanzania sijui ni upole au ujinga ndio umetujaa kuna vitu tunaburuzwa tu na hatufanyi lolote

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo ndilo analojaribu kukumbusha Lema.
 
Lema, upinzani mmeudhoofisha wenyewe. Haya yote ni matokeo ya 2015. Mlikula yamini lakini itawatafuna hadi mtubu na kuanza uelekeo mpya. Tulisalitiana kishamba mno na mnafikiri ile dhambi itafutika kirahisi.

Mnakumbuka ule "utafiti" wenu kabla ya kumpokea EL mliokuwa mnautumia kumchinja Dr Slaa? Hivi mnafikiri zile issue zinakufa kirahisi tu?

Bora ujengwe upya upinzani imara hata kama itagharimu miaka 50 ijayo kuliko huu wa sasa ambao hata sasa bado mnavizia makapi ya MaCCM yagombee kupitia chama chenu. Badilikeni nyie kwanza kabla ya kuisema CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nani kakudanganya upinzani umedhoofika.
 
Kabla ya vyama vingi,kulijuwa na majaribio 8 ya kuipindua serikali(kuasi)!Baada ya mfumo wa vyama vingi hakuna hata jaribio moja ambalo limewahi kutokea la kuipindua serikali!
Fikiri ukiwa umezirudisha akili kichwani kutoka mfukoni ulipoziweka!
Hata hili hatalielewa!!
 
Nyerere ndiye mwanzilishi wa chama kimoja na ndiye aliyelazamisha ccm kukubali vyama vingi. Alifanya hivyo kwa kuona mbali. Alishabaini kuwa chama kimoja ni janga kubwa. Watu walijimilikisha ccm na kuitumia kwa maslahi yao binafsi. Wakati wa tume ya Nyalali alishuhudia pia nguvu kubwa iliyotumiwa kufanya asilimia ya wananchi wasiotaka vyama vingi ionekane kubwa! Watu walisafirishwa kwa malori kwenda kutoa maoni ya kukataa vyama vingi. Haya yote ni kinyume na maono yake. Nyerere akaona salama ya Watanzania ni vyama vingi. Leo hii angekuwa hai hakuna mtu hata mmoja angewazia huu ujima unaoendelea sasa.
 
Heshima kubwa sana kwa haya maneno kuntu kutoka kwa mh Lema kiongozi wa watu
Anaandika GODBLESS J. LEMA (MB) Arusha

Vuta Picha Vyama vyote vikafutwa katika kipindi hiki kikabaki CCM tu chama ulichonacho wewe.

Then hao uliokua unawaona hawafai akina Mbowe, Mdee, Heche, Nassary, Lema n.k wakaona ni UJINGA KUFA unatetea watu wasiojua kujisaidia wenyewe. Wakajiuliza Kwani tunakwama wapi? Acha na sisi tukaungane na CCM mtesi wao na sisi tuishi vizuri tu.

Then Wabunge wote katika Majimbo yote wakatokea CCM kila kitu kikaamuliwa ndani ya Chama.

Mbowe akasaidiwa kujenga Bilcanas mpya maisha yakaendelea kama tunavyoona watu wanasamehewa kubomolewa nyumba zao wakijiunga na CCM.

Mbowe, Mnyika, Lijualikali tayari wanatambulika na system ya Uongozi hapa nchini. Kama DC wa Dodoma anaejitambua kama karai amepata vipi hawa wenye makarai yao watakosa?

Then fikiria wewe Mtanzania wa kawaida utaishije na atakusaidia nani tena kuhoja kuhusu pesa yako?

Kama walipokuwepo watu wa kuhoji pesa yako bado walikua watu wanakula kwa kujificha japo kweli zinaliwa. Vipi wakikosekana?

Hivi mshawahi kufikiria madhara ya hizi Juhudi za Kudhoofisha Upinzani au huwa mnashangilia tu?

Mtaishi kama "Mbwa Koko" na hutatambulika tena kama mfuasi wa CCM watatambuana viongozi kwa viongozi. Who is going to deal with you?

Leo Viongozi wa CCM wanawanyenyekea kidogo wananchi ni kwa sababu wanajua kuna Uchaguzi awamu ijayo.... Na Pengine Jimbo likaenda Upinzani. Ikibaki CCM pekeake nani atakunyenyekea wewe? Nani atakuja kujua hata unaishije?

Mshafikiria?

Hamtamuona Polepole tena! Anakuja kueneza nini? Watakua ofisini tu wakilipana mishahara. Watawachagulia kila kitu na hakuna cha kuwafanya.

Mshafikiria?

Ni ngumu kuelewa kwa kuwa haijatokea na mnaangalia leo tu.

Huwa natamani hii hali itokee hata kwa muda wa mwezi mmoja tu.

Mtakopwa hadi mishahara mtasema wapi? Nani atawapigania kipindi hicho hata kina Lissu wanakula mema ya nchi tu.

Hicho ndo kipindi hata ajira mpya kuna zingine itabidi wapate kwanza watoto wa viongozi na wengine mtapata zitakazobakia.

Hicho ndo kipindi mtapigwa hadi fimbo makazini, nadhani Dalili za Makofi zimeanza na hakuna wa kuwatetea.... Ukienda kushtaki makahamani unawakuta wale wale. Unapeleka kesi na unafungwa wewe. Wa kupiga kelele itakua ni familia yako tu wengine wote wanaogopa.

Akina Mbowe kipindi hicho watakua wanakula kuku kwa mirija tu.

Mtawaita na hawataitika tena. Ipo sababu kubwa sana ya Kuilinda Demokrasia na vyama Vya Upinzani. Walioianzisha na Kuitetea kwa Damu hawakua wajinga they focused on their future.

Hatubembelezani hapa kuilinda demokrasia ya kweli maana kesho ni yetu sote.

Kila Unachotaka kukishabikia kipime kwanza madhara yake ya baadae.

Watu mnatamani vyama vya Upinzani vyote vife au vifutwe ila ipo siku mtavililia na hamtavipata.

Tafakari

Siku njema

In God we Trust
 
Back
Top Bottom