Godbless Lema: Kuna mwingine atahama CHADEMA baada ya Meya wa Jiji la Arusha kuhamia CCM

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,974
Maneno hayo ameyaandika kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii baada ya aliyekuwa Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro kujiunga na CCM.

Calist Lazaro alikuwa rafiki wa karibu na Godbless Lema tokea wakiwa wote wanachama wa TLP kabla ya wote kuhamia CHADEMA.

Inasemekana Godbless Lema alifanya mbinu zote halali na haramu ili kuhakikisha rafiki yake anateuliwa na CHADEMA kuwa mgombea wa kiti cha Umeya wa Jiji la Arusha kupitia CHADEMA pamoja na kwamba alishindwa katika kura za maoni ndani ya CHADEMA.

Inasemekana walianza kutofautiana baada ya kuzidiana na kudhulumiana kwenye ''madili'' yatokanayo na uongozi wa Jiji. Hii inaonyesha urafiki wao wa karibu ulikuwa wa kimaslahi (tumbo) na sio kiitikadi na falsafa!

Maelezo ya Lema yanaonyesha kuna tatizo la kutoaminiana ndani ya CHADEMA!

Ni nani mwingine atafuata kuondoka CHADEMA baada ya Calist kujiunga CCM kama ambavyo Lema anabainisha?
Screenshot (3).png
 
Kiongozi au Mwanachama yeyote aliye makini atahama kutoka Chadema kwenda CCM.
Nyinyi wote ni watoto.. Historia ni mwalimu mzuri sana! KANU ya Kenya ilipokuwa madarakani, ilikuwa kama CCM inavyofanya sasa. KANU iko wapi leo! nani alidhani KANU ingelikufa? Hivyo hivyo chama cha Kaunda Zambia? UPC ya Obote iko wapi?etc, etc, etc. Unadhani leo CCM ikitoka madarakani kitatokea nini kwa "uthabiti" wa CCM, ! Nyinyi ni watoto hamsomi historia ya haya mambo!

CDM haina fedha, haina dola, haina polisi, haina jeshi, haifanyi mikutano, walafi wanahama , lakini bado inaogopwa. Unalisemaje hilo?
 
CCM ibadirike.
Ihangaike kuwapata wananchi watakaowapigia kura badala ya kuhangaika kuwapata viongozi waliopigiwa kura.
Kiongozi kama Lazaro hawezi kubadirisha mawazo yangu kwenye sanduku la kura ikiwa utendaji wa chama hicho haujakidhi mahitaji yangu ya kimaisha.
 
Sasa wewe akili yako iko wapi? Kama huoni lolote baya ndani ya CCM, mtaji wa akili yako nauwekea mashaka. kama umesikia kauli za Mkapa juu ya CCM , nadhani akili yako igelikuwa imeshakuwa mtaji!
Tafakuri kwa kila jambo hujenga nafsi, ila hamaki na mihemuko, hudhuru nafsi, na moyo hugubikwa na upofu. Wanayo heri walio wanyoofu, maana nafsi zao huishi zikinawili; kinyongo, gadhabu na fitina huwa mbali nao.
 
Nyinyi wote ni watoto.. Historia ni mwalimu mzuri sana! KANU ya Kenya ilipokuwa madarakani, ilikuwa kama CCM inavyofanya sasa. KANU iko wapi leo! nani alidhani KANU ingelikufa? hamsomi historia ya haya mambo!
Wasilinganishe KANU na CCM .KANU ilikuwa Chama Cha makabila makuu mwawili jamii za kijaluo na jamii za kikikuyu .walipogombana kila kabila likaamua kuanzisha chake.Wajaluo akina Raila odinga kwao na wakikuyu kwao.Kanu ikabakia na vikabila vidogo vya Kenya.

CCM sio Chama Cha Cha kikabila wasilinganishe na KANU

Chadema na KANU Haina tofauti wachaga wakijiondoa chadema inakufa
 
Tafakuri kwa kila jambo hujenga nafsi, ila hamaki na mihemuko, hudhuru nafsi, na moyo hugubikwa na upofu. Wanayo heri walio wanyoofu, maana nafsi zao huishi zikinawili; kinyongo, gadhabu na fitina huwa mbali nao.
Hizi quotations zako hazina objectivity ni viswahili masikini ambavyo wahaya hamna itikadi navyo, maana wahaya kiswahili si lugha yenu! Nawajua fika tena fika sana sana!
 
Wasilinganishe KANU na CCM .KANU ilikuwa Chama Cha makabila makuu mwawili jamii za kijaluo na jamii za kikikuyu .walipogombana kila kabila likaamua kuanzisha chake.Wajaluo akina Raila odinga kwao na wakikuyu kwao.Kanu ikabakia na vikabila vidogo vya Kenya.

CCM sio Chama Cha Cha kikabila wasilinganishe na KANU
Yehodaya unakosa objective analysis! Sasa makabila hayo yamekufa? The issue is KANU ilikuwa na "nguvu" kama CCM, kwanini ilikufa? Watu walifuata kula/njaa /maslahi mle, baada ya kula kuisha ikasambaratika. CDM hawana pesa, hawana Jeshi, hawana askari, hawana majumba, hawana magari ya kutanua/kustarehe, hawana magereza, hawaitwi waheshimiwa, hawafanyi miktano, wanafungwa kila leo, wanapigwa risasi etc, etc LAKINI BADO CCM inaiogopa CDM kufanya nao uchaguzi wa haki! Unafikiri ukiweka uwanja sawa, CCM itasimama? Jiwe anajua ndio maana nguvu zake zote ziko kuiua CDM na si TLP, CHAUMA, ACT and the like parties!
Have a nice day, it is time to shamba!
 
Hizi quotations zako hazina objectivity ni viswahili masikini ambavyo wahaya hamna itikadi navyo, maana wahaya kiswahili si lugha yenu! Nawajua fika tena fika sana sana!
Walau umetumia neno "quotations" nadhani ungetumia tuu neno "nukuu" maana sioni maana ya kandika vijineno vya wale wakati msamiati na istilahi za kiswahili vipo vya kutosha. Itoshe tuu kusema, ukikosa hoja utajibaraguza kwa kushambulia makabila, umbile, rangi, n.k

Ukisoma nilichoandika, hakuna nukuu bali mawazo na maono yangu, ila kwa upofu ulionao, hata neno la muhusika wewe hudhani ni nukuu (quotation kama ulivyoandika)
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom