Godbless Lema kuanza maombi ya kufunga na kuomba kwa siku saba

kwa wakristo huwa inakubalika kushirikisha watu wengine ktk maombi anayokuwa nayo mtu ili nao wamsaidie muhusika kuyapeleka mbele za Mwenyezi Mungu. hata hivyo kwa mujibu wa maandiko matakatifu yatupasa kuomba Mungu kwa shukrani na si kumuomba alipize kisasi. Haki mbinguni, duniani sheria. ni vema CDM wakaendelea na tamko lao la kukata rufaa, kwa utaratibu wa kawaida uliowekwa kwa mujibu wa sheria ili kupata haki yao kwa mujibu wa sheria.

Nadhani kuna kuteleza kidogo. Tunatakiwa tumuombe mungu ili mapenzi yake yatimie (na sio kulipiza kisasi). Kama mungu ataona inafaa sasa kuwazuia wale wote wanaosababisha maisha ya watanzania kuwa magumu basi kupitia sala tunatakiwa tumuombe aingilie kati kulingana na mapenzi. (baba yetu ...... utakalo lifanyike duniani kama mbinguni...)
 
wabunge ni viongozi wa wananchi wanapaswa kupima wanayoyasema.pili lema kwa kiwango cha uwezo wa akili yake ubunge ni cheo kikubwa mno,pengine chadema ifikirie kumpa udiwani,huwezi kumlinganisha na mjembe ya cdm kama zito,slaa,mnyika,nassarii,lissu etc.lema ni mzigo kwa cdm,hafai kuwa kiongozi

we unadhani Lema ni sawa na yule muimba tarabu wa bagamoyo ambaye anatfuna kodo zetu pale magogoni na kusubiria nani kafa ili akauze sura? Kazi ya Rais sio kulala matnga kwenye misiba 2 bali ni kusimamia rasilimali zetu zisitafunwe na wakina Hussein Gonga na lusinde.
 
Ni lazima Nape au Mwigulu waje humu watujibu hili swali,
hivi ni kwanini pro-ccm hamtaki kusikia neno Mungu? Kwa hali hii basi mtasema makanisa na misikiti ni CDM kwani wote wanataja Mungu.
KAMA PRO-CCM MMEANZA KUPIGANA VITA NA MUNGU! Basi hii ni kazi kweli kweli
 
MH LEMA jana alitangaza kuanza maombi ya kufunga na kuomba kwa siku saba kuanzia jumatano ya tarehe 11 April 2012 na kuomba kila mwananchi anayependa haki kwa imani yake kumuunga mkono katika maombi hayo ya kufunga na kuomba. Pia aliomba maombi hayo yaendane na kuwasaidia maskini na wajane na wale wasiojiweza kwa vile vitu ambavyo Mungu ametubariki kwavyo.

Lengo kuu la maombi hayo ni kumuomba Mungu aingilie kati na kulipiza kisasi kwa wale ambao wametumia nafasi zao kushinikiza hukumu isiyo ya haki ambayo ilitolewa hivi karibuni na kumfanya aende likizo katika nafasi yake ya ubunge na pia maombi ya shukrani kwa Mungu kwa yote yaliyotokea. Hayo aliyasema jana katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya NMC jijini Arusha.

Fikra za madenge
 
godbless lema wamekupa likizo ya lazima...nahisi kufulia kunakurabia..maana zile poshoposho zetu utazikosa na hilo prado tafadhali urudishe...ila usijali nitakupa Toyota Vitz utesee mtaani...unacheza na ubunge ww wakati maisha yenyewe mafupi.......nyooooo
 
MH LEMA jana alitangaza kuanza maombi ya kufunga na kuomba kwa siku saba kuanzia jumatano ya tarehe 11 April 2012 na kuomba kila mwananchi anayependa haki kwa imani yake kumuunga mkono katika maombi hayo ya kufunga na kuomba. Pia aliomba maombi hayo yaendane na kuwasaidia maskini na wajane na wale wasiojiweza kwa vile vitu ambavyo Mungu ametubariki kwavyo.

Lengo kuu la maombi hayo ni kumuomba Mungu aingilie kati na kulipiza kisasi kwa wale ambao wametumia nafasi zao kushinikiza hukumu isiyo ya haki ambayo ilitolewa hivi karibuni na kumfanya aende likizo katika nafasi yake ya ubunge na pia maombi ya shukrani kwa Mungu kwa yote yaliyotokea. Hayo aliyasema jana katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya NMC jijini Arusha.

Nahisi kucheka, huyu Mungu wetu kafanywa binamu siku hizi???? too late!
 
Kwani mbunge wa jimbo anahusikaje na ukabila.Wabunge wa CHADEMA wametokana na uwezo wao na siyo ukabila
 
Vipi hiyo funga itakwenda sambamba na maandamano au ndo paln B baada ya Plan A ya maandamano kushindwa?mungu mkubwa hivi white house ingekuwa uchagan si mngewatisha sana akina Jk!
 
Leo nimesali kanisa la Mikocheni 'B' Assembless of God,Dar Es Salaam.
Katika hali ya kustaajabisha kuna Mchungaji ameibiwa simu ya Blackberry baada ya kuisahau kidogo alipokuwa amekaa hivi majuzi.Sasa,ikaamuliwa waumini wafanye maombi ili aliyeiba arukwe akili!!
Sasa hapo ni kisasi?Hapana,si kisasi hata kidogo.Katika biblia,tunasoma kuwa Mungu alimpa adhabu ya kifo Anania baada ya kudanganya katika matoleo yake.
Nilitamani sana kumwomba Mchungaji aliyekuwa anaongoza sala hiyo aunganishe na hitaji langu nililonalo hadi sasa kuwa Mungu amshughulikie Jaji Rwakibarila mhusika ikiwa ametumia hila katika kufikia hukumu dhidi ya kamanda wangu Lema.Sikufanya hivyo,na kwa kweli nisingeweza kufanya hivyo maana sote tunajua Mikocheni 'B' inaongozwa na Mbunge,Dkt Mhe.Mch.wa CCM..
Hata hivyo nimeamua kuungana na Lema katika kumwomba Mungu ili amshughulikie Jaji ipasavyo.
 
Pro-ccm mnamapepo?mbona mkitajiwa Mungu mna mnapagawa au ndio mashetani yenu kama alivyosema Lukuvi pale kawe katika kanisa la Gwajima?
 
Back
Top Bottom