Godbless Lema kuanza maombi ya kufunga na kuomba kwa siku saba

MWINUKA E

Member
Feb 8, 2012
97
28
MH LEMA jana alitangaza kuanza maombi ya kufunga na kuomba kwa siku saba kuanzia jumatano ya tarehe 11 April 2012 na kuomba kila mwananchi anayependa haki kwa imani yake kumuunga mkono katika maombi hayo ya kufunga na kuomba. Pia aliomba maombi hayo yaendane na kuwasaidia maskini na wajane na wale wasiojiweza kwa vile vitu ambavyo Mungu ametubariki kwavyo.

Lengo kuu la maombi hayo ni kumuomba Mungu aingilie kati na kulipiza kisasi kwa wale ambao wametumia nafasi zao kushinikiza hukumu isiyo ya haki ambayo ilitolewa hivi karibuni na kumfanya aende likizo katika nafasi yake ya ubunge na pia maombi ya shukrani kwa Mungu kwa yote yaliyotokea. Hayo aliyasema jana katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya NMC jijini Arusha.
 
Hakika hii imetulia ili angalau haya mapepo ya kutokutenda haki yawatoke hawa watawala wetu.
 
Sasa ndio nimeamini chadema nichama cha udini pamoja na viongozi wao wote ,hiki chama nihatari sana maslahi ya taifa letu
 
Sasa ndio nimeamini chadema nichama cha udini pamoja na viongozi wao wote ,hiki chama nihatari sana maslahi ya taifa letu

Wewe ndo wa hatari sana usiye mjua na kumwamini mungu. Kufunga na kuomba ni kwa dini zote. Kiongozi mzuri na mkweli ni yule mwenye kumcha mungu. Huwezi kuibia nchi yako, kuingia mikataba mibovu kwa masrahi yako na huwezi kukandamiza demokrasia na uhuru wa watu wako kama wewe ni kiongozi mwenye utii wa mungu.
 
Acha unafiki hakuna dini ambayo haina maombi ya kufunga. Na alisema kila mtu afunge kwa imani ya dini yake. Hata freemason wenyewe wana maombi ya kufunga. We wa wapi?
 
Jamani mbona pro-ccm hampendi kusikia habari za Mungu? Au mna mapepo? Kwani ni dini gani isiyomjua mungu? Na kwani kufunga na kuomba ndio kosa na ni dini gani isiyofanya hivyo koz hata freemasons wenyewe na ushetani wao wanamjua mungu! KWELI CCM MMEFIKA PABAYA SANA KAMA NDO HIVI MKISIKIA MUNGU BASI MNAANZA KUTOKA POVU.
 
Yani kabisa,sio udini tu,ukabila pia.hawana busara kabisa hawa watu.wananchi wanatakiwa kuwa na umakini wa hali ya juu ktk kuchagua viongozi wao.mi kuna sehemu naenda nakuta kabisa wanaongea kichaga.utafikiri tanzania ni ya wachaga.
 
wakristo tumefundishwa kusamehe sasa sielewi ni Mungu gani atakayepokea hayo maombi ya kulipiza kisasi

Tumeibiwa kura za uraisi, ubunge, udiwani, ukitongoji, watu wetu wameuawa, wamebambikiwa kesi zisizo zao, wamehukumiwa na mahakama kwa makosa ambayo hawajayafanya, wanalazimisha dola ifanye vile wanavyotaka kulinda maslahi yao na kukandamiza upinzani halafu unatuambia tuwasamehe, HAPANA hili haliwezekani na wala halikubariki lazima tufunge tumwombe Mungu yeye akaaye mahali pa juu palipoinuka ataenda kutenda lile linalofaa kulingana na mapenzi yake.

Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi (Mathayo 5:44)
 
Yani kabisa,sio udini tu,ukabila pia.hawana busara kabisa hawa watu.wananchi wanatakiwa kuwa na umakini wa hali ya juu ktk kuchagua viongozi wao.mi kuna sehemu naenda nakuta kabisa wanaongea kichaga.utafikiri tanzania ni ya wachaga.

kweli ufinyu wa akili na mavi pia huchangia! Mbona mi sio mchaga lakini among wa makamnda wa CDM au na zitto naye ni mchaga?
Alafu naskia pro-ccm hamtaki kusikia neno MUNGU.?
 
Sasa ndio nimeamini chadema nichama cha udini pamoja na viongozi wao wote ,hiki chama nihatari sana maslahi ya taifa letu

Acha ushamba ww, udin uko wap hapo? Lema alisema kila m2 akaombe kwa iman yake, awe muislam au mkristo kwa yoyote atakayetaka kujiunga naye ktk mfungo huo anakaribishwa.
 
Mungu anisaidie sana nami niweze kufunga, pengine tunaweza kufanya uchaguzi mdogo wa raisi
Wee bwana pishilia mbali hayo. Unataka huku nako kuwa na ka Bingu wa Mutharika? Aisee!
 
Sasa ndio nimeamini chadema nichama cha udini pamoja na viongozi wao wote ,hiki chama nihatari sana maslahi ya taifa letu

We ndo Mdini kama hauna cha kuchangia c ukae kimya tatizo lenu magamba mkisia mambo yanahusu Mungu tu moto unaanza ukawaka kwenye mioyo yenu mnafki mkubwa wewe acha mambo ya ajabu bwana mtu mzima wewe unaongea kauli za kisenge kisenge!
 
maombi ni muhimu sana ila ni muhimu kuomba msamaha uliowakosea kwa kuwaza na kunena.eg matusi aliyomtukana batilda yalikuwa mazito sana kabla hajaanza kufunga akaungame,maana huku ar wakati wa kampeni kila mtu aliyasikia hayo matusi,tungefurahi kusikia lema akiungama kwanza
 
Yani kabisa,sio udini tu,ukabila pia.hawana busara kabisa hawa watu.wananchi wanatakiwa kuwa na umakini wa hali ya juu ktk kuchagua viongozi wao.mi kuna sehemu naenda nakuta kabisa wanaongea kichaga.utafikiri tanzania ni ya wachaga.

Mch.Msigwa mchaga? Wenje mchaga? Zitto mchaga?
 
Back
Top Bottom