Godbless Lema: Imebidi tumuondoe Zitto Kabwe usiku maana anafuatiliwa na watu tusiowajua

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema juzi Jumatano Februari 6, 2019 walilazimika kumuondoa mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe baada ya kufuatiliwa na watu ambao hakuwataja.

Akizungumza wakati akichangia taarifa ya kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria leo Ijumaa Februari 8, 2019, Lema amesema kama CCM wakitawala kwa haki, kwa kufuata sheria na Katiba hana tatizo hata wakitawala milele.

“Lengo letu ni kuwaona mnatutawala kwa haki na ndio maana ya upinzani lakini leo hii chuki inajengwa leo kiongozi mmoja M-NEC anasema Lissu (mbunge wa Singida Mashariki) akitua ashambuliwe,” amesema Lema.

“Leo mwenyekiti (Mussa Azzan Zungu), Zitto hayuko bungeni tumemuondoa juzi alikuwa anafuatiwa usiku kwa kazi za kibunge sio za kuuza madawa ya kulevya si za kubaka watoto ni kazi za kibunge.”

Akizungumza na Mwananchi alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Lema, Zitto amesema, “Tukio ni la kweli lakini mimi siwaogopi wafanye watakalo. Wabunge wenzangu Silinde (David-Momba) na Upendo Peneza (Viti Maalum Chadema) waliowatambua watu hao waliniondoa pamoja na Antony Komu (Moshi Vijijini) na kupelekwa mahala salama.”

Huku akizungumzia matukio yaliyowahi kumkuta ikiwa ni pamoja na kutaka kutekwa Lema amesema, “Leo hii kuna watu wanaozea mahabusu kwa kesi za utakatishaji fedha. Kenya kila kesi ina dhamana kasoro uhaini, Uganda hata uhaini una dhamana ni haki. Dhamana ni haki kuu katika katiba.”

Amewataka mawaziri na makatibu wakuu kujiandaa kwenda jela ama kubadilisha sheria ambazo zina upungufu.

“Mtafanya mtakachoweza kufanya, tunaweza tusirudi bungeni tena, mkasema tutamuweka mtu wetu atalinda utawala uliopita. Utawala uliopita haulindwi,” amesema Lema.
 
Naiona mbegu ya chuki kubwa sana miongoni mwetu. Sitaki kuamini kabisa kama watanzania sasa tunachukiana kiasi hiki . Hivi ni nani ameileta hii chuki?

Mbona zamani watanzania walikuwa na tofauti za kisiasa, lakini hawakuchukiana namna hii . Nini kimetokea Tanzania?

Dunia nzima sasa inatushangaa sisi . Kuna rafiki yangu anaishi Kenya juzi alinipigia simu akaniuliza nini kometokea huko Tanzania? ,mbona mnataka kutoana roho?.

Sitaki kuamini kama sisi ni Watanzania walewale wa siku zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We nani anataka kukutoa roho? Je unawamini wanasiasa? Kama unawaamini Zitto alifukuzwa cdm kama msaliti na wenzake leo kabadilika nini?

Tusipende kutoa majibu ya jumla jumla kwa tweet za wanasiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto naye ni mzito, na anajibebesha mazito yanayoacha maswali mazito..

~kwanini asiwapige picha,kuanzia gari na hata hao wafuatiliaji wake...na hizo picha wakazisambaza kwa mitandao.!?

~ulimwengu wa teknolojia anashindwa kuajiri hata mpiga picha wa siri.!??

HAWA wanasiasa sio wa kuwaamini kiivyoo...'akili za kuambiwa changanya na zako'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mm tangu sarakasi za lowasa ni fisadi then wakasema sio fisadi na kumpa agombee na kulamba matapishi yao niliichukia siasa kabisa
Mkuu leo buku 7 yako umeitendea haki!! Maana leo unamwaga povu bila nukta tokea alfajiri! Nennda dirishani sasa kapokee buku 7 yako!! Imetosha kwa leo,wakikuzingua tuite,tutakutetea tu,sisi tunapenda haki tu!
 
Bwana Lema tujuze umemuondoa Zitto yupi msaliti au yule sultan wa Act?
Hakuna watu vigeugeu kama chadema
 
CHUKI HII KWA KIASI KIKUBWA INALETWA NA GENGE FULANI LA WATU PALE CHADEMA WAKIONGOZWA NA MREMA,LEMA NA MBOWE na hii ndio source kubwa kwa yanayomsibu LISSU LEO HII.....

Hapa ni kama unaanika nguo kavu.
 
We nani anataka kukutoa roho? Je unawamini wanasiasa? Kama unawaamini Zitto alifukuzwa cdm kama msaliti na wenzake leo kabadilika nini?

Tusipende kutoa majibu ya jumla jumla kwa tweet za wanasiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi wewe unataka kitokee nini ili ukubali kuwa sasa hivi tuna tatizo hapa kwetu . Au unataka yakukute wewe mwenyewe au familia yako ndo ujue iko shida?

Hivi unadhani msichana mrembo kama Akwilina aliwahi kufikri iko siku atakufa kwa risasi?

Hivi wewe unadhani ni bora kuliko Nape aliyetolewa bastola mchana kweupe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unashangaa nini wazungu wakiongea ni Lissu ni mabeberu, wakiongea na serekali ni wadau wa maendeleo! Au umesahau Dr. Slaa alikuwa anaitwa padri mzinzi akiwa cdm, kaenda ccm ni mzalendo!
Tatizo unaulizwa vingine unajibu vingine au ndio Lissu alivyowafundisha kujibu maswali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sio kama jiwe uadui binafsi anaufanya uadui wa nchi
Persecutions, political repression

How Dictators Come To Power In A Democracy

by Jim Powell

Dictatorships are often unexpected. They have arisen among prosperous, educated and cultured people who seemed safe from a dictatorship – in Europe, Asia , Africa and South America.

Consider Germany, one of the most paradoxical and dramatic cases; to add, consider Tanzania, also one of the paradoxical and dramatic cases
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom