Dr Slaa ni balozi akiwakilisha nchi. Dr Slaa amebaki na heshima kubwa ambayo viongozi wenu hawana kwasasa. Hutaki sikulazimishi.Leo hii Slaa yuko wapi?
Lema kama kinyongaa,pia Lema kama sunguraa,sizitaki mbichi hizi.Kwa kifupi Lema asitufanye mazuzu ,yeye ndiye zuzu,hayoyite angesema wakati ule Lowassa yupo Chadema na sio baada ya kutoka,mbona alifyata mkia kama mbwa koko.Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka kuhusu uamuzi wa aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa kurejea CCM.
Lema amedai kuwa uamuzi wa Lowassa unadhihirisha kuwa ameweka mbele maslahi yake binafsi kuliko mabadiliko aliyokuwa anayahubiri alipoingia Chadema.
Alidai kuwa Lowassa alifikia uamuzi huo ili kulinusuru shamba lake linaloshikiliwa Mkoani Tanga, shamba lake la mifugo linaloshikiliwa Dodoma pamoja na kumnusuru mkwewe Sioi Sumari na kifungo dhidi ya kesi inayomkabili.
Sumari anatuhumiwa kwa kula njama ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kughushi pamoja na utakatishaji wa fedha.
“Mtu huyu alitaka kuwa Rais, hali ya kisiasa ilivyo sasa watu wapo magerezani, wanapata misukosuko ya kibiashara, hawana cha kuipa CCM ili wapate ahueni, lakini kwa sababu yeye anacho cha kuwapa CCM ilia pate amani. Hajaona gharama ya kufanya hivyo,” Lema amekaririwa na Gazeti la Mwananchi
“Chadema imepata baraka kuondokewa na mtu kama huyu. Alikuja kwa ajili ya kutaka urais na sio mabadiliko aliyokuwa akiyanadi. Nchi inataka demokrasia, katiba mpya, sheria mpya na inakabiliwa na ubanaji wa vyombo vya habari… mwanasiasa makini hawezi kuungana na CCM,” aliongeza.
Lowassa alijiunga na Chadema mwaka 2015 baada ya jina lake kuondolewa kwenye kinyang’anyiro cha watu waliokuwa wakiwania nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM. Aligombea urais na kuleta ushindani mkubwa dhidi ya Dkt. John Magufuli wa CCM.
Juzi alipokewa na Dkt. Magufuli, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lowassa alieleza kwa ufupi kuwa amerejea nyumbani. Alipokewa katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
hatoweza kumjibu hadi anakufamaswalo.mengine.magumu.mnoo..dont try this at home
Unateseka na nini! wewe CCM ni baba yako, au mama yako?Mimi huwa na mshangaa sana huyu bwana anajifanya ana DNA ya Chadema yani mtu akihama toka chadema kwenda chama kingine anamuona kama mkosaji sana na ni adui wa Chadema. Mbona wewe mwenyewe ulitoka TLP ukahamia Chadema. The problem is unaiona Chadema ndo baba yako na mama yako kwani kila ulichonacho sasa hivi ni hizi ruzuku za chadema mnazogawana otherwise ungekuwa bado unauza magodoro pale mianzini Arusha na ile gari yako Honda mbovu. So usiwe una panic sana mtu akitoka Chadema those are normaal things in politics brother
Mimi mwanachama akitoka CCM kwenda kwingine simuoni kama mkosaji hivyo CCM siyo mama yangu wala baba yangu
Basi wewe sio mwananachama ni mganga njaa.Mimi mwanachama akitoka CCM kwenda kwingine simuoni kama mkosaji hivyo CCM siyo mama yangu wala baba yangu
Asishambulie wanaotoka akawaona wakosaji sana, yeye aendelee kuganga tu njaa zakeKama ndio imemfanya asiuze magodoro ma gari yake mbovu(kama ulivyosema) kwanini asiifanye baba na mama yake?
Unapata tabu sana na Lema binti,tulia awavuruge akili zenu
Sent using Jamii Forums mobile app