Godbless Lema awataka wananchi kuvuta subiri, kujiandaa na maandamano makubwa

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Feb 9, 2010
899
1,084
*Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakisubiri serikali ipatie ufumbuzi suala la mgawo wa umeme unaondelea nchini ambao Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameahidi utamalizika Agosti 30, mwaka huu.

Lema alisema endapo muda huo utaisha bila tatizo hilo kumalizika hatakuwa na pingamizi kwa wananchi hao kuingia barabarani kufanya maandamano kushinikiza kupatikana kwa nishati hiyo aliyodai kuwa kukosekana kwake mbali ya uchumi wa nchi kuyumba linaongeza kasi ya vijana kuondolewa kwenye ajira.

Aliyasema hayo juzi alipokuwa akifafanua hatua yake ya kukwepa kupokelewa kwa maandamano yaliyoandaliwa na madereva wa daladala mwishoni mwa wiki katika eneo la Kisongo kwa lengo la kumpokea akitokea mjini Dodoma anakohudhuria vikao vya Bunge la bajeti ambayo yalikuwa yaishie kwenye viwanja vya NMC.

Lema alisema kuwa leo atakutana na madereva wa magari madogo ya abiria maarufu kama vifodi kusikiliza kero zao kama alivyowaahidi wiki iliyopita alipowasiliana nao akiwaomba kuacha mgomo wao uliodumu kwa siku tatu mfululizo ili wananchi wasiendelee kuteseka.

Alisema* kwa kuwa serikali imeonyesha nia ya kusikiliza kero za madereva hao na wako tayari kuzipatia ufumbuzi aliona hakuna sababu ya kuandamana na yeye kama mwakilishi wa wananchi wa Arusha Mjini ataendelea kufanya mazungumzo na serikali mpaka madereva hao wapatiwe haki zao ikiwa ni pamoja na kuacha kuonewa.

"Nawaomba wananchi wasubiri mpaka Agosti 30 kama ahadi ya Pinda (Waziri Mkuu)* haitatimia hapo tutaandamana mpaka kieleweke; hatuwezi kuadhimisha miaka 50 ya taifa huru tukiwa gizani huku serikali ikikosa sababu za msingi za kuwepo kwa tatizo hilo," alisema Lema.

pinda ukija na majibu ambayo hayana muelekeo wa kulitoa taifa kwenye giza, tutaandamana mpaka mtakapo achia nch
 
count on me kamanda LEMA. lazima tuikomboe nchi yetu chini ya udhalimu wa kina LUKUVI
 
hongereni chama cha kususa na maandamano kwenu solution ni kuandamana tu keep it up!
 
hongereni chama cha kususa na maandamano kwenu solution ni kuandamana tu keep it up!

Ukimsusia mlevi pombe anashangilia. Sasa mkuu unataka tususie kuandamana ili mafisadi wa CCM wafilisi nchi halafu watoto wetu wawe watumwa?
Pili, tusipoandamana leo dhidi ya ufisadi wa CCM hata watoto wetu watayalaumu makaburi yetu kwamba tulikuwa waoga mno na watatushangaa sana. Lazima tuandamane mpaka kileweke.
 
Maandamano is the only solution, no way back!!! coz mwisho wa siku ni patokee makutano fahamu, KUDAI UHURU NI RAHISI KULIKO KUDAI HAKI????
voxy populi voxy dei!!!!!
 
Ukimsusia mlevi pombe anashangilia. Sasa mkuu unataka tususie kuandamana ili mafisadi wa CCM wafilisi nchi halafu watoto wetu wawe watumwa?
Pili, tusipoandamana leo dhidi ya ufisadi wa CCM hata watoto wetu watayalaumu makaburi yetu kwamba tulikuwa waoga mno na watatushangaa sana. Lazima tuandamane mpaka kileweke.
Mwambie huyo mana mda umebakia kidogo TAHIRIRI itakuwa Dar.. Mwanza wataongoza mapambano, wakifuatiwa na Arusha, Mbeya na Kigoma watakuwa njiani kuelekea Dar..hapo ndipo mafisadi wote watakapo kamatwa na kufunguliwa mashtaka
 
Maandamano ndiyo njia sahihi kwa serikali isiyotaka kusikiliza wananchi wake. tutaandamana mpaka tone la mwisho
 
Back
Top Bottom