Godbless Lema amuonya Millard Ayo kwa kuonesha unyama wa Polisi wa Kenya na kuficha unyama wa Polisi wa Tanzania

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,472
215,294
Instagram media - B-VAE5gnzAt ( 717 X 640 ).jpg
 
Chombo cha habari akianzishe Millard Ayo, mafanikio yapatikane halafu wajinga fulani waanze kumpangia jinsi ya kufanya kazi zake!

Wakati anaanzisha chombo hakuenda kumuomba Lema ushauri halafu baada ya kufanikiwa eti ndio wajinga fulani wanaanza kutoa ushauri!

Kijana Millard Ayo hata baada ya kufeli kidato cha nne lakini hakukata tamaa aliamua kujiunga chuo kwa kozi ya mwaka mmoja ya Uandishi wa Habari, Arusha. Huo ukawa mwanzo wa mafanikio yake ambayo leo wajinga fulani wanataka kumpangia nini cha kufanya.

Kama Lema anadhani Millard Ayo hatangazi yale ambayo yeye anadhani yanafaa yatangazwe basi Lema aanzishe chombo chake cha habari! It's just simple!

Kulazimisha mambo fulani yafanywe kwa matakwa yako ni udikteta kama udikteta mwingine!
 
MsemajiUkweli,

Wala hata watazamaji hatuangaiki na mafanikio ya muanzilishi wa online tv ila kinachosikitisha ni kuwa double standard- kitu ambacho kikikomaa ni rahisi sana kushuka chini kwa hicho chombo Cha habari.

Unajuaje huo umaarufu wa Ayo tv labda umetokana na namna mwanzo habari zake alikuwa hana upendeleo wa habari lakini kwa sasa ameanza kupendelea baadhi ya habari na nyingine kuona hazina umuhim either kwa kuogopa mamlaka au vinginevyo!

Ni kazi sana kutengeneza brand ya kitu lakini ni rahisi sana kukishusha na kikadharauliwa hasa ukijisahau kidogo tu na kujiona umeshafika kileleni
 
MsemajiUkweli,
Double standard ndo anacholalamikia Mhe.Lema pia huna haja ya kutumia lugha za kuudhi kutoa hoja zako haikazii hoja inaweza ikakimbiza wasomaji wengine halafu kubalance stori wakenya wakiruka nae kwa kusambaza habari za kuichafua kenya wakati hayo ya polisi aggression (Excessive Force) hata huku kwetu yapo sio ishu ya yeye millard kushikia bango utawatetea wakenya ama la!
 
Kwahiyo walichofanya polisi Wa Kenya kimeripotiwa na Millard ni kuichafua Kenya Ila angeripoti ya Tanzania haichafui Tanzania bali amfurahisha lema vile abalanshisha stories?

Yoyote mwenye access na habari apaswa kuripoti tu pia vyombo vya habari viko mob si lazima Millard, muacheni na Uhuru wake kikubwa habari za kweli nanyi mripoti za polisi Tanzania waliowatandika bakora watanzania walokaidi amri ya kujikinga na korona.
 
Kwahiyo walichofanya polisi Wa Kenya kimeripotiwa na Millard ni kuichafua Kenya Ila angeripoti ya Tanzania haichafui Tanzania bali amfurahisha lema vile abalanshisha stories? Yoyote mwenye access na habari apaswa kuripoti tu pia vyombo vya habari viko mob si lazima Millard, muacheni na Uhuru wake kikubwa habari za kweli nanyi mripoti za polisi Tanzania waliowatandika bakora watanzania walokaidi amri ya kujikinga na korona.
Dude!.Polisi huwajui wewe utakuja kukutana na mikiki yao utamkumbuka Mhe.Lema inawezekana Mhe.Lema yupo kisiasa zaidi lakini soma katikati ya maneno yake utagundua tabia za polisi tanzania,kenya,uganda and most of african countries hawaheshimu kabisa haki za raia uje kuzushiwa jambo ukamatwe na polisi hadi umefikishwa mahakamani ndo utajua millard ayo alipaswa kuwamulika!
 
Wala hata watazamaji hatuangaiki na mafanikio ya muanzilishi wa online tv ila kinachosikitisha ni kuwa double standard- kitu ambacho kikikomaa ni rahisi sana kushuka chini kwa hicho chombo Cha habari. Unajuaje huo umaarufu wa Ayo tv labda umetokana na namna mwanzo habari zake alikuwa hana upendeleo wa habari lakini kwa sasa ameanza kupendelea baadhi ya habari na nyingine kuona hazina umuhim either kwa kuogopa mamlaka au vinginevyo! Ni kazi sana kutengeneza brand ya kitu lakini ni rahisi sana kukishusha na kikadharauliwa hasa ukijisahau kidogo tu na kujiona umeshafika kileleni
Unauliza:
''Unajuaje huo umaarufu wa Ayo tv labda umetokana na namna mwanzo habari zake alikuwa hana upendeleo wa habari''

JIBU: Mmiliki wa chombo cha habari (Millard Ayo) ndiye anayejua chanzo cha mafanikio yake na hajamuomba Lema ushauri.

Cha kushangaza na kuchekesha unatoa ushauri kwa Millard Ayo ambaye ameishafanikiwa. Kufanikiwa ni ishara kuu kuwa anajua sababu zinazofanya biashara yake ishuke lakini kikubwa zaidi hajakuomba ushauri.

Anzisha chombo chako cha habari na utumie ushauri wako kwenye chombo hicho! It's just simple!
 
Chombo cha habari akianzishe Millard Ayo, mafanikio yapatikane halafu wajinga fulani waanze kumpangia jinsi ya kufanya kazi zake!

Wakati anaanzisha chombo hakuenda kumuomba Lema ushauri halafu baada ya kufanikiwa eti ndio wajinga fulani wanaanza kutoa ushauri!

Kama Lema anadhani Millard Ayo hatangazi yale ambayo yeye anadhani yanafaa yatangazwe basi Lema aanzishe chombo chake cha habari! It's just simple!

Kulazimisha mambo fulani kwa matakwa yako ni udikteta!
Hapa tayari umeshapanic.
 
This is one of the best idiotic post of the century

Sent using Jamii Forums mobile app
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom