Godbless Lema ampa pole Rais Magufuli kwa kufiwa na mkwe wa mtoto wake

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
Mbunge wa Arusha mjini Mhe Godbless Lema ametoa pole kwa Mbunge wa Iringa Mjini Mhe Peter Msigwa kwa kufiwa na Dada yake, Vile vile Mbunge Huyo ametumia nafasi hiyo kumpa pole Rais John Magufuli na Familia yake kwa kuondokewa na Mama wa Mke wa Mtoto wake ambae anajulikana kwa jina la Joseph John Magufuli.

Akiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram Mhe Lema amesema "Tumemaliza safari ya kumpumzisha Mama Tryphosa Sanga ambaye ni Dada wa Mh Peter Msigwa na ambaye pia ni Mama Mkwe wa mtoto wa Mh Rais John Magufuli, Hivyo nimempa pole pia Mh John Magufuli na Familia yake kwa msiba huu"

IMG-20190401-WA0274.jpeg
 
Ingefaa zaid kama jiwe ndo angempa pole Msigwa. LEMMA wakati mwingine anajivunjia sana. We kula buyo tu huwezi kupata CREDIT kwa kumnyenyekea JIWE.
Namkumbuka Dr LISSU alivyosema hamuungi mkono na anatamani awekewe vikwazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona wanataka kuficha kua jiwe kaenda kuhani kwa sababu ya mwanae kufiwa na mama mkwe , lengo Lao ionekane jiwe kaenda kwenye msiba wa mpinzani

USOGA WI KUA KATI MWINA NSONGOO
 
Back
Top Bottom