Godbless Lema aliomba bunge kutunga sheria ya kuweka ukomo wa Upelelezi kwa jeshi la polisi dhidi ya kesi za washitakiwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,377
217,438
Mh Lema ambaye pia ndiye Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi , ametoa hoja hiyo kabambe alipokuwa akichangia bungeni , ambapo amedai kwamba baadhi ya watu wanakomolewa kwa kisingizio cha upelelezi kutokamilika .

Ametoa mfano wa Mkurugenzi mmoja wa shirika la serikali aliyewekwa ndani muda mrefu kwa tuhuma za ufisadi huku akisubiri upelelezi ukamilike , lakini baadaye akafutiwa mashitaka na DPP na kisha Kurejeshwa kazini .

Amewashangaa wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa waliojivika Uungu Mtu kwa kuamuru watu kukamatwa watakavyo kiasi cha kudharau hata maelekezo ya Waziri Mkuu , hii ni miongoni mwa hotuba kali sana za Mh Lema alizowahi kuzitoa kwenye Bunge la Tanzania ( naitafuta video yake ili mupate uhondo kamili )

#Tuendelee kunawa mikono ili kujikinga na virusi vya Corona
 
Hii katiba na sheria tulizonazo vikimkuta mtu km dikteta uchwara ambaye sasa ni dikteta kamili lazima awaumize wananchi km tumavyoona watu wanakaa mahabusu indefinitely wakisubiri uchunguzi ambao kimsingi unakua haupo.........

Bado ccm watatumia wingi wao kukataa akili kubwa za wapinzani na kuendelea kukandamiza watz kwa kisingizio mfu cha uchunguzi
 
Hapo ukabambe wake Ni UPI? Upelelezi una taratibu zake, hoja ya msingi ingekuwa MTU asikamatwe kama hakuna ushahidi Wa kutosha, hats miaka kumi wapeleleze tu...
Sasa hizo taratibu za upelelezi zina loop holes zinazosababisha watuhumiwa wanadhulumiwa haki zao ndiyo maana mbunge ambaye ni mtunga sheria anashauri sheria ya upelelezi ibadilishwe iwe na kikomo isitegemee tu busara ya jaji/hakimu.

Hebu jifunzeni kusikiliza na ku-appriciate hadi hoja za msingi za watu msiowapenda as long as ni jamii nzima ndiyo itanufaika na sio Sugu na Mdee pekee.

NB:
Sasa nimeelewa kwanini wabunge wa CCM wanapiga makofi kumshangilia mbunge anayesema ili kupambana na korona tusitangaze idadi ya wagonjwa wa korona🤣🤣🤣
 
Umeandika kisomi sana mkuu
 
Mh Lema ambaye pia ndiye Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi , ametoa hoja hiyo kabambe alipokuwa akichangia bungeni , ambapo amedai kwamba baadhi ya watu wanakomolewa kwa kisingizio cha upelelezi kutokamilika .

Ametoa mfano wa Mkurugenzi mmoja wa shirika la serikali aliyewekwa ndani muda mrefu kwa tuhuma za ufisadi huku akisubiri upelelezi ukamilike , lakini baadaye akafutiwa mashitaka na DPP na kisha Kurejeshwa kazini .

Amewashangaa wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa waliojivika Uungu Mtu kwa kuamuru watu kukamatwa watakavyo kiasi cha kudharau hata maelekezo ya Waziri Mkuu , hii ni miongoni mwa hotuba kali sana za Mh Lema alizowahi kuzitoa kwenye Bunge la Tanzania ( naitafuta video yake ili mupate uhondo kamili )

#Tuendelee kunawa mikono ili kujikinga na virusi vya Corona
Hatuhitaji sheria kwenye hili.

Tunahitaji mapito na mabadiliko ya criminal justice act na kanuni zake
 
Hapo ukabambe wake Ni UPI? Upelelezi una taratibu zake, hoja ya msingi ingekuwa MTU asikamatwe kama hakuna ushahidi Wa kutosha, hats miaka kumi wapeleleze tu...
Upelelezi unakusanya ushahidi, unavyomkamata mtu wakati hujapeleleza, au umepelelezi unaendelea inamaana kwamba, huna ushahidi. Unakua Ni uonevu. Nchi wa wenzetu Wanalupeleka mahakamani wakiwa wamaliza upelelezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom