Godbless Lema aitikisa Tarime; Kagasheki adai anachochea vurugu

Aibu kwa mtu mzee kama Kagasheki kuongea uwongo mchana kutwa.
Kwanini wanashindwa kufanya uchunguzi na utafiti wa tatizo la Tarime, wanaishia kujaribu karata tu? Ndiyo mambo ya semina elekezi nini?...fyuuuu?
 
Kagashek ametoa kauli tata kuwa waliouwawa Tarime walikuwa wahalifu lakini serikali imetoa msaada wa mazishi. je serikali imeanza lini kuoa msaada kwa waharifu? Amepima kauli yake kweli au ndio sias za Tanzania?

serikali haiko kimpangilio....kila mtu ataibuka na kusema la kwake...tutasikia na kuona mengi msimu huu...
 
kinachomsumbua kagasheki na serikali yake ni hofu na woga dhidi ya chadema ambacho kinatikisa nchi nzima.

na tutazidi kupambana na wakurya ni wenzangu na nitapambana kudai haki zetu na dhahabu yetu pale nyamongo hii serikali aitufai kabisa ndugu tupambane kwa uwezo wetu wote
 
Kagashek ametoa kauli tata kuwa waliouwawa Tarime walikuwa wahalifu lakini serikali imetoa msaada wa mazishi. je serikali imeanza lini kuoa msaada kwa waharifu? Amepima kauli yake kweli au ndio sias za Tanzania?

kweli serikali hii ni ya kutoa huduma za mazishi kwa raia wasio kuwa ni wema? Ama kweli Mungu anapotaka kufanya kitu hata wale ambao mnawaona ni wazuri hakika wanageuka kuwa wabaya sikutegemea kauli kama hizi kutoka kwa huyu muhaya mtani wa wakurya
 
Mkuu mbona unakurupuka, hapo kwenye red ebu tuambie Katiba ya Tanzania inasemaje kuhusu hicho cheo ulichokitaja
We ambae hujakurupuka Tuambie Katiba inasemaje kuhusiana na Jeshi la Polisi kuwapiga Risasi nakuwaua Wananchi wa5 wa Nyamongo huko Tarime.
 
, waziri kwa kauli yako unataka kuuambia umma kuwa wananchi waliompigia kura mpendwa wao wana akili finyu kukubali kirahisi kupokea ushauri kutoka kwa mtu wasiyeishi wala kuongozwa naye wa kumfanyia fujo mb wao? mh, naibu waziri tanguliza uzalendo kwa nchi yako na watu wako kwanza kabla ya kuficha ukweli juu ya ndg zetu wa tarime. ushabiki huu ni kama bomu linalosubiri kulipuka wakati wowote kwani wananchi wa sasa wanaelewa wanachofanya na si wa kupelekwa pelekwa kama wale wa mwaka 47. kila baya anasukumiwa lema. this is unfair!
 
mh.Lema mahali ulipo heshima kwako mkuu huwa unafanya vitu ambavyo kimsingi ni wachache wanaweza kufanya.tunaitaji akina Lema wengi zaidi wasiogopopa chochote,wanafanya mambo kwa moyo dhabiti,wenye kutoa hoja bila kumung'unya maneno pia na kujituma.God blesse you abudantly.
 
Hapo kwenye red, saizi Tanzania ingekuwa kama Somalia, Lema Hamna kitu wewe ni Mbunge wa Arusha unakwenda Tarime kama nani? msitulete vita Tanzania:sorry:

bila shaka wewe ni mmoja kati ya wale mabibi kizee wanaodanganywa kwamba Chadema italeta vita,endelea kupokea kanga za bwelele waache wanaume wakina Lema wafanye kazi,na mapinduzi yataletwa na vijana sio nyie vikongwe
 
Mbunge wa arusha mjini na waziri kivuli wa mambo ya ndani akiwa ameambana na mbunge wa vitimaalum chadema ester matiku leo walitembelea tarime kwenye yale mauaji ila kabla hawajaenda huko walienda kwanye ofisi za mbunge wa jimbo hilo na kuwachwa mdomo wazi pale mbunge wajimbo hilo na watendaji wake walipo kimbia ndipo lema na matiku wakaamua kwenda kwa mkuu wa wilaya napo huko walikutana na vizingiti

ila lema akamlazimisha mkuu huyo wa wilaya kumpa taarifa za awali ndipo mkuu huyo alipo ropoka na kusema hawa wananchi ni wajinga sana walistahili kuuwawa na lema akamjibu nashukuru sana hii itakuwa nimoja ya taarifa zangu.

lema na msafara wake ukawa unaelekea kwenye eneo la mauaji ndipo wakakutana na kundi kubwa la wananchi watarime wakamzuia lema na kusababisha umati mkubwa sana na wakamlazimisha lema kuhutubia ndipo lema alipo anzakuongea nao na baada ya hapo walimlazimisha lema kufanya maandamano ndipo lema alipo kataa kuepusha vurugu zaidi na hivyo lema akashindwa kuendelea na safari yake ya ukaguzi, kamanda LEMA alikuwa akitokea JIJINI MWANZA

Naikumbukwe pia LEMA ni waziri kivuli wa mambo ya ndani so alikuwa ameenda kutembelea eneo la tukio na ndipo alipo amua kufuata hizo taratibu kwa kumfuata mbunge wa jimbo hilo ili amueleze kilichotokea ndipo walipo ingia mitini .

SOURCE JF
viongozi wa hii nchi wanatumia chadema kama defensive mechanism yao-na wanataka kujitoa as if kulikuwa hakuna matatzo yoyote-ni uchochezi tu wa chadema-sijui kwa nini wanataka ku-fool jamii ya tz hivi-na wanataka kuichafua chadema ionekane kama chama chenye kuleta migogoro tu-kumbe sivyo
 
Naona huyu jamaa naibu waziri amepauka mawazo ya kuongea! Fulani anachochea vurugu halafu inatoa msaada wa mazishi? Yeye ni waziri mwenye mamalaka ya usalama wa ndani amechukua hatua gani?
 
Kuna mtu jana alitahadharisha kuwa huenda serikali ika-mbrand Lema kuwa ndiye anayechochea hizi vurugu na kweli imekuw hivo...

Mtego wa Noti kwenye Hilo kamwe Hawatafanikiwa kumbuka Kagesheki amesoma Sheria na kwa dhamana yake kama Naibu waziri wa Mambo ya Ndani iwapo Lema angekuwa ameenda Kinyume au amevunja Sheria basi angekuwa ashakamatwa saa nyingi.Hawa Watu wa Chadema wapo Makini sana kumbuka walipoingia Tarime moja kwa moja walienda kwenye ofisi za Dc nakujitambulisha nakueleza kilicho wapeleka ye kama Waziri Kivuli wa Mambo ya ndani na mwenzie Ester Matiko Waziri Kivuli wa Uwekezaji.Badae walienda Ofisi Za Mbunge wa Tarime ambapo hawakufanikiwa kuonana nae so hilo swala lakuhamasisha fujo na Blabla zingine ni kelele tu.These People bana are so Strategic na wanafanya mambo yao Kwa Taadhari ya khali ya Juu.
 
Naibu waziri wa mambo ya ndani Balozi Kagasheki amesema kuna mbunge kutokea chama ulani na mkoa fulani yuko Tarime anachochea vurugu
MyTake...anamaanisha Mh. Lema wa Arusha ambaye yuko Tarime hivi sasa...
Source...TBC1

Yeye Waziri yuko wapi sasa? Amekaidi amri ya JK eh?
 
Kama Kagasheki ameona Mheshimiwa Lema ana makosa kama anavyodai, angetulia akusanye ushahidi na ampeleke mahakamani..Kusema ukweli Kagasheki amekurupuka na hizi kauli zao zitazidi kuleta maafa Tarime!!
Je Arusha ni mbunge yupi kachochea fujo za kumng'oa Mary Chi(Ki)tanda?
 
Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh Hamis Kagasheki amesisitiza kuwa mbunge wa Arusha mh Godbless Lema ndiye aliyekwenda kuchochea wananchi wa Tarime kuvamia mgodi wa Morth Mara. "nilisema jana na leo narudia tena, huyu mbunge ametoka mkoani kwake na kwenda kule kuchochea fujo. Hii haikubaliki" amesisitiza
source-tbc 1


Niseme, ni makosa makubwa kwa viongozi kama Kagasheki kuendelea kujejeli wananchi kuwa hawana uwezo wa kufikiri wala kuamua mpaka waambiwe hivyo ni mwanasiasa! Haya ni madharau kwa Watanzania. period.

Naomba wanaJF mnivumilie nitaandika essay ndefu kidogo lakini nataka nieleze kile ninachoona ni unafiki wa wakubwa wetu. Kabla ya yote niseme siungi mkono watu kuvamia mgodi lakini naweza kuelewa ni kwa nini wamevamia huo mgodi.

Matatizo ya wana-Tarime na mgodi wa North Mara hayajaanza leo, hata wakati Barrick wananunua mgodi walinunua mgodi na mgogoro juu (package). Kagasheki anaweza kusema ni nani alikuwa anachochea hiyo migogoro huko nyuma? Kwa waliofika North Mara kuna wananchi wanaoishi karibu sana na ulipo mgodi hasa sehemu ya kumwaga mchanga. Jioni baada ya ku-blast watu wanakuja kuukoteza vipande/mchanga kama source ya kujipatia kipato. wamebatizwa -Intruders!

Lililo wazi ni kwamba hawa intruders wengi wao ni wananchi waliokuwa wanajishughulisha na uchimbaji eneo ulipo mgodi na sasa hawana alternative means ya kuishi baada ya kuondelewa kwenye maeneo ya machimbo kupisha wawekezaji. Kwa wengi wasio fahamu, yapo makubaliano juu ya wajibu wa serikali kwa wananchi walioondelewa kwenye maeneo yao. Hivyo hivyo wawekezaji nao wana list yao ya nini wanatarajiwa kufanya ili kuhakikisha jamii inayozunguka mgodi wanafaidika. Kwa mfano mgodi wana kiasi wanalipa 'levy' kwa vijiji vya jirani lakini cha ajabu huwa haya malipo yanakuja moja kwa moja serikali kuu - yaani hazina! and no one knows wanavijiji wanafaidikaje na haya malipo. no one! vijiji vinabaki mdogo wazi!

Pia kulikuwa na programme imeanzishwa na Barrick ya kusaidia wachimbaji wadogo dogo kwenye masuala ya skills/training, processing, na masoko. Kutokana na ukweli kwamba wengi wa hawa wananchi wanatumia zana duni na pia 'grade' ya gold wanayopata sii ya juu sana basi wengi wamekuwa wanawauzia 'middle-men' kwa bei ya chini. Barrick kushirikiana na shirika moja la kimatifa walikuwa wametafuta soko ili hawa wachimbaji waweze kuuza huko moja kwa moja huko. Tatizo la huu mkakati likawa ni mtaji.

Hata hivyo Barrick walikubali kutoa sehemu ya mtaji, shirika la kimataifa nalo lilikuwa tayari kuchangia kiasi, serikali nao walitakiwa wajitutumue. Na huu mpango ulikuwa uwe on commercial basis lakini kwa masharti nafuu ili kadri mtaji unavyokuwa basi wachimbaji wengi nao waweze kupata capital na everything was in place. (ni kama ka-bank ka wachimbaji wadogo hivi). Kumbuka training ilikuwa ni kati ya huu mkakati.

Hatua za awali zilifanyika na wapo baadhi wa wachimbaji walipelekwa mbeya (I believe ni Mbeya Institute) kuangalia mafunzo yatakavyokuwa yanaendeshwa. Mpaka hapo mambo yalienda vizuri na miongoni mwa waliokuwa mstari wa mbele kusimamia huu mpango walikuwapo watanzania wenzetu. Well, kama ilivyo kwenye umme kwamba 'mgao sasa mwisho' lakini bado tuko kwenye mgao tena wa nguvu, huu mkakati umekumbwa na matatizo hayo hayo. lack of commitment and a shared vision. Cha kuhuzunisha ni kwamba mkakati kama huu unapodorora wanaoumia ni wananchi wa kawaida na sasa tuna msiba Tarime. Kwa kifupi kuna mambo mengi sana ambayo yanakwenda sivyo na nahisi viongozi wetu wanasema hili wakiwa na sisi wananchi, lakini wanasema jengine wanapokuwa na wawekezaji. na huu ndio unafiki ninaongelea hapa.

Kila mwaka tunawasikia wanasiasa wakisema 'tuna mpango madhubuti wa kusaidia wachimbaji wadogo wadogo'! Ni lini watawasaidia maana watu wanataka kulisha familia zao, wanataka kusomesha watoto wao, wanataka umeme, wanataka barabara. Ni lini wanasiasa hawa wataanza kutekeleza hiyo mikakati ili wana-Tarime wafaidike na rasilimali zilizowazunguka? Ni lini?

Muwekezaji kama Barrick ni mfanyabiashara, yuko Tanzania kwa maslahi yake na si kwa sababu anatupenda saaana hivyo akaamua kuhamia Tarime! Ana shareholders na ana targets za profits. Ni biashara imemleta hap. Na siwalaumu Barrick moja kwa moja kwa sababu kama muwekezaji nani alimkaribisha? Hivi unapokuwa na mgeni si unafagia fagia ili mazingira yawe ya kuridhisha? sasa serikali ilijiandaaje kabla ya huyu mgeni kuja?

Nimalizie, siamani muwekezaji anaweza kuja Tanzania akaanza kufanya mambo anavyotaka bila kujali sheria zinasemaje. Ikitekea hivyo basi ni udhaifu kwa serikali husika. Kagasheki asianzishe malumbano ya kisiasa, atatue matatizo ya msingi. Wana-Tarime wanauliza walisheje familia zao, watasomashaje watoto wao, watapataje malazi mazuri na kubwa zaidi watapaje maisha bora with or withour muwekazaji. hayo tu Mheshimiwa Kagasheki.
 
Yeye Waziri yuko wapi sasa? Amekaidi amri ya JK eh?

kama kweli yeye ni waziri anaye kubalika na chama chao cha magamba aende tarime saizi tuone kitakacho tokea mkama mwenyewe kakimbia vibaya
 
Wana JF huyu Kagasheki hata shuleni alikuwa ***** tu waliosoma naye wanamjua alifeli pekeyake darasa zima form four Kahororo Sec. Asipoteze muda kumjadili
 
Kama Kagasheki ameona Mheshimiwa Lema ana makosa kama anavyodai, angetulia akusanye ushahidi na ampeleke mahakamani..

Hapo ndio pamenishangaza, yeye ni waziri ambaye jeshi la polisi lipo chini yake. Kama ameona Lema amehusika kwa namna yoyote kwanini asiwaagize wamkamate halafu wamfungulie mashtaka? Au anajaribu kuwasafisha polisi walioua raia waonekane safi na wananchi ndio wajinga! Kwamba wameshawishiwa tena na wakuja kufanya fujo? Kwani wao hawana akili?
 
Yeye Waziri yuko wapi sasa? Amekaidi amri ya JK eh?

kama kweli yeye ni waziri anaye kubalika na chama chao cha magamba aende tarime saizi tuone kitakacho tokea mkama mwenyewe kakimbia vibaya
 
Back
Top Bottom