Godbless Lema, achana na Siasa za kuongelea watu, na majungu jikite nini utaifanyia nchi hii ya Tanzania

Siasa ni watu watu ni siasi
Mapungufu ya mwanasiasi ni daraja na ngazi ya mwanasiasa
Ulitaka ongelee mapungufu ya Wanyama ?!
Sema Lema na ww Rudi Tz sion ulichokimbia..
Labda ulitaka familia yako iishi huko
Rudi Nyumbani wakati wenu wa kuchukua nchi ni sasa Gaidi hayupo tena
Uyu mkimvua ushingi mshaingia ikulu
Muendelee kunywa Konyagi.
 
Siasa ni watu watu ni siasi
Mapungufu ya mwanasiasi ni daraja na ngazi ya mwanasiasa
Ulitaka ongelee mapungufu ya Wanyama ?!
Sema Lema na ww Rudi Tz sion ulichokimbia..
Labda ulitaka familia yako iishi huko
Rudi Nyumbani wakati wenu wa kuchukua nchi ni sasa Gaidi hayupo tena
Uyu mkimvua ushingi mshaingia ikulu
Muendelee kunywa Konyagi.
Narudia, siasa si umbea na majungu. Siasa ni maono na mikakati ya kuwaongoza wananchi kwa kuwaletea maendeleo. Hatupo kusikiliza majungu. Tunataka tuone nini kitafanyika kuhusu uchumi, kuhusu maendeleo ya jamii, kuhusu afya na kadhalika. Siyo kila siku mtu kuongelea watu. Kuna usemi usemao akili ndogo uongelea watu, lakini akili kubwa uongelea maswala makubwa ya kijamii. Sina ushabiki wa kumshabikia mtu tu, kwa uropokaji. Bali natumia akili kujiuliza huyu kiongozi ana maono yapi, mawazo gani mapya aliyonayo kuifanya Tanzania ipige hatua kimaendeleo.
Sijawahi muona huyo Lema wako, kafanya kongamano la vijana hata online tu kuongelea maswala yanayohusiana na vijana hasa kuwakwamua na ugumu wa maisha walionao. Mfano, Kupigania vijana kuwa na mikopo nafuu ya kuwainua kimaisha. Lema anatoka eneo la wafugaji, je amefanya nini kuinua maisha ya mfugaji na wakulima. Kwann asipate muda wa kukaa na hawa watu kisha akaja na wazo mfano ngozi nyingi za wanyama zinapotea, kuna wazo la kuanzisha viwanda vidogo kama ilivyo ethiopia kutengeneza bidhaa ya ngozi.

Je amefanya kampeni yoyote kuleta mabadiliko ya kuwa na makazi bora hasa sehemu za wafugaji na wakulima kuwahamasisha kujenga nyumba bora na za kudumu? Uongozi si lazima uwe ikulu, ni moyo wa kuwatumikia wananchi na kujenga mawazo kwa jamii ili iweze piga hatua kimaendeleo. Hapo wananchi watakuona unafaa, na ipo siku utafika unakotaka. Si majungu na umbea.
 
Back
Top Bottom