Godbless Lema acha kupoteza nguvu zako bure

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,797
71,216
Umekuwa ukishawishi watu wa Arusha kujiandikisha kupiga kura kwa mikutano na matangazo kiasi cha kufikia gari la matangazo kukamatwa.

Umejiuliza kwa nini watu wamegoma kujiandikisha uchaguzi serikali za mitaa?
Maagizo ni kuwa asitangazwe mpinzani kuwa mwenyekiti wa mtaa au kijiji hata kama kashinda, sasa wewe unawatengenezea CCM wapigakura ili kuwafanikisha?

Hebu acha, ya ngoswe muachie ngoswe ngoja wapiga kura iwe 20% na CCM washinde 100% wenyeviti wote na Magufuli afurahi kama alivyo agiza.
 
Ayaaaaaaa jamaa anazingua sasa jamani CCM ,waachwe wajifanyie uchaguz wao wenyewe huko na jiwe afueahi # hakuna kujiandikisha wala kupiga kura####\
Halafu kesho kutwa watendaji wakitimiza agizo la "nakupa mshahara unatangaza mpinzani?" Haohao kina Lema ndio wanakuja kulalamika na kulialia eti iko siku.
 
Wewe unataka kumuonea Lema pasipo sababu za msingi. Kama kuna ulazima wa kususa basi vema ungewashauri viongozi wakuu wa chama wakatoa tamko rasmi la chama kuwataka wanachama kususia zoezi la kujiandikisha.
 
Umekuwa ukishawishi watu wa Arusha kujiandikisha kupiga kura kwa mikutano na matangazo kiasi cha kufikia gari la matangazo kukamatwa.
Umejiuliza kwa nini watu wamegoma kujiandikisha uchaguzi serikali za mitaa?
Maagizo ni kuwa asitangazwe mpinzani kuwa mwenyekiti wa mtaa au kijiji hata kama kashinda, sasa wewe unawatengenezea CCM wapigakura ili kuwafanikisha? Hebu acha, ya ngoswe muachie ngoswe ngoja wapiga kura iwe 20% na CCM washinde 100% wenyeviti wote na Magufuli afurahi kama alivyo agiza.
Natamani aisome pamoja na Zito Kabwe waelewe huu ujumbe.

Yes, wanahangaikia wenyeviti ili chama kipate viongozi kuanzia ngazi ya chini ila inaonyesha namna gani wanasiasa ama wanasahau mapema au hawako na sisi au wanahisi aliyetoa hayo maelekezo alikuwa anatania na walioelekezwa watapuuza

Niwahakikishie, hata kama aliyetoa maelekezo alikuwa anatania ila ukweli ni kwamba viongozi walioelekezwa hawatapuuza maana kila mmoja anatafuta apige vipi zeze lake na vinubi mfalume amfurahie!? Maana zawadi toka kwa mfalume huwa inathamani kubwa hata kama ni andazi la shilling mia
 
Umekuwa ukishawishi watu wa Arusha kujiandikisha kupiga kura kwa mikutano na matangazo kiasi cha kufikia gari la matangazo kukamatwa.
Umejiuliza kwa nini watu wamegoma kujiandikisha uchaguzi serikali za mitaa?
Maagizo ni kuwa asitangazwe mpinzani kuwa mwenyekiti wa mtaa au kijiji hata kama kashinda, sasa wewe unawatengenezea CCM wapigakura ili kuwafanikisha? Hebu acha, ya ngoswe muachie ngoswe ngoja wapiga kura iwe 20% na CCM washinde 100% wenyeviti wote na Magufuli afurahi kama alivyo agiza.
Nyinyi ndio wapinga maendeleo.
Uchaguzi unafanyika kwa uhuru na haki.
Kura zinapigwa vituoni na kuhesabiwa vituoni mbele ya mawakala wa vyama, kura wangeiba vipi?.
P
 
Lema kaokoka, mwakani anakuwa muhubiri wa redio safina na kuachana na ubunge, mwache afanye kazi ya kumpendeza Mungu
 
Nyinyi ndio wapinga maendeleo.
Uchaguzi unafanyika kwa uhuru na haki.
Kura zinapigwa vituoni na kuhesabiwa vituoni mbele ya mawakala wa vyama, kura wangeiba vipi?.
P
Umeongea point kubwa ujue Kuna baadhi ya watu wanaendeshwa na miemuko kuliko akili hata Mimi nashangaa hizo kura wanaibiwaje? mbona hatasijawahi kusikia mawakala wa upinzani wakilalamika au kutosaini form za matokeo wakati wao ndio wasimamizi wa matokeo Kama mawakala wao wanasaini form za matokeo kuridhia matokeo hao wanasiasa malalamiko yao yanatokea wapi?au ndio kisingizio zakushindwa.
 
Haiwezekani ulazimishe watu wajiandikishe lakini kura zao usiziheshimu.
"Nakulipa mshahara, nakupa nyumba na gari halafu unamtangaza mpinzani?"
Sasa mpinzani hataki kujiandikisha unamlazimisha?
 
Umekuwa ukishawishi watu wa Arusha kujiandikisha kupiga kura kwa mikutano na matangazo kiasi cha kufikia gari la matangazo kukamatwa.

Umejiuliza kwa nini watu wamegoma kujiandikisha uchaguzi serikali za mitaa?
Maagizo ni kuwa asitangazwe mpinzani kuwa mwenyekiti wa mtaa au kijiji hata kama kashinda, sasa wewe unawatengenezea CCM wapigakura ili kuwafanikisha?

Hebu acha, ya ngoswe muachie ngoswe ngoja wapiga kura iwe 20% na CCM washinde 100% wenyeviti wote na Magufuli afurahi kama alivyo agiza.
Inasemekana huyo Lema ndio mgpmbea ubunge wa CCM hapo Arusha mjini 2020.......,yule Gambo amekubali matokeo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom