Godbless Jonathan Lema, anastahili kutendewa haki , anastahili pongezi, anastahili kuungwa mkono

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Jonathan Lema , anastahili kutendewa haki , anastahili pongezi, anastahili kuungwa mkono kwa njia zote ili aweze kupata haki yake.

Amefuata nyayo za mashujaa mbalimbali waliowahi kutokea Duniani, yawezekana leo tusimuelewe lakini hakika ataeleweka tu.

Watesi wake wanaohangaika na ndoto wanakosea sana kwani katika mafundisho ya dini ya kikristo Suala la Vijana kuota ndoto ni la Kiimani sana. Hivi angeota uchumi wa viwanda utafikiwa 2019 angelikuwa mahabusu?

[HASHTAG]#JusticeforLema[/HASHTAG]
 
kwani hatendewi haki mkuu...si ana watetezi wazuri waliomtetea mara nyingi tu na akashinda....kuendelea kukaa mahabusu ina maana tuanze kuhoji uwezo wa watetezi wake(mawakili)
 
Haki km mawakili wake wanajichanganya vile..wao ndo wanaofanya anaendelea kusota zaidi wanashindwa kung'amua hata vifungu vidogo vidogo...
 
Sikupendezwa na kauli ya Lema kumtabiria mtu mwngine kifo, kwani kifo na magonjwa ni yetu wanadamu wote na ni mpango wa Mungu!

Yalitokea pia kwa Edward Lowasa, kutabiriwa kifo na magonjwa,jambo ambalo halikuwa sahihi!

Yoote hayo ni makosa, ila ni kwanini sheria inabagua wakosaji wa kosa lilelile?
 
Anayofanyiwa Mhe. Lema ni dalili tosha kuwa bado Nchi hii inasafari ndefu kuwa HURU ! Kila siku nawaambia kuwa bado uhuru wengi hawaelewi. Mhe. Mbunge anashikiliwa kijanjajanja kwa takribani mwezi je mwananchi wa kawaida wa Nyanungu, mtama, kibondo n.k itakuwaje?. Na hii ni kwa sababu taaluma inaongozwa na siasa. Mahakama inaendelea kujidhalilisha!
 
Si mlisema Lema hahitaji kumpigia mtu magoti?

Na kwamba yeye ni aluwatani?

Kwamba kesi yake inasimamiwa na mawakili wasomi?

Kwamba Arusha kitanuka kama haki haitendeki?

Kwamba Lema ni jeshi la mtu mmoja?

Sasa hiyo haki, na aungwe mkono kutoka wapi mtu anaejitisheleza?
 
Joshua Nassari ndo mbunge ninayemkubali sana kwa upande wa Upinzani,wengine km akina Lema ni shida ..
 
Lema si nabii mwsmbie aje aniombee make najua wewe alishakuombea ndo maana una fikra kma hizo
 
Kama nchi yetu ikifuata haki bila kuangalia huyu ni chama Fulani basi wafuasi wengi wa upinzani wasingekuwa ndani kama tuonavyo, wala wafuasi wengi wa upinzani wasingekuwa wanakaa mahabusu kwa muda usiojulikana bila sababu, ukiangalia kwa utagundua kabisa kinachoisumbua nchi hii ni vyama kuwa bora zaidi kuliko haki ya mtu, maendeleo, ukweli,nk. Tukiweka hisia ya vyama vyetu pembeni sioni kama lema kwa ndoto tu hizo alizoota awekwe ndani ya siku zote bila kupata dhamana, huo ni uonevu wa watu weusi tulivyo pindi tunapokuwa juu, mambo ya kukomoana kukomeshana ,kuabudiana pasipo sababu, sioni mahali ambapo lema kaua,au ana kesi kubwa ya jinai ambayo inasababisha hadi dhamana asipate, ndo maana trump anasema Africa kwa ujumla tunatakiwa tutawaliwe tena ili tujifunze kuwa more civilized na kuheshimu maoni ya pande tofauti bila kuchukuliana hatua za kukomoana.
 
Sikupendezwa na kauli ya Lema kumtabiria mtu mwngine kifo, kwani kifo na magonjwa ni yetu wanadamu wote na ni mpango wa Mungu!

Yalitokea pia kwa Edward Lowasa, kutabiriwa kifo na magonjwa,jambo ambalo halikuwa sahihi!

Yoote hayo ni makosa, ila ni kwanini sheria inabagua wakosaji wa kosa lilelile?
Huu ni upinzani naselikali.... Mpango WA serikali katili na dhalimu kama hii nikufuta upinzani nchini nasi kundeleza vyama vingi na kukuza demokrasia ......... Hivyo usishangae kwa anayotendewa Lema na hakutendewa Bulembo na wenzake...... HAKUNA HAKI, HAKUNA AMANI, HAKUNA TUMAINI TANZANIA NI HUZUNI . kuona haya
 
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Jonathan Lema , anastahili kutendewa haki , anastahili pongezi, anastahili kuungwa mkono kwa njia zote ili aweze kupata haki yake.

Amefuata nyayo za mashujaa mbalimbali waliowahi kutokea Duniani, yawezekana leo tusimuelewe lakini hakika ataeleweka tu.

Watesi wake wanaohangaika na ndoto wanakosea sana kwani katika mafundisho ya dini ya kikristo Suala la Vijana kuota ndoto ni la Kiimani sana. Hivi angeota uchumi wa viwanda utafikiwa 2019 angelikuwa mahabusu?

[HASHTAG]#JusticeforLema[/HASHTAG]
Mnapiga makelele mitandaoni tu wakati hata ofisi za mitaa hamjawahi kufungwa. Kazi yenu kujifanya mnasaport nje wakati kwenye majanga mnakimbia. Hivi ingekuwa kafungwa lisu au mbowe angekuwa bado lupango?

Mimi siungi mkono hoja zako kwasababu zimekaa kinafiki,usikute hata mkewe hujawahi kwenda kumfariji.
Harafu Jamaa ananyea debe mwenyekiti anatangaza operation kata funua Yaani hapa ndio unaona Kuwa mabadiliko sio kuzungusha mikono tu na kupiga pushup majukwaani. Sitaki siasa ila namuonea huruma Jamaa kwa mateso anayopitia huku wenzake wapo kitaa tu
 
Anastahili kuungwa mkono kwa Ndoto yake?hii inaonyesha waafrika tulivyo,badala ya kumsifia afanye kazi tunaunga mkono ndoto za kuuawa rais,kwani alichaguliwa aote au atekeleze ahadi yake?aache mambo ya uana harakati wananchi wanataka maendeleo siyo ndoto.
 
Mahakama zetu zipo kwa ajili ya kulinda watawala na maslahi zao. Haki inapatikana kwa Mungu tu
 
Si mlisema Lema hahitaji kumpigia mtu magoti?

Na kwamba yeye ni aluwatani?

Kwamba kesi yake inasimamiwa na mawakili wasomi?

Kwamba Arusha kitanuka kama haki haitendeki?

Kwamba Lema ni jeshi la mtu mmoja?

Sasa hiyo haki, na aungwe mkono kutoka wapi mtu anaejitisheleza?
Wewe ni mpuuzi moja kati ya mizigo inayosumbua nchi hii.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom