God was created when the first con-man met the first fool

Na ukweli ni upi?
Ukweli ni kwamba mungu muweza wa yote na mjuzi wa yote mwenye uwezo wote aliyeumba huu ulimwengu ambao una mabaya ya kila aina hayupo, angekuwepo kusingekua na mabaya wala kutilia shaka juu ya uwepo wake
 
Waziri wako wa afya anakataza zinaa humsikii.
Wazazi wako wanakukataza zinaa husikii

Utamsikiliza Mungu usiemuona?

Waziri hana mamlaka ya kuzuia zinaa kwasababu hana uwezo wote, angekuwa na uwezo huo angeweza kuzuia bila hata kututangazia.

Pili kama tu waziri ambaye hana uwezo wote anatamani kuzuia jambo hili lisiwapate raia wake inakuaje mungu mwenye uwezo wote na upendo wote kwa viumbe vyake ashindwe kuzuia jambo hili???
 
Ukweli ni kwamba mungu muweza wa yote na mjuzi wa yote mwenye uwezo wote aliyeumba huu ulimwengu ambao una mabaya ya kila aina hayupo, angekuwepo kusingekua na mabaya wala kutilia shaka juu ya uwepo wake

Any proof? I mean, una ushahidi wa hayo uliyoyaandika hapa?
 
Si uniambie contradictions unazoziona?
Mungu muweza wa yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote aliyeumba huu ulimwengu wenye mabaya hayupo kwasababu ulimwengu unam contradict kwa uwepo wa mabaya hivyo unaonesha ulimwengu huu haujaumbwa na mungu huyu

Mungu huyu ni wakufikirika tu hayupo kihalisia
 
Mazuri ni yapi na mabaya ni yapi? Na ni standard gani unayoitumia kuamua hiki ni kitu kibaya na hiki ni kizuri?
 
Mazuri ni yapi na mabaya ni yapi? Na ni standard gani unayoitumia kuamua hiki ni kitu kibaya na hiki ni kizuri?
Magonjwa, vifo njaa, matetemeko, tsunami nk. Yote hayo ni mabaya

Na mazuri ni yale yaliyo kinyume na hapo
 
Magonjwa, vifo njaa, matetemeko, tsunami nk. Yote hayo ni mabaya

Na mazuri ni yale yaliyo kinyume na hapo
Anaeamua kipi kibaya na kipi kizuri ni nani?
Wewe au Nani.

Pharmaceutical companies wanatamani magonjwa yaongezeke wapate kuuza dawa.
Na hospital binafsi zinatamani wagonjwa waongezeke ili biashara iwe nzuri.

Mashirika na watu binafsi yanayoshughulikia Habari za VIFO na Mazishi na wao wanatamani Vifo viongezeke wafanye Biashara.

Tsunami na matetemeko yanafaidisha wengi mno tofauti kabisa na wewe unavyoelewa.

Watengeneza Silaha wanatamani vita visiishe ili wauze Silaha.

Sasa nani mwenye kuamua kipi kizuri ktk Hii Dunia ? Na nani apewe hicho anachotaka?

Au hujasikia msemo usemao "kwako kilio kwangu sherehe?

Kazi ya kipi kizuri kwetu na kipi kibaya ni KAZI YA MUNGU.
Wewe funga mkanda ujiandae tu chochote utakachopangiwa.
Hata kwenda haja kubwa wewe huna hiari kweli utaweza kujua kipi kibaya au kizuri kwako?
 
We mtoto unaelewa maana ya neno MUNGU?
Au Unaropoka tu.
Yaani wewe ghafla umeshakuwa mungu!
Teh teh teh teh.

Mnakatazwa kupiga Viroba lkn ubishi tu.
Matokeo yake ndio haya.

Wewe neno mungu unalielewaje au huyo mungu wenu hewa wa mawinguni mnaimagine anafananaje..

Au wachungaji wenu matapeli wamewafundishaje juu ya huyo mungu wenu anaeenda kutukuzwa bila hivyo anawachoma na moto wakusadikika..
 
Who made you?

Wewe umezaliwa..
Gari ndilo limetegenezwa. haya maswali mengine niya watoto wenu kuuliza..

Kibiologia wewe ni matokeo ya mbegu ya baba yako na yai la mama yako.mbona jepesi
 
Kama ilivyovigumu kwa computer yako kukufikiri na kujua mawazo yako,ndivyo ilivyokwako kumfikiri Mungu na kujua Mawazo yake. Kama ulizaliwa mwaka mfano : 1990 June,huwezikujua yaliyokuwepo kabla yake hata ukifikirije Bali aliyekuwepo kabla ndiye awezaye kukuhabalisha.

Wakiniabarisha kwa udaku wakushukiwa na roho mtakatifu bila shaka ntaajibu waondoe upumbavu wao kwanza sababu huyo roho mtakatifu hajawahi kuexist
 
Hicho ndicho walichokua wanakitaka walioleta huu upuuzi.

Wewe kuamini uwepo wa kitu ambacho hakipo unaona hupotezi muda.

Kweli wewe ndiwe mlengwa
Nitaendelea kuamini Mungu yupo hata Kama hayupo maana sipungukiwi na chochote.
 
Maana halisi ya Mungu ni kitu kinachotukuzwa kwa kuabudiwa
Sio kwamba Mungu hayupo, hata wewe pia ni Mungu. Shida inakuja vile tunavyomchukulia huyu Mungu sijui kumwabudu, kumsifu kumtolea sadaka n.k hapa ndipo tulipologwa na wazungu. Hakuna Mungu wa aina hiyo Mungu ni Mimi na wewe yaani sisi ni Mungu.
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom