Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,741
- 40,868
Mwanzoni kabisa baada ya kuchaguliwa kwa Magufuli na kazi ilipoanza nilisema kitu ambacho sidhani kama watu wengi walielewa au walidhani nasema tu kwa sababu ya ushabiki. Nchi yetu ilipokuwa imefikia kiongozi yeyote ambaye alikuwa anakuja kuupokea uongozi uliopita jukumu lake la kwanza kabisa lilikuwa ni kusafisha; kuleta nidhamu na kubwa zaidi kupambana na ufisadi kama simba mbele swala. Sidhani kama watu walitegemea shock and awe ambayo inaendelea sasa nchini na labda inakwaza watu wengi.
Ni lazima tutambue kabisa kabla ya watu kupewa majumu sasa na bajeti mpya ya nini kinaenda kufanywa mwaka wa kwanza wa Magufuli ni lazima mianya yote izibwe kwanza, viongozi matatizo wachomolewe, na fedha ambazo zililiwa au kuchomolewa zirejeshwe. Ni lazima tuelewe kwanini kuna mkazo sana wa kuhakikisha fedha zinarudishwa kabla watu hawajapelekwa mahakamani. Ni rahisi zaidi kumpeleka mtu mahakamani kuliko kumfanya arudishe fedha!
Ni kweli itauma, ni kweli tutashangaa "duh" na wakati mwingine tunaweza hat akuhisi "eeh mbona anamgusa na huyu" lakini kama nilivyosema wakati ule "tengua tengua" bado ipo,, inakuja na hadi hivi sasa sidhani kama hata robo ya uchafu ulioharibu taifa letu umeshughulikiwa. Litagusa hata watu tunaowaheshimu au kuwapenda lakini tuliposhangilia aliposema "atatumbua majipu" tukumbuke hakusema majipu ya wengine tu! Au majipu ya maadui zetu tu. Yakianza kutumbuliwa ya nyumbani mwetu, marafiki zetu, jamaa zetu kama nilivyosema wakati ule tugune tu lakini ndiyo hivyo; "hakuna namna nyingine".
MMM