Mechi ya leo saa 08:00 mchana huu ya Kilimanjaro Stars (Tanzania) dhidi ya Burundi katika Senior Challenge Cup ni muhimu sana sio tu kwa michuano hiyo lakini pia kwa FIFA World Rankings! Hivi sasa katika eneo hili la EAC sisi TZ tupo namba 124 tukiwa nyuma ya Waganda (86), Warundi (112), Wajivuni (117)--tukiwa juu ya Wanyarwanda tu. Kwa hiyo mechi ya leo ina umuhimu mkubwa kwetu ili itupandishe chati ya FIFA. Inatakiwa walio karibu na vijana hivi leo (au TFF for that matter) wawaeleze vijana kuhusu umuhimu huo. Go go boys!!