GMO Maana yake nini? na je tunahitaji hiyo GMO?, nasikia ipo kwenye mafriji yetu.

KIDUNUNDU

JF-Expert Member
Dec 3, 2012
1,148
2,129
Kuna shida ya chakula duniani na wataalamu wanajaribu kushinda hiyo vita kwa kutumia tekinolojia inayoaminika kuwa itafanya vyakula viwe vingi na uzalishaji wake uwe mwingi. Je Africa kama bara ikiwa imebarikiwa ardhi yenye rutuba na pahala pengine pana ardhi ambayo haijawahi tumika , je inahitaji hii tekinolojia leo, na nini madhara yake?.
 
Mkuu GMO,ni kifupi cha maneno ya Kiingereza-Genetic Modified Organism,kwa kweli Bidhaa yoyote itokanayo na Teknolojia hii inakuwa ni Hatari sana kwa Afya kwani hupelekea matatizo mengi km vile Cansa,Matatizo ya Kijenetiki,nk.Hivyo kwa Serikali yetu kupitia Wizara ya Kilimo,Idara ya Afya ya Mimea ktk Sheria inayojulikana km Plant Protection Act of 1997,No-13,Inazuia uingizwaji na Uuzwaji wa Mazao au mimea iliyozalishwa kwa Teknolojia hiyo.
 
sikuhizi kuna hadi genetic modified people... hadi humu jf wamo wengi tu!
 
We hushangai mazao kumea ndani ya miezi mitatu skuiz,miti ya matunda inakuwa na kutoa matunda ndani ya mwaka mmoja hadi miwili unadhani kuna maajabu gani yefanyika hapo,geneticaly modified seeds tayari zinatumika bongo kutengeneza geneticaly engeneered crops,nshasikia kwenye matangazo wakizinadi mbegu za monsanto ambao ni moja ya ma pioneer wa GE seeds.
Naona tusubiri waje wataalamu wakilimo watuelezee vizuri
 
Back
Top Bottom